Mikopo ya kausha damu ipo mtaani, tuwe makini

Mikopo ya kausha damu ipo mtaani, tuwe makini

Mliokopq pesa x nipeni mbinu mana nina line za wana wawili ambazo ni extra hata zikizimwa miezi miwili sawa na yangu ikiwemo wataweza nitafuta kwenye nini tena nikizma line.
 
Kutokujua kwetu sheria ndio sababu majambazi hao wanaojiita wakopeshaji wanakuwa na nguvu.

Mtu pekee anaeruhuisiwa kuchukua samani yako ni yule aliekuuzia samani hiyo kwa mali kauli (Hire purchase) na ukashindwa kupeleka marejesho. Kinyume na hapo mdai yeyote mwingine ni sharti afuate process za kimahakama.

Alichofanyiwa huyo dada ni uvamizi, ana haki ya kufungua kesi na hata kudai fidia. Anaweza hata kusema katika vitu walivyochukuwa kulikuwa na kiaisi cha fedha.

Wabongo pia ni wavivu sana kusoma mikataba. Unapokuwa na shida ya pesa, unasaini chochote utakachopewa bila kusoma. Kumbe umesaini uhai wako kwa walaghai wa mjini.
nenda kakope halafu usilipe uone!
 
kuna mmoja nimeona fb juzi unalipwa masaa 24 hahuitaji dhamana nkawacheki he wanataka nitume 25k ya kujiunga si unikate huko...akagoma.... nkawaza waleeee wanataka kurudisha hela zaooo..nkazima simu nkatoa betri kama masaa mawili nkarudisha nkasema ahsante mola nimekoma nao sirudi tena
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji106]
 
Mkuu ni kama umenikumbusha vile,nipo safarini naenda wilaya x,mala paa naona msg ikisema una mfahamu furani Nini Fulani? Sikujibu msg,mara akapiga. Haloo unaongea na Afisa mikopo kutoka kampuni ya KOPA FASTA, unamfhamu furani bini furani nikasema ndio namfahamu Kuna Nini? Akasema uyu ndugu alikopa Katika kampuni yetu na ajalipa na tukimpigia simu apokei.Mimi nikamuuliza je namba yangu umenipata wapi? Akasema wakati anajaza mkopo online aliweka namba Yako kama mtu wa karibu.Kwaiyo mpigie simu mwambie alipe mkopo. Kilichonikela ni huyu ndugu yangu kutumia namba yangu kukopea pasipo kuniambia,nimempigia simu kumuuliza analeta maneno kibao Yani nime mmaindi kinoma [emoji12][emoji12][emoji12][emoji12] Nimemwambia alipe deni haraka..Dahhhhhh .Kausha damuuuuuuu ni hatariiii.
Na wewe ni ndezi kwanin umaind wakati hawana uwezo wa kukufanya lolote
 
Wana message za vitisho hao hadi kwa wazamini
Mdhamini wangu Ni kitambulisho Cha NIDA , nimehama mji na kubadilisha laini.
Mwanzoni walipiga simu Sana Hadi wakani refer kwa debt collector, nikaona kumbe hii laini na huu mji ndivyo wanavyojua. Nimehamia mwanza mtaa wa Nyerere naishi kwa amani.
Sitaki mikopo Yao Tena.
 
Mdhamini wangu Ni kitambulisho Cha NIDA , nimehama mji na kubadilisha laini.
Mwanzoni walipiga simu Sana Hadi wakani refer kwa debt collector, nikaona kumbe hii laini na huu mji ndivyo wanavyojua. Nimehamia mwanza mtaa wa Nyerere naishi kwa amani.
Sitaki mikopo Yao Tena.
Kwani wanaweza kutrack location kupitia namba ya simu kukukamata?? Mimi wananidai 27000 pamoja na penalty wakibip nawaambia wasubiri subiri
 
Siku hizi wamestukia namba, wanataka nida na mdhamini, unapoishi , mjumbe na mwenyekiti wa serikali za mitaa. Ukiwapa hivyo huchomoki.
ndichoo kilichomkuta mjumbe wangu mdada alikwenda kwa mjumbe kumsaidia karatasi za kuonyesha mwenyeji alafu anadaiwa ajifiche we mjumbe kachukua fimbo kasoogeza pazia yumoo kamdanganya toka usiwe na wasi wasi awafanyi chochote ,,,,,,,
wajumbe si wa tu wa zu ri walah
 
Dawa ya deni kulipa

Kuna jamaa alikopa hela kwa kausha damu. Akawa halipi marejesho na riba ikaja kuwa kubwa mno kushinda fedha alizokopa. Jamaa wale wakamtafuta na kumtia ndani. Mkopaji aliwekewa dhamana siku ya pili na akina kausha damu wakamfungulia mashitaka. Kuona hivyo na jamaa akaenda kufungua kesi ya kuwashitaki kausha damu kuwa wanafanya biashara ya fedha bila kulipa kodi serikalini. Kausha damu nao wakakamatwa na kufunguliwa mashitaka. Kuona hivyo kausha damu wakaenda kufuta ile kesi ya mkopaji na kukimbia kusikojulikana. Mkopaji naye akaenda mahakamani akafuta kesi. Kwa hiyo hapa ni kuwa DAWA YA MOTO NI MOTO.
 
Back
Top Bottom