Kuna jamaa alikopa hela kwa kausha damu. Akawa halipi marejesho na riba ikaja kuwa kubwa mno kushinda fedha alizokopa. Jamaa wale wakamtafuta na kumtia ndani. Mkopaji aliwekewa dhamana siku ya pili na akina kausha damu wakamfungulia mashitaka. Kuona hivyo na jamaa akaenda kufungua kesi ya kuwashitaki kausha damu kuwa wanafanya biashara ya fedha bila kulipa kodi serikalini. Kausha damu nao wakakamatwa na kufunguliwa mashitaka. Kuona hivyo kausha damu wakaenda kufuta ile kesi ya mkopaji na kukimbia kusikojulikana. Mkopaji naye akaenda mahakamani akafuta kesi. Kwa hiyo hapa ni kuwa DAWA YA MOTO NI MOTO.