Mikutano imeanza bila kuwa na hoja za kuitikisa Serikali ya Rais Samia

sasa mkuu si uanzishe mikutano yako ya hadhara na uwe na hoja zako za msingi
 
Kumbe alitaka apokelewe na weMbo
 

Kumbe anasubiri nini kutoa hilo ghala?
 
Unakatwa na misukule
 
Mfumuko wa Bei wa mbolea haukusababishwa na serikali ya CCM Bali ulikuwa Ni mfumuko katika soko la Dunia,Ndio maana unaona serikali ikiwekeza mabillioni ya Ruzuku ili kumtua mzigo mwananchi
Unayajua makato yanayokatwa wakati wewe unanunu mafuta ya magari?
 

Tukadhani:

1. Mama hana uungwaji wowote mkono kwenye huku alikotufikisha na hali hii ya maisha, ikiwamo bei za vyakula ambazo sasa ni za juu mno.

2. Mama hana uungwaji mkono wowote kuhusiana na wingi wa tozo na kodi kwa watu.

3. Mama hana uungwaji mkono wowote kwenye matumizi na utumbuaji wa kufuru unaofanywa na walioko madarakani, almaarufu walamba asali.

4. Mama hana uungwaji mkono kwenye lolote jipya kwamba kuna tumaini la kuirekebisha hali iliyopo.


Labda wewe unamwunga mkono kwenye yapi au lipi?
 
Suala la Bei za vyakula ningependaa kukwambia kuwa lazima utambue kuwa kilimo Ni biashara ,na siku zote hakuna anayeipenda kupata hasara katika biashara yake,kwa miaka mingi Sana wakulima licha ya kufanya kazi kwa bidii na kwa kuvuja jasho lakini walikuwa hawanufaiki na jasho lao kwa kuwa waliofaidika na jasho lao walikuwa vimvulini,Rais Samia kwa kulitambua Hilo akaona kuwa hiyo siyo haki kwa kuwa kila mtu Anastahili kuheshimiwa katika kazinyake na kupata kile anachostahili kulingana na juhudi zake,kwa kuwa wakulima walishuhudia wakipangiwa Bei na mahali pa kuuza mazao yao licha ya kuwa walikuwa wakuingia gharama kubwa za uzalishaji,Juhudi hizi za mh Rais zimeleta Tabasamu Katika Mioyo ya wakulima ,ambao kwa Sasa wanamuunga mkono mh Rais na kuahidi kumlipa kwa kumpigia kura za kishindo uchaguzi ujao

Suala la tozo ,ningependaa irejee utafiti uliyoonyesha namna watanzania wanavyoiunga mkono suala Hilo,kwa kuwa wanatambua kuwa ili tupate huduma Bora za Afya ,Elimu ,maji Safi na salama,n.k Ni lazima kila mmoja wetu achangie kulingana na kipato chake,lakini kila mtanzania mwenye akili timamu anatambua kuwa maendeleo hayaji kwa miujiza pasipo kufanya kazi na kujitolea ,ndio sababu ya mh Rais Kuendelea kuungwa mkono na mamillion ya watanzania katika suala hilo
 
Huteuliwi ng'o !!!!
 

Unaelewa suala la bei za vyakula linaletwa hapa kwa maana rahisi ya kuonyesha mfumuko wa bei ulivyopitiza?

Unajua mfumuko wa bei huu unatokana sana na bei za mafuta ya diesel na petrol kupanda mno? Kumbuka sekta zote za uzalishaji zinahusisha nishati hii.

Unaelewa tozo na kodi kiasi gani zilizomo kwenye nishati hii?

Unajua walamba asali hauwahusu mzigo wa kodi na tozo lukuki tunaoubeba sisi kimakato wala kimatumizi?

Kumbe wewe unadhani kwenye mfumuko huu wa bei kuna awaye yote asiyekuwa mlamba asali mwenye kushangilia?

Tambua kuwa kwenye mfumuko huu wa bei hayupo mmoja mwenye kushangilia. Kukuthibitishia hilo itisheni mkutano mjaribu kuuhalalisha, mtaupata mrejesho.

Mfumuko wa bei hudhibitiwa. Waliopo kwetu ndiyo hawa wenye magari ya 400m/- plus na bila ya aibu huku kodi haziwahusu. Matanuzi ya hivi hata beberu tunakokopa na kuomba Kila leo hana!
 
Njoo ufanye mkutano wa hadhara huku nyanda za juu kusini uwaambie wakulima na wananchi kuwa wawaunge mkono kwa kuwa Bei ya mahindi Yao na Mchele watahakikisha kuwa vinashukaa Bei,majibu watakayokupa uje uyalete hapa
 
"Mfano suala la mfumuko wa Bei watanzania waliona namna serikali yao ilivyofanya juhudi katika kukabiliana nalo ,mfano katika mafuta serikali ilikuwa ikitoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi"

Lucas mwashambwa !

Ebu niambie nikuelewe!

Sasa...pamoja na hayo mabilioni ambayo umeyataja,kuwa yamewekwa kama Ruzuku,ili kuokoa au kushusha mfumko wa bei...

.....inakuwaje kwamba bado bei ziko vilevile kwenye Masoko,Maduka na Mabucha?

Au unatuambia kwamba Sania Anatoa Ruzuku!

Halafu Mwigulu Anaficha bila kuziweka kwenye Mzunguko!

Wananchi wanahitaji kuona matokeo,ya kile kinachotamkwa na serikali.

Halafu pia!
Lucas mwashambwa

Unapaswa kuelewa kitu kimoja hapa!

Serikali inapoweka Ruzuku kwenye mbolea au Mafuta,halafu "Tozo" ikawa Palepale!

Umeme ukaendelea kuwa tatizo Sugu....

Bado tatizo linakuwa halijatatuliwa!

Sababu ni sawa na kutoa pesa mkono wa kulia na kuziham8shia mkono wa kushoto!

Serikali inakuwa inawakaamga watanzania kwa mafuta yao yenyewe!

Soma hiyo na uache mapambio mengi,wakati watu wanashindia mlo mmoja majumbani.

Kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima,halafu ukafungua mipaka na kuruhusu wageni wakiingia nchini na kufanya ulanguzi wa Mazao kiholela mashambani kwa hao wakulima!

Badala ya wageni kuishia kwenye Masoko ya kimataifa ya mazao!
Ambayo yalianzishwa kimkakati,ili pamoja na kuweza kutumia bei elekezi,lakini pia serikali ingekata kodi yake na pia kuongeza pato la Taifa.

Sasa inakuwa kinyume chake!
Hiyo Ruzuku,inawanufaisha Wakongomani,Wakenya,Wanyarwanda na pia mpaka Sudan kusini wananufaika na chakula kitokanacho na mbolea ya Ruzuku iliyokusudiwa kumuinua mkulima wa Tanzania.

Nasema hivyo kwa sababu,nimeshuhudia wakulima wakiuza mazao yao kabla hata ya kuvunwa mashambani.
Hii ni kutokana na mazingira magumu ya kipato,na uhotaji mkubwa wanaokuwa nao kwenye suala la Raslimali Pesa.
 
Mungu ibariki tanzania mungu ibariki CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…