Majibu Yangu kwako....
Lucas mwashambwa
Nimeamua kuanza, kwa kuziweka hoja zako!
Sambamba!
ili twende hoja kwa hoja!
Wasomaji pia mniwie radhi kwa hilo,ila ni vizuri kupambanua!
"Lucas mwashambwa, post: 45119830, member: 674699"]Asante mkuu kwa maswali yako,ningependaa kukujibu kuwa katika uwekaji wa pesa za Ruzuku uliofanywa na serikali ya Rais wetu mpendwa mama Samia ilileta tija Sana mfano katika mbolea kabla ya Ruzuku mbolea ya DAP ilikuwa inapatikana kwa laki moja na 40 lakini msimu huu mbolea hiyo hiyo Ya DAP inapatikana kwa Elfu 70 tu,je huoni hapo kuwa imeleta tija? Huoni kuwa mkulima kapunguziwa mzigo wa Bei? Huoni inamsaidia mkulima kumudu Bei?
Suala la kutokufunga mipaka nalo ningependaa nikujibu kuwa lazima utambue kuwa kilimo Ni biashara na ufungaji wa mipaka miaka yote Ndio umekuwa ukimdidimiza mwananchi au mkulima kiuchumi na kubakia katika dimbwi la umasikini licha ya kuhenyeka Sana na jembe lake begani lakini mkulima amekuwa anashindwa hata kujenga nyumba Bora na hata kumuda gharama za Mahitaji mengine kutokana na kunyonywa katika Bei kwa kupangiwa Bei na mahali pa kuuza.
Ilichokifanya na I achokifanya serikali yetu shupavu na madhubuti chini ya uongozi Mahiri na imara wa mama Samia ni kuhakikisha kuwa inatunza chakula Cha kutosha katika maghala yake na kupeleka sehemu zenye uhitaji kwa Bei nzuri,suala kuwa watu wanaingia Hadi vijijini na kuiokosesha serikali Kodi ningependaa kukujibu kuwa huwezi ukasafirisha mahindi bila kulipia ushuru kutoka katika eneo husika nakufika mbali,fedha hizi za ushuru zimekuwa chanzo kizuri Cha halmashauri nyingi hasa huku kwetu nyanda za juu kusini na kusaidia katika Uendeshaji Wa shughuli mbalimbali Kama vile utolewaji wa huduma za kijamii Kama vile ujenzi wa shule, zahanati, Barabara, usambazaji wa maji Safi na salama n.k
Nitakujibu vizuri sana kesho asubuhi panapo majaaliwa!
Kada Mtiifu
Lucas mwashambwa !
Kwa uwezo wake Mola!...hatimae
Asubuhi njema imewadia nikiwa wa afya njema.....
Naomba nikujibu kama nilivyoahidi hiyo jana!
Nianze na Mbolea ya "DAP" kuwekewa Ruzuku na hivyo kushuka bei kutoka 140,000/= kwa mujibu wa taarifa yako!
Na kushuka hadi 70,000/=
Pamoja na hatua hii kuwa nzuri kwa mkulima,wewe hupaswi kuitumia sasa hivi kuiita mafanikio!
Kwa sababu ndio kwanza imeanza kutekelezwa,na mafanikio yake,yatategemea ufanisi wa maafisa ugani huko vijijini,kama watafanikiwa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuitumia kwa ufanisi.
Na impact yake itayegemea pia na muenendo wa ms8mu wa upatikanaji wa mvua!
Kuanzia mwaka ujao.....
Halafu pia uelewe,hiyo ruzuku,imekuja baada ya huyo huyo mkulima kukatwa Tozo kibao,na kumdidimiza kimapato kutokana na ititiri wa Tozo na Ushuru wa Halmashauri.
Lakini nikukumbushe tena! uelewe kwamba hoja hapa ni nini kimepelekea maisha ya watanzania kuwa ya shida,ghafla baada ya utawala wa Samia kuingia Madarakani??
Kuhusu ufunguaji mipaka holela!
Umesema kwamba,"mkulima sasa ananufaika na bei sahihi ya mazao yake!"
Huo ni Uongo tena wa kiwango cha hali ya juu!
Mkulima hanufaiki chochote na hizo bei,wanaonufaika ni walanguzi wanaolangua mazao kinyela mashambani tena saa ingine kabla hata ya kuvunwa!
Na hao wakulima kwa sababu wana uhitaji mkubwa wa Pesa!
Wanajikuta wanauza mpaka akibavyao binafsi ya chakula!
Hivi tunapiandika humu JF, mojawapo ya kundi kubwa linalotaabika na maisha haya ni hao hao waliouza npaka akiba yote ya chakula!
Na pia uelewe,bei kubwa ya chakula,haitaweza kumnufaisha chochote mkulima,endapo utitiri wa kodi,Tozo na ushuru wa halmashauri hautaondolewa na kubaki kodi walau moja tu ya halali.
Kwamba halmashauri zinajenga miradi ya Maendeleo kupitia ushuru wa mazao,ni uongo mtupu!
Huko ndiko chaka la wezi limejikita,halmashauri ndio kikwazo kikubwa cha Maendeleo ya nchi hii.
Na kila siku wakurugenzi wa halmashauri hizi,wanaendelea kukamatwa sababu ya ubadhilifu nchi nzima!
Pesa zinazojenga hiyo miradi,kwa mujibu wa serikali yenyewe!
Zinatokana na Mikopo!
Fedha za misaada ya Uviko!
Tozo tunazokatwa muamala!
Kodi ya mapato!
Huko halmashauri wamejaa sampuli ya wewe,wanasifu ili mafunhu yaende!
Halafu wanajua jinsi ya kupiga!
Kuhusu Serikali kutunza chakula kwenye maghala!
Hili nalo linaonyesha ni jinsi gani,serikali isivyo na watendaji wenye weledi.
Haiji akilini kwamba,seriksli inajivunia kuhifadhi chakula kwa mamilioni ya tani.
Wakati huo huo,inashindwa kuitoa sasa hiyo akiba,ili iwasaidie wananchi,ili kushusha bei ya mfumko inayoendelea kuwaumiza wananchi.
Na huenda huko serikalini viongozi wana nunua na kuneemeka na hiyo akiba ya chakula,wakati sisi tukihenyeshwa na walanguzi.
Maana kwa Tanzania hii,viongozi madishi yao yameangalia matumboni zaidi.
Kama unabisha....tutajie ni wapi serikali imepeleka chakula mpaka sasa,ili kujaribu kunusuru mfumko wa bei masokoni?
Kuhusu huduma za kijamii!
Hapa Serikali inaweza kujisifu kwa kujenga miundombinu ya najengo ya mashule,mahospitali na zahanati!
Lakini Wananchi wanacholilia ni uduni wa hizo huduma,ambazo zinatolewa ndani ya hayo majengo!
Mashuleni wanalilia kiwango duni cha Taaluma!
Wanalilia kiwango Duni cha vifaa kazi ya ufundidhaji kwa walimu,ikiwemo pia maslahi duni kwa walimu!
Walimu ndio watum8shi ambao ni wahamga wakubwa wa mikopo na madeni nvhi hii!
Mahospitalini!
Huko wananchi wanalilia gharama kubwa za matibabu ndani ya nchi hii,kwamba mtu anatibiwa kulingana na salio lililopo,salio likikata na Uhai pia unakuwa hatarini kukatika.
Tunashuhudia ufisadi mkubwa kupitia Bima za afya nchini.
Tunashihudia wizi wa madawa ya wagonjwa mahospitalimi tena waziwazi mchana kweupe!
Kila daktari kwa asilimia kubwa,anamiliki aidha Pharmacy au ka- Dispensary kake.
Pale hospitali ya Umma alipiajiriwa,yeye anapageuza kituo cha kutafutia wateja.
Pamoja na kuiba Dawa kuoeleka kwake!
Nimekujibu kadri ya ulivyoandika mwenyewe
Lucas mwashambwa !
Tunaishi na Tunashuhudia pia!
[/QUOTE]
Nashukuru kwa kunijibu,ngoja nami nikujibu Kama ifuatavyo.
Kuhusu mbolea za Ruzuku kumnufaisha mkulima ningependaa kukwambia kuwa manufaa yake sisi wakulima tunaayaona hasa muda huu ambapo mahindi yamekuwa na yameanza kutoa mbelewele,suala la Hali ya Hewa Ni suala lingine ambalo Ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuhusiana na mvua kunyesha ama kuchelewa kunyesha lakini serikali yenyewe imetekeleza wajibu wake katika kumuwezesha mkulima kupata mbolea kwa Bei nafuu.
Kuhusu mkulima kutokunufaika na Bei na kwamba anayenufaika ni mlanguzi ningependaa kukujibu kuwa Mimi Ni mkulima nipo mkoani huku na ninacho kueleza naeleza kitu nachokijuwa kwa uhakika ,Napenda kukwambia kuwa Tangia msimu uliopita Bei ya mazao ilikuwa Ni nzuri Sana Tangia wakati wa mavuno ambapo mkulima alipata kuuza mazao yake kwa bei nzuri tena kwa kuchagua amuuzie Nani mwenye Bei nzuri,Hali hii haikuwepo miaka iliyopita kwani wakati wa mavuno Bei ilikuwa inakuwa mbaya Sana na ya chini Sana iliyopelekea mkulima kupata hasara kubwa Sana ukilinganisha na gharama alizottumia katika uzalishaji.
Suala la ushuru na Kodi,Ningependaa kukujibu kuwa huwezi ukafuta kila ushuru na kila tozo au kila Kodi kwa kuwu Hakuna nchi Duniani ifanyavyo hivyo,kwani ili tupate huduma Bora za kijamii Ni lazima serikali ikusanye Kodi,tozo,ushuru n.k nakutumia kwa Nidhamu katika kuwekeza kwenye kuwaletea maendeleo wananchi,ndio maana serikali inafuta unapoona panafaa kufanya hivyo baada ya utafiti wa kiuchumi kutathimini athari zake kiuchumi.
Suala la ubadhirifu katika halmashauri,ningependaa kukujibu kuwa serikali ya mama yetu shupavu Jasiri imara na shujaa haina mzaha katika kila Senti ipatikanayo kwa kila mwenye kujaribu kugusa pesa za umma,ndio maana umeona wakurugenzi mbalimbali wakifishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya Fedha za umma,kuondolewa madarakani na kubanwa kisheria.
Kuhusu huduma mahospitalini,Ningependaa kukujibu kuwa serikali yetu ya mama Samia imefanya juhudi kubwa Sana katika kuboresha huduma za Afya hapa nchini ikiwemo kujenga vituo vya Afya,usambazaji wa madawa ,vifaa Tiba na kuajiri wataalamu kwa kadri Hali ya uchumi unavyoruhusu Kama ambavyo tuliona mwaka Jana namna serikali ilivyoajiri wataalamu wengi wa kada ya Afya.