Mikutano ya hadhara imeruhusiwa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kudhihaki Magufuli?

Mikutano ya hadhara imeruhusiwa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kudhihaki Magufuli?

Nimefuatilia mikutano ya chadema kila kona ya nchi inaonekana mikutano hiyo ni mbinu za ccm kumchafua magufuli na wananchi wahisahau au wasitambue ufisadi unaoendelea nchini
Ninaomba michango yenu

Kama unampenda sana nenda kanywe nae chai - JK Nyerere

Kama unampenda sana nenda chato ukazikwe nae - Zitto
 
Ndo muda, km ulivyosema wameruhusiwa. Acha waseme ambayo walikosa pakuyasemea kwa miaka zaidi ya 7 Sasa. Yakiisha wataacha tu kuwa mvumilivu.
 
Magufuli kinguvu alijichagua kuwa rais, akaona haitoshi akatuchagulia wabunge (hadi wabunge wa viti maalum kutokea CHADEMA), madiwani, wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji. Hivi mtu wa namna hiyo, leo hii akisemwa vibaya, kutakuwa na tatizo?
 
Hawatoweza kufanya tumsahau kiongozi ambaye,

1. Alisaidia wafanyabiashara wadogo kufanya biashara Kwa uhuru.

2. Bandari ya dar iliongeza Kasi kiutendaji, mzigo ilitoka bila zengwe.

3. Ndugu zetu waliheshimika walipoenda kujifungua hospitali, hawakutukanwa kama Leo.

4. Alifanikiwa Kwa kiasi kikubwa kuwatisha waizi wa Nchi hii.

5. Bosi yule mpenda TEMBO alipofichwa TEMBO waliokuja Hadi mjini bila HOFU.

6. Wanyama hai hawakuuzwa nje.

7. Mabilionea wazawa waliongezeka.

8. Samaki ziwa Victoria waliongezeka baada ya kudhibiti uvuvi haramu.

9. Majambazi walihamia Nchi Jirani kumuhofu uncle.

10. Maalbino hawakuwindwa kama swala mbugani.

11. Umeme haukukatwa.

12. Watoto pendwa walitimuliwa wakabaki kupika majungu na kuchora vikatuni.

13. Tuliheshimika Africa nzima kupatikana mwana Africa mwingine.

14. Alichukiwa na vyama vya upinzani, Alichukiwa na Chama chake CCM, bt alipendwa sana na wananchi MASKINI.

15. Tulinunua Mchele 800 per kg ktk uongozi wake.

16. Alizuia LOCKDOWN ambapo majirani walitaabika Kwa njaa enzi za CORONA ya mchongo.

17. Hakusafiri kutembeza bakuli kuomba msaada Kwa majirani.

18. Alisaidia kutatua foleni ktk Jiji la Dar.

Magufuli Abarikiwe huko aliko.
 
Magufuli kinguvu alijichagua kuwa rais, akaona haitoshi akatuchagulia wabunge (hadi wabunge wa viti maalum kutokea CHADEMA), madiwani, wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji. Hivi mtu wa namna hiyo, leo hii akisemwa vibaya, kutakuwa na tatizo?
Ndio lipo tatizo kwa sababu ameweza kufanya yote hayo kwa sababu ya ccm na hadi sasa serikali iliyopo madarakani imetokana na huko kujichagua kwa nguvu Magufuli hadi hao wabunge bado wapo bungeni hata wale covid 19 bado wapo, na ccm hawako teyari kubadili chochote katika hayo.

Ccm watamsema Magufuli kwa mengine ila hayo ya uchaguzi hukuti wakimsema Magufuli kwa huo uchaguzi.
 
Kama tunajamii toxic namna hii tunasafari ndefu sana kama taifa yaani haki ya kikatiba ya vyama vya siasa kufanya siasa huru mtu saivi anawaza habari za kuchafuana

Yaani kama mtu ni mchafu ni mchafu tuu kama ni msafi ni msafi tuu watu wanajivika upofu na kuchagua nani wa kumuhukumu kwa kuangalia mkosaji zaidi

Sio samia sio magufuli wote ni wale wale na ndio maana hakuna kilichobadilika tangu na tangu kikubwa tuishi kwayale machache mazuri yaliyofanywa na yanayofanywa
 
Nimefuatilia mikutano ya chadema kila kona ya nchi inaonekana mikutano hiyo ni mbinu za ccm kumchafua magufuli na wananchi wahisahau au wasitambue ufisadi unaoendelea nchini
Ninaomba michango yenu
Ndugu peno hasegawa mbona unaonekana kupagawa na kukosa UFAHAMU wala UELEWA wa haki zako za kisheria na kikatiba ndani ya nchi yako?

Shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na maandamano yako tangu enzi na enzi kwa mujibu wa katiba ya JMTbp - 1977 na sheria zilizotungwa baadae.

Huu ni uhuru na haki za kisiasa za raia wa Tanzania. Kwa hiyo, acha wazifurahie kwa namna hiyo..!

Wewe kama shida yako ni "kudhihakiwa Kwa Magufuli", jikite hapo na wanaJF watakusaidia kukujibu na kukuelimisha bila shaka..

Otherwise, stop being hypocrite because of your ignorance..!!
 
Yaani mikutano ya Chadema iwe ni mbinu ya CCM ya kumnanga Magufuli? peno hasegawa ni akili zako hizi au umevuta harufu ya mavi somewhere?

Mnamsema Mbowe ameramba asali kwa kumsema Magu, je uyo wa ugenini aliyesapa juzi bila baraka za mwenyekiti wake pia ameramba asali?


Siasa ni sayansi, SSH kwenye ili kuruhusu mikutano ya kisiasa ame'score 95% siasa za Kitanzania ili ku'win trust ya vyama pinzani.
2025 upinzani unapigwa mapema kwenye masanduku. SSH mental wake wa siasa ana balaa saaaana.
 
Ukishakuwa kibaraka hauna njia!
Yaani ukiamka unapewa kabrasha ya nani kumtuhumu au nini umtuhumu....inasadikika? kuna mmoja ana kabrasha kibao anatembea nazo kati ya mihadhara na ulaya...?.

Mabeberu wana kila aina ya sababu za chuki dhidi ya Hayati Rais, waulizeni vibaraka wao humu.
 
Nimefuatilia mikutano ya chadema kila kona ya nchi inaonekana mikutano hiyo ni mbinu za ccm kumchafua magufuli na wananchi wahisahau au wasitambue ufisadi unaoendelea nchini
Ninaomba michango yenu
Akizushiwa mambo ya uongo ambayo hakuyafanya fungua kesi mahakamani, hakuna anayemchafua mbweha yoyote bali ukweli ndiyo unaosemwa. Jiwe kila aliyeteseka na udhalimu wa utawala wake lazima atayaongelea mateso aliyopitia na ukweli ni kwamba Muhutu yule katesa, kapora, kateka, kaua na kadhulumu wengi sana.
 
Toka huo ukweli uanze kuwekwa wazi wananchi wameupokeaje?
Vizuri mno na bado wanaendelea kuupokea yaani shauku yao haiishi ndiyo maana unaendelea kumwagwa hadharani, this is a piece of an iceberg.
 
Back
Top Bottom