Milango minne ambayo haijawahi kufunguliwa

Milango minne ambayo haijawahi kufunguliwa

wangezitia moto tu. kulikuwa na haja gani ya kuendelea kuhifadhi kitu ambacho hutaki watu wajue?
Ndio puzzle lenyewe mkuu... Zamani watu walipenda kuzikwa au kuzika nyaraka zao za siri... Tofauti siku hzi hizi tamaduni hazipo na teknolojia imekua sana.
 
Umeandika vyema sana mkuu, hapo kwenye Taj Mahal, nilipata nafasi ya kutembelea mahali hapo mwaka huu, ni moja kati ya kivutio kikubwa sana huko India, na hilo jengo ni marble haswaa iliyonakshiwa kwa michoro iliyochongwa na wahunzi kwa weredi na ustadi wa hari ya juu.
Kuingia katika hilo njengo, mlangoni mnapewa kama mifuko ya kufunika viatu ili uweze kuingia kwa ndani na kwa juu kabisa ndiko kuna makaburi mawili tu, yaani kaburi la Shah Jahan na mkewe, ! Wakati wa usiku, jengo hilo linang'aa kutokana na vito vilivyonakshiwa kwa utadi. Sehemu hiyo inalindwa sana na wanajeshi wa nchi hiyo. Asante sana kwa uzi mkuu, umefanya nikumbuke mbali.
Karibu sana mkuu.... Nimefurahi kupata witness na ni kati ya majengo ninayotamani kutembelea sana kujionea uzuri na kujifunza mengi zaidi....niliangalia show moja ya mwanamuziki nguli wa ala YANNI alifanya performance yake kwenye ground ya huo mjengo muda wa usiku ilikuwa maridadi sana.
 
Kuna milango hapa duniani kwenye maeneo ya kihistoria kwa miongo au karne kadhaa haijawahi kufunguliwa. Swali linakuja ni kwanini? Imezoeleka unaweza kufungua mlango wowote utakavyo, lakini kiukweli kuna ambayo imepigwa kofuli au kuzibwa kiasi cha kwamba haifunguki kabisa. Pia haijajulikana kama kuna mali za thamani au siri/maajabu au historia yeyote iliyohifadhiwa nyuma ya milango hiyo.

Tuangalie milango minne ambayo haijawahi kufunguliwa na kujulikana kilichomo ndani yake.

1. THE TAJ MAHAL
View attachment 1153730

Hili jengo lipo India na inasemekana kuwa ni kati ya jengo zuri sana hapa duniani. Shah Jahan alianza ujenzi kwenye miaka ya 1631 kwa ajili ya kumuenzi mke wake wa tatu ambae alikuwa anampenda sana na walidumu kwa miaka 19,ila bahati mbaya alifariki wakati anamzalia mtoto wake wa 14! Shah Jahan alihuzunishwa sana na kuondokewa na kipenzi chake na kuamua kumuwekea kumbukumbu kwa jengo la Taj Mahal.
View attachment 1153735

Ujenzi wake uligharimu tembo 1000, vidume 20,000 na miaka 20 kumaliza ujenzi wake. Usanifu wa jengo hili ni wa kipekee kwani lina minara yenye mita 40 urefu na zimelizunguka jengo hilo kama linavyonekana hapo juu. Tukirudi kwenye mada kuu, Taj Mahal ina vyumba ambavyo havijawahi kufunguliwa kuna nadharia kadha wa kadha juu ya vyumba hivyo. Moja, wanadai ujenzi wake mkubwa umehusisha marbles ambazo hubadilika na kuwa calcium carbonate kama vikiwa wazi na kuruhusu carbon dioxide kuingia, maana hiyo litatengeza nyufa. Pili, ni Mumtaz Mahal mke wa Shah Jahan kuwa alizikwa ndani ya Taj Mahal wayetezi wa nadharia wanasema mwili wake umehifadhiwa kwenye sakafu ya chini kabisa (basement) ya jengo hilo na kwenye hali ile ile aliyokuwa nayo wakati anafariki.

2. THE GREAT SPHINX OF GIZA
View attachment 1153738

Hii ni kati ya sanamu kubwa kabisa kuwepo hapa duniani ina urefu wa takribani mita 19,upana wa mita 73 na kimo cha mita 20. Kulingana na wanahistoria mbali mbali hii sanamu imejengwa miaka 4500 iliyopita. Sanamu ina kichwa chenye taswira ya mwanamke na umbo la simba kama inavyoonekana hapo juu. Ilichukua vidume 100 ndani ya miaka 13 kukamilisha ujenzi huu. Wajenzi wake walikuwa wanatumia nyama za mbuzi na kondoo tu. Kwa kutumia kifaa kinachoitwa seismograph cha kurekodia mitikisiko ya dunia hasa matetemeko hivyo kutumia kifaa hiki waligundua umbaki wa mita 7.6 kwenda chini kuna chamber mbili za mstatili usawa wa sanamu kwa mbele. Watu wanaamini kuwa kumehifadhiwa za siri, pia kuna siri za kale za bara lililopotea la Atlantis. Nadharia hizi hazina ushahidi wa mashiko na kwasasa mamlaka zimezuia uchunguzi zaidi wa chamber hizo.

3. SREE PADMANA-BHA-SWAMY TEMPLE

View attachment 1153741

Temple hili lipo Keraka huko India. Ujenzi wake ni wa kipekee na umejizoelea umaarufu duniani kote. Ndani yake kuna chamber 6 zenye herufi ABCDEF, huku zikiwa na milango imara na mikubwa ya chuma. Miaka iliyopita mamlaka ziliamua kufanyia utafiti juu ya chamber hizo na kutaka kujua kuna nini nyuma ya milango hiyo. Ilikuwa kazi kubwa sana na mnamo mwaka 2011 walifanikiwa kufungua chamber 5 tu. Walishangazwa na yaliyokuwamo ndani humo kama masanduku yaliyojaa dhahabu, mawe mbali mbali ya thamani na vito vingine vilivyopambwa kwa madini ya almasi ambapo kadirio lake ni takribani $ 1 trillion. Ila vipi kuhusu chamber ya 6 ambayo ina label B? Chamber B bado imebaki gumzo na watu wanaamini kuna nguvu za ajabu zinazolinda mlango huo. Auditor General (Vinod Rau) aliiambia supreme court kuwa chamber B iliahafunguliwa na si chini ya mara 7 na watu hawakupatwa na chochote kama mkosi n.k.

4. THE FIRST EMPERO'S TOMB


View attachment 1153790

View attachment 1153791

Mfalme wa kwanza wa China Qin Shin Huang alizikwa katikati ya China chini kwenye milima ambayo inalindwa na mitego mingi kama mishale ya moto n.k kwa yeyote atakaejaribu kuvamia tomb hilo. Tomb hilo la kihistoria lipo kaunti ya Lintong, jimbo la Shaanxi, ilichukua takribani miaka 38 kukamilika miaka 2000 iliyopita na lilikamilika baada ya miaka 7 ya kifo chake. Mfalme huyo alifariki Septemba 10, 210 BCE. Mnamo mwaka 1974 kuna wakulima walikuwa wanafanya shughuli zao za ukulima ila walipofika karibu na Xi'an wakakutana na sanamu ya ajabu ya mtu. Ikagundulika kuwa ni moja ya sanamu ya askari wa jeshi la mfalme huyo (Terracota Soldiers) ambapo inakadiriwa kuwa chini humo kuliwa na kaburi lao na sanamu zipatazo 8,000 farasi 520 n.k vilichimbiwa chini. Mpaka sasa sanamu za askari 2,000 ndio zimepatikana, ila alipozikwa mfalme ndipo maajabu yalipo.
View attachment 1153795

Wanasayansi mbalimbali na wanahistoria wanadai bado hakujawa na teknolojia ya kufungua lango la kaburi lake. Pia jirani kuna mito miwili (Yellow river na Yangtze) ambayo ina madini sumu ya Mercury ambayo imeizunguka Xi'an. Pia wanaamini madini ya meecury ndiyo yaliyosababisha kifo cha mfalme huyo na alikuwa anatumia anti-mercury pills mara nyingi kujikinga na madini hayo. Wanaamini kwenye kaburi lake kuna vito vingi vya thamani na mambo mengine ya kihistoria. Ardhi ya eneo hilo inadhihirisha kabisa uwepo wa mercury kwenye mito hiyo miwili kwani imeathirika kabisa na kuwa tishio kwa watafiti na wachimbaji wa tomb hilo.

View attachment 1153794
Nimepata elimu hapo asante
 
Okay kwa hiyo ndiyo hii kibongo bongo tunaita "rasimali watu"? Basi nikahisi vidume vilitumika kama matofali.
Na hao tembo ni tembo wanyama, walitumikaje? Aaagh sorry kwa maswali. Tatizo kichwa kizito.
Yeah manpower hiyo.... Tembo walitumika kubeba materials n.k.... Tembo wa kufugwa si tembo wetu wa Serengeti.
 
Vipi kuhusu jiwe jeusi la kule arabuni,naskia wengi wanatamani kuingia waone yaliyomo.
Je haliwezi kuingizwa kwenye list ya 5 hapa.
Lile ambalo lipo kona ya mashariki mwa Kaaba?
 
Back
Top Bottom