Makiwendo
JF-Expert Member
- Aug 12, 2015
- 9,980
- 34,404
Uandishi mzuri....Mpangilio mzuri....Ikikupendeza ongeza Aya Mdakuzi....Msaada wa Mauti
WANAUME hao watatu hawakuwa na hamu ya kumsaidia tena Milembe kwa "dua". Kwani Genja alitoa panga lake, lenye makali yaliyokuwa tayari kwa kazi ya kinyama.
Iliogopesha sana. Bila kusema neno, Milembe aliinyanyua mikono yake juu kwa hali ya kama kujisalimisha, na kutii amri zao zote tangu wakati huo.
Kwani aligundua kuwa amezungukwa na watu katili. Kwa wakati huo, mwanga wa mwezi uliangazia kwa mbali, ukiwa unampa Milembe kivuli cha kifo.
Pigo la Kwanza
Pigo la kwanza lilimfanya Milembe atazame kwa mshangao. Macho yake yalifumba kwa sekunde chache.
Kabla hajapata nafasi ya kutambua kilichotokea, damu nyingi ilianza kuchuruzika kwa kasi toka kwenye jeraha la kichwa.
Milembe alijaribu kupaza sauti ya kuomba msaada, lakini pigo la pili lililopiga shingoni mwake lilikatiza yowe kabla hazijafika mbali.
Pigo hilo lililokuwa na nguvu zaidi, lilimuondoa uhai wake kwa haraka sana.
Mkono wake wa kulia ukakatwa, ukining'inia pembeni kama ishara ya mwisho ya upinzani wake wa kiutu, mwili ukapoteza nguvu.
Milembe hakuweza tena kupumua. Kilichobaki kilikuwa mwili uliojeruhiwa vibaya, ukiteleza chini kwenye sakafu ya nyumba isiyomalizika.
Mara baada ya kumuua, Genja na wenzake walitoweka haraka, wakijua wameacha alama kubwa ya kifo nyuma yao. Hakukuwa na kurudi nyuma.
Walikuwa wamepanga kila kitu kwa ustadi—kutoweka kwa simu za Milembe, kutupa ushahidi kwenye choo cha shimo, na kuficha kila ushahidi wa mauaji hayo.
Lakini, walisahau kama waliacha chupa ya Fanta kando ya mwili wa Milembe. Walifanya kosa kubwa la kiufundi.
Itaendele...
Ova
Hapo kwenye chupa ya Fanta ndiyo hasa napataka...kumeanza kuchangamka..