Milioni 150 Rais Samia kaipata wapi?

Milioni 150 Rais Samia kaipata wapi?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Hizi pesa zote Mil.150 Rais kapatia wapi za kugawa hovyo ?
20231231_191715.jpg


Moja ya kazi ya Rais wa JMT ni kusaidia kusambaza dini?
===
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 150 kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT la Bethel Usharika wa Nshara Machame Mkoani Kilimanjaro anakosali Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Akizungumza leo katika ibada ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo, Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye husali katika Kanisa hilo awapo nyumbani Machame amesema alishirikisha Watu mbalimbali kuhusu kuchangia ambapo miongoni mwao ni Rais Samia.
 
Wenzenu wasomi wanajiongeza. Wana madili, huu uwekezaji wanaouleta Wana share zao pale wanafaidika. Wana migodi, miradi Kwa majina feki na mengi.

Mil 150 ni bajeti Yao ya miezi miwili kama sio mmoja

Amka ndugu
 
Kwani Tanzania kuna dini udini hakuna nishaenda Somalia kule ndio kuna udini tz wewe ukifuga nguruwe Shauri yako ww kama unakuku wako ukijichinjia wew tu kuna taifa ni hatar
 
Hizi pesa zote Mil.150 Rais kapatia wapi za kugawa hovyo ?
View attachment 2858754

Moja ya kazi ya Rais wa JMT ni kusaidia kusambaza dini ?
Mkuu umesahau kuwa rais ana fungu maalum la pesa ambazo haziko audited.
Ukiwa rais unaweza amua pesa uwe unawapa ndugu zako na hakuna wa kukuuliza maana haziko audited.
 
Popote Tanzania siku hizi viongozi husema Rais amewapelekea pesa.
Watu wote (watumishi wa serikali,wanasiasa na raia wengine wanajua kwamba pesa zote za Tanzania ni za Rais (utani tu).
Pesa zake aweza kugawa anavyotaka, hakuna wa kuuliza.
Hata hivyo, zile alizotoa kanisani hazihusiani na serikali, familia imetajwa. Familia ya Rais haiwezekani ikose 150m katika mazingira ya kawaida siku hizi.
 
Back
Top Bottom