Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 1,091
- 3,695
Super power anafundishwa jinsi ya ku hit Target. Hii ni baada ya mashambulizi ya Russia kwenye soft target nchini Ukraine kupungua wakambembe wazee wakazi wameona watoe darasa kidogo.
taarifa ni kwamba.
Vyanzo vingi vya Urusi vimeripoti kuwa Ndege mbili za kimkakati aina ya TU-95 zimearibiwa Leo baada ya shambulizi la drone kwenye kituo cha anga cha Engels-2 huko Saratov nchini urusi.
Cha kushangaza ni kuwa kituo hicho kipo Zaidi ya km 600 kutoka uwanja wa vita wa Ukraine.
Watu kadhaa wameuawa katika milipuko katika viwanja viwili vya ndege vya jeshi la Urusi, kulingana na ripoti ya Russia
Watu watatu wamekufa na kujeruhi sita katika uwanja wa ndege karibu na mji wa Ryazan, kusini-mashariki mwa Moscow, vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vinaripoti.
Watu wengine wawili wameripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko katika uwanja wa ndege katika mkoa wa Saratov.
Haijajulikana ni nini kilisababisha milipuko hiyo.
Maeneo yote mawili ni mamia ya kilomita kutoka mpaka wa Ukraine.
Washambuliaji wa kimkakati wa masafa marefu wa Urusi wanaaminika kuwa katika kituo cha ndege cha Engels katika eneo la Saratov.
Gavana wa mkoa wa Saratov alisema vikosi vya usalama vinakagua kile alichokiita "ripoti za tukio katika mitambo ya kijeshi".
Ripoti hizi - za milipuko miwili katika maeneo mawili tofauti ya kijeshi - zitachochea uvumi kwamba Ukraine inaweza kuwa nyuma yao, mhariri wa BBC Kirusi Steven Rosenberg anasema.
Milipuko hiyo imekuja baada ya picha za satelaiti kutolewa wiki iliyopita zikionekana kuonyesha ongezeko la shughuli za ndege za kijeshi katika kambi ya anga ya Engels.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amefahamishwa kuhusu matukio hayo mawili yaliyoripotiwa, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.
Alipoombwa kuzungumzia milipuko hiyo miwili, Bw Peskov aliambia kikao chake na wanahabari Jumatatu kwamba hakuwa na habari kuhusu matukio hayo na ameona tu ripoti za vyombo vya habari kuzihusu.
Wakati huo huo, Ukraine imesema kuwa Urusi imezindua wimbi jipya la mashambulizi ya makombora nchini humo, huku tahadhari za anga zikitangazwa mjini Kyiv na katika maeneo mengi.
source.
bbc
russia media.