Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Anaandika Milton Mahanga
RC MAKONDA JISAFISHE NA KASHFA HII AU JIUZULU

Hebu Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, kama hii "CV yako" inayotembea mitandaoni ikisemekana imethibitishwa na Mchungaji Gwajima ni ya uongo, tunaomba uikanushe na uweke CV yako ya kweli ili kuweka heshima yako na nafasi yako, na ili sisi wakazi wako wa Dar es Salaam tuwe na imani na wewe bosi wetu. La sivyo kama ni kweli chukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yako ya ukuu wa mkoa.
=========================

CV YA PAUL MAKONDA

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bushite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bushite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg.Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Mayor Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management &Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokua akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carriers 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community &Economic Development (CED).

18. Mwaka 2012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community &Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi A Bushite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bushite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
Milton Mahanga inaonekana ni MTU ambaye uwezo wake wakufikiria sio mzur.Yeye alitajwa na Msemakweli kuwa ana PhD fake na pia anatumia Nina siyo lake.Na yeye anashambulia wengine
 
Hebu ajuaye cv ya aliyekuwa naibu waziri qa kazi atujuze maana naye ni ya kuunga unga nashangaa anajishebedua kumkwaza mako. Hata udaktari wake wa falsafa ulisimikwa na fisiem leo kawasaliti kwa kutopata nafasi ta kugombea ubunge kuoitia fisiem.
Huyu Mahanga kwanza anatumia jina la watu wengine.Na amefoji PhD
 
Akanushe ya nini haingiliani na kazi yake,anadai vyeti siyo vyake akashitaki na amlete mwenye vyeti mahakamani kuthibitisha
 
Kuwa darasa la saba au kuwa na zero sio ishu kabisa.
Kuna viongozi wengi linawahusu.
Kugushi ni habari ingine kabisaaa.
Anaelewa sana ana maslahi binafsi kwenye utetezi wake
 
Hivi shilawadu mbona hawampigii hata sim kumuulizia juu ya kashfa hii aisee
 
HIZI POROJO ZA MAMBO YA MAKONDA NA VYETI HUMU MTANDAONI ZIMETUCHOSHA. YA NINI KUZUNGUKA MBUYU, SI MKAE KIMYA ALIYETUHUMIWA AJISAFISHE, YA NINI KUWEKA MAJIBIZANO. MNATUCHELEWESHA SAFARI YETU YA VIWANDA, WACHA MAJUNGU TUPIGE KAZI, Kama haupo safi kaa pembeni sio kuendeleza majungu na kama upo safi umechafuliwa JISAFISHE ukikataa basi kaa na uchafu wako, kadri busara zako zinavyokuongoza
Wewe endelea na kazi yako. Huku usipite. Hii kashfa ni zaidi ya Richmond maana imetokea kwa mtu anayetuaminisha yuko karibu na Mungu kuliko wote.
 
NASEMA HIVI ISIJE IKATOKEA MKANIONA MIMI MNOKO AU NINA ROHO MBAYA HUMU JF...SITAKI NA NASEMA SITAKI KUSIKIA MAMBO YA AS.GWAJIMA HUMU KWA SABABU YULE NI MTUMISHI WA MUNGU SASA NYIE KAMA HAMNA YA KUJADILI NI BORA MKALALE AU MKANUNUE MAHARAGWE YA MBEYA MLE...ONGEENI YOTE LAKINI HAYA NASEMA NIMEKATAA NA NITAMCHUKULIA MTU YEYOTE SHERIA BILA KUJALI CHEO CHAKE WALA ALIKUWA NANI ..NIMEMALIZA SASA NOLE NIKUTE MTU ALIYETAJA HILO JINA HUMU
Hata makaburu hawakutaka kusikia jina la Desmond Tutu.

The more you refuse to hear my voice, the louder I will sing
 
namuomba Rais amteue Makonda awe MKUU wa Wakuu wote wa mikoa nchini na sisi tulioko nje ya Dar tunufaike na utendaji wake uliotukuka
Ndio utasikia mkuu wa wakuu wa mikoa anamwamkia messenger wa ofisini kwake, kisa kazidiwa elimu
 
Ni ujinga kuamini kwamba Rc Makonda alifeli darasa la 7 mwaka 1996 na mwaka 1997 eti akajiunga form kidato cha kwanza Pamba Sekondary shule ya Serikali. !!!!! Duh....Uongo kweupeeee, Kujiunga kidato cha kwanza sekondary ya Serikali LAZIMA uwe umefaulu na ndiyo maana TSM9 hutakiwa Shuleni unakojiunga. Sasa yeye aliipataje wakati alifeli.?? UONGO MKUBWA.
Kulikua na Shule ya jioni ya kulipia.
darasa la nne alifeli akahamia mjin ili asome tution, duh!? nakumbuka mwaka wetu darasa la nne alifeli mmoja tu (mwaka 1997). kama hii taarifa ni ya kweli, basi acha tu tununue sembe hata 3000 kwa kilo.
 
Daahhh sawa we uliota mapema mno vyumba viwili na sitting sh ngapi mkuu hata choo kiwe cha nje poa tu huku Chamwino hovyo sana
 
Daahhh sawa we uliota mapema mno vyumba viwili na sitting sh ngapi mkuu hata choo kiwe cha nje poa tu huku Chamwino hovyo sana
Mkuu kwa wenzangu 150,000/- kwa mwezi zidisha mara miezi 12. mi ninayo pangisha ipo Oysterbay pana pakana barabara na Area D bei ni 30 kwa mwezi vyumba 2 na sebule ni tsh 90 malipo kwa miezi 6 mazungumzo yapo sharti uwe n Familia(mke au mume hata kama hamna watoto)
 
Mkuu kwa wenzangu 150,000/- kwa mwezi zidisha mara miezi 12. mi ninayo pangisha ipo Oysterbay pana pakana barabara na Area D bei ni 30 kwa mwezi vyumba 2 na sebule ni tsh 90 malipo kwa miezi 6 mazungumzo yapo
sharti uwe n Familia(mke au mume hata kama hamna watoto)

Daah sawa mkuu
 
Hapo juu 14 na 15 sijui zingine ila nakumbuka huyo jamaa hakuwepo chuoni, nikafikili amehairisha mwaka kwa ajili ya mambo ya ya siasa. Mana ni kweli kuna kipindi cha masomo hakuonekana chuo na alioanza nao HAKUMALIZA NAO CHUO.
Daudi Bashite bado ana nguvu kubwa sana kwa mteule
 
Back
Top Bottom