Mimi Bibi Yenu Mpambanaji nimedhulumiwa kwa kutokujua sheria

Mimi Bibi Yenu Mpambanaji nimedhulumiwa kwa kutokujua sheria

Kwa huo umri wako Bibi mwachie laana tu itampata yeye na ukoo wake ,Pole sana.
 
Mimi sio MTU wa kukaa kwa wheelchair, asubuhi natembea kutoka kwangu Mikocheni A, Migombani Street hadi sanamu ya Askari, Samora na kurudi. Nina maisha mazuri kuliko ninavyoweza kueleza. Ujana wangu niliutumia vyama. Nakukaribisha inbox uulize maswali, uone na picha, videos, na wewe uje uone shamba kubwa la SAMAKI, mabanda makubwa ya kuku na maghorofa ya ng'ombe wa maziwa.
Hivi vitu vyote una uhakika na wwe ulivipata kihalali!? Isije kua na wwe ulikanyaga haki za watu enzi ya ujana wako sasa karma ndiyo imekuja ili ulipe dhuluma zote za ujanani wako!?
 
Kuna mtu mmoja yuko kwenye taasisi fulani nyeti ya serikali. NI MTU mzito sana, Akaniambia Bibi, kazini kwangu kuna fursa ya kupiga, ambayo itakunufaisha na wewe.

Nikamwambia ni fursa gani hiyo? Akanipa mpango mzima. Akasema tuanzishe kampuni, yeye na jamaa zake, Ila kwasababu ya conflict of interest hisa zake ziwe kwa jina langu.

Basi, michakato ikaanza, kampuni ikawa registered Brela, na biashara ikaanza, kampuni inapiga dili hela zinaingia.

Makubaliano yetu yalikuwa mwisho wa mwaka anipe 5,000,000/. Mwisho wa mwaka wetu ni mwezi November.

November ikapita, sina kitu, piga simu jamaa hapokei, naenda nyumbani kwake anajificha, ofisini naambiwa yuko meeting.

Mwisho wa siku nikamwambia Kaka, naona hauko tayari kunilipa, basi furahia matunda ya dhuluma yako.

Akaanza kunipiga mikwala kwamba hata kwenye ma shareholders simjui hata mmoja, wala sijawahi kuhudhuria vikao vya bodi ya wakurugenzi na wala sijui vinafanyika wapi.

Basi nikamwambia namwachia Mungu, mi uchawi siuwezi. Yaani unafanya biashara kwa jina langu na hela hutaki kunipa!!!!

Basi kaa nayo.
Akaniambia nenda mahakamani kama unaweza utapata haki yako.
POle sana mtu mzima mwenzangu.....vp tu inbox nikufariji 🙂
 
Mkuu kufanya ubia na mtanzania kwa 99.9% ni kama suicide mission, lazima ulie tu, mimi nimepoteza zaidi ya 150m kwa kuamini watu na kufanya partnership nao usimuamini mtanzania kabisa hasa hao wasomi.
Mwambie hasa hawa hawo waliokariri mm siwezi kuwaita wasomi mana wanachokisimamia hawakielew
 
Hapo wamekwisha kutoa wewe kama shareholder kwa kushimdwa kuhudhuria vikao ama kulipia shares

Angalia brela kama bado upo

Alafu mil 5 ni hela gani kujirisk kiasi hicho?

Lingetolea lolote wewe ndie ungepewa kesi

Hapo ndio basi tena
 
Mkuu kufanya ubia na mtanzania kwa 99.9% ni kama suicide mission, lazima ulie tu, mimi nimepoteza zaidi ya 150m kwa kuamini watu na kufanya partnership nao usimuamini mtanzania kabisa hasa hao wasomi.
Kwanza pole sana kwa dhuruma ulizofanyiwa.
Pili, usipoteze imani kwa generalized instinct kwamba Watanzania wote ni wazurumaji
 
Back
Top Bottom