Kuna wanaotaka kuleta mchafuko wa kisiasa maana siamini kwamba operations kama hizi mama Samia anaweza kuziagiza zitekelezwe.
Ninaweza kuandika kwamba Yeye kama Mwenyekiti wa Chama kinachounda serikali inayosimamia vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi yetu ana taarifa za kutosha juu ya hiki kinachoendelea nchini kwa sasa kwa muktadha ufuatao.
Ni sahihi kwamba kazi ya idara ya usalama wa taifa ni kukusanya taarifa, kuzichanbua na kuishauri serikali juu ya hatua za kuchukua. Kwa maana hiyo ili taarifa zipatikane watu wa idara ya usalama wa taifa wamesambazwa na wanafanya kazi katika idara zote za serikali kuanzia sehemu za kisekta ikiwemo siasa na kuanzia ngazi ya juu kabisa mpaka ngazi ya mtaa tunapoishi.
Kila siku Rais huwa anapokea briefing au muhtasari wa mambo yote yanayoendelea nchini kisiasa,kiuchumi na kijamii pamoja na yale yanayoendelea nje ya nchi au katika mataifa mbali mbali na hatua zinazochukuliwa ndani na nje ya nchi. Na katika briefing hizo idara ya usala wa taifa ni mojawapo ya idara zinazotoa taarifa kwake. Hii ni kutokana na ukweli mabadiliko ya sheria ya idara ya usalama wa Taifa yaliyofanyika yaliifanya idara hiyo iwe chini ya Rais.
Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo idara ya usalama wa Taifa. Kwa msingi huo IGP humpatia hali halisi ya usalama wa ndani na mwenendo wa shughuli mbali mbali ikiwemo shughuli za vyama vya siasa na hatua zinazochukuliwa.
Rais pamoja na nafasi hizo alizonazo kikatiba pia ni mwenyekiti wa Chama Kinachotawala nchi. Katika chama kuna idara mbali mbali zikiwemo za usalama wa chama propaganda na zile za kupanga namna gani ya kushughulika na wapinzani wa kisiasa. Hivyo katibu mkuu wa chama huripoti kwa Mwenyekiti juu ya mambo hayo na hatua zinazochukuliwa kila wakati. Kwa msingi ni vigumu kutofautisha chama na serikali au serikali na chama.
Hivi karibuni viongozi na wajumbe wa kamati kuu ya chama akiwemo Speaker alikua na kauli mbiu ya "pita nao wote wanaokosoa utendaji kazi wa serikali' Huyu ni kiongozi wa juu wa serikali ambaye anasimamia chombo kinachotunga sheria ikiwemo sheria ambayo ambayo imetungwa ya kuwapa kinga wafanyakazi wa idara ya usalama wa taifa kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo mauaji wakati wanatimiza majukumu yao pamoja na kuwa na mamlaka ya ukamataji kama askari polisi. Kwa ufupi imekua ni jeshi kama majeshi mengine. Mwenye kuipeleka sheria hii bungeni ni Rais kupitia waziri mwenye dhamana husika.
Ni hivi majuzi tu Rais alitamka wazi wazi kwamba wanaodhaniwa kuwa wametekwa ni drama na Tanzani ni mahala salama ambapo vitendo vya utekaji na mauaji haviwezi kufanyika. Lakini uwkeli ni kwamba alisikia Yowe na sauti hiyio kwamba watu wanaotekwa wapo na hasa wale ambao wapo kinyume na sera za chama chake pamoja na ugumu wa maisha ambao haushabihiani na utajiri wa nchi anayoiongoza.
Ni hivi karibuni tuu viongozi wawili waandamizi katika chama na serikali yake wametoa matamshi tata ambayo yananasibishwa na mauaji na utekaji na hakuwahi kutoka hadharani kukekemea na wala vyombo vya dola anavovisimamia havikuwahi kuchukua hatua yoyote juu ya watu hao. Hii ni picha halisi kwamba anahisika na anajua yale ambayo yanatokea ila anaamua kukaa kimya kwa sababu ya maslahi ya chama chake. Mathalani kule kanda ya Ziwa kiongozi wa chama alisikika wazi wazi akiwataka jeshi la polisi kutowatafuta watu ambao kwake aliwaita wanaomtusi Rais pindi watakapowapoteza. "kukosolewa kwao hutafsiri kama matusi" ingawa hakuna hata mtu mmoja alishwahi kuburuzwa mahakamani na akathibtika bila mashaka yoyote kuwa amemtusi Rais au mtawala.
Kiongozi mwingine ambaye alifutwa kazi au alibadilishiwa majukumu ni DC wa huko kanda ya Kaskazini aliyeeleza wazi wazi mambo yanayofanyika maaporini ili kuhakikisha ushindi unapatikana.
Hayo ni machache yanayoonesha kwamba Rais anajua kinachoendelea juu ya uhalifu huu dhidi ya binadamu. Hii ni dhahiri kwamba majaji ambao ni wateule wake wametupilia mbali kesi inayotaka ufafanuzi juu ya maswala haya ya utekaji na wakati huo huo Speaker anatupilia mbali mjadala unawowasilishwa na mbunge juu ya vilio vya utekaji.
Wakati hayo yakiendelea na vijana kuendelea kutekwa mitaani Jeshi la polisi linakataa uhusika wake lakini halitoi taarifa ni watu gani wanahusika na matukio hayo na kwanini yawalenge watu fulani pekee na sio ordinary citizens. Maswali hayo yakiwa hayajapata majibu tuanapata taarifa ya Kutekwa mzee kada wa chadema katika mazingira ambayo ni sahihi yanahusishwa na vyombo vya ulinzi na usalama. Uwepo wa askari wa usalama barabarani, gari za polisi kuhusika, marehemu kufungwa pingu, wahusika kuwa na silaha ni maswali ambayo hayana majibu.
Jeshi la polisi halitoi state warning or alert isipokua linatoa taarifa ya kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ma siku chache mtu anakutwa marehemu tayari, katika maeneo ambayo Roma Mkatoliki alitelekezwa na akakimbia nchi mpaka leo. Jeshi hilo hilo la polisi limejitokeza na taarifa nyepesi huku likitumia nguvu kubwa pale Mwananyamala hospitali kutotaka postmortem huru ifanyike kabla ya mwili kuchukuliwa na kwenda kuhifadhiwa.
ikiwa Amiri Jeshi Mkuu hajui na vyombo vyake havijui basi Taifa liko hatarini.