Mimi kada wa CCM lakini mauaji ya kada wa CHADEMA Ali Kibao limetukera

Upo sahihi sana.

Hawa watu wanateka na kuua wakosoaji wa Serikali na watawala. Je, ndani ya CCM hakuna wakosoaji? Kwa hali ilivyo sasa, huenda zamu ya Mpina ipo karibu.

Bila kujali upo chama gani, hawa mashetani wanaweza kukufikia kwa kupanga au kwa kukosea. Kama ikitokea, hata humu ndani ya CCM, akatokea hayawani mmoja akaenda akawajaza maneno kuwa wewe unamkosoa Rais au Serikali yake, ujue watakufikia.

Kwa wenye akili, wajiulize, Zacharia alikuwa CHADEMA?
 
Huyu muuaji sio mtoto mdogo, atakua Ni MTU mwenye 50+ years.
Ina maana hapa duniani Hana zaidi ya miaka 25 ya kuishi. Hivi kweli unamwaga damu ya mtu ili ui njoi kwa miaka 25 tu.?
Nadhani huyu muuaji atakua na familia, nyumba na account nzuri benki, hivi kuua kutamuongezea furaha ya kuishi siku zake chache zilizobaki?

KARMA IS A BITCH.
 
Wambieni wanachama wenzako mkitumaliza ndio hamtakufa?
 
Mkuu wanakwambia Life is Short live it to the fullest.......Hapo wanaongezwa vyeo kwenye category yao. Achana na Pesa mamilioni ya kula bata baada ya kazi nzuri
 
Je marehemu alikuwa na bifu na serikali
 
Muuaji atafahamika tu.
 
Ile sheria iliyopitishwa Bungeni kuhusu Usalama wa Taifa ilikua ni mwiba sana
 
Unakumbuka ile kauli ya mwenzeni '...tukiwapoteza msiwatafute?'
 
Hakika inasikitisha na kuumiza sana, mhimu ni wahusika kukamatwa na kufikishwa mbele ya Sheria na pengine kunyongwa ikibainika na kuthibitika KWa waliofanya mauaji ya raia na mtanzania mwenzetu.siasa za majitaka kamwe zisipewe nafasi katika nchi yetu.
 
Wanauwa na kufira watu halafu hawafanywi chochote
Wanapongezwa
 
Wengi walio CCM ni kwasababu ya njaa ila hawaipendi toka moyoni
 
Hatuna usalama wa Taifa bali kuna usalama wa serikali, polisi pia wako kwa ajili ya usalama wa serikali sio raia - kama ni raia kweli leo pangekua na hekaheka. Hatuna bunge kama chombo kinachoithibiti serikali bali bunge la sasa ni mkono au mwendelezo wa serikali - suala la speaker husika..kipindi cha kinBa Samweli Sitta, Mama Makinda kidogo bunge lilikua balanced - bunge la sasa ni kama kikao cha secretariat ya CCM.
Baba wa Taifa alitusaidia katika kuvunja ukabila na kuleta usawa lkn kwenye suala la Usalama alivuruga sana - system alizoasisi ndo hizi zinazotusumbua mpaka sasa - vyombo vya ulinzi viko katika kulinda sana serikali na viongozi wake kuliko raia...
Njaa, uoga, umaskini nako ni changamoto - huwezi ukasikia kiongozi yoyote mkuu wa serikali kaongelea hili suala mfano : waziri mkuu, makamu wa Rais, IGP, Kamanda wa polisi - wote hawa wabahibernate kabisaaaa..ndo muone jinsi bado tuko nyuma sana...
 

YAANI WAFANYE HAYO RAIS ASIJUE? WEWE UNAFANYA MASIKHARA SANA. RAIS SI ALISHASEMA HIZO NI DRAMA SI MAMBO YA KWELI. AKINA SOKA WANAPIGIWA KELELE WAACHILIWE RAIS HAJUI? YEYE ANAISHI WAPI?
 
Mwambie aache kutoa amri kuwateka watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…