Rayamikhal
Senior Member
- Sep 14, 2026
- 110
- 207
Rafiki yangu jana alinipigia simu, Akiwa na wasiwasi mkubwa. Ikabidi niulize shida ni nini akasema maisha yamekuwa magumu upande wake ikabidi aombe kazi, akatuma Maombi kadhaa kwenye mahotel makubwa ya kitalii akafanikiwa kuitwa hotel X. Shoga yangu aliishia form 4 hana ujuzi wowote wa hotel zaidi ya stationery. Alifanyiwa usaili siku hiyo Ila bahati mbaya ni kuwa walimwambia sehemu iliyopo ni mafunzo kwa miezi 3 chakula kipo pia sehemu ya kulala ipo lakini hatolipwa kitu mpaka miezi 3 itimie. Sasa nikamuuliza mbona unahofu akasema hotel Ile ni kubwa na ya kifahali vipi akifanishwa kazi za ngono wakati anajitolea? WanaJF nimewaletea hili nataka ushauri ili nimpe shoga yangu aone mawazo yetu yatamsaidia kiasi gani.