Mimi kama mwanamke nitajuaje kwamba kazi ya hotel haitaniitaji nivue nguo zangu?

Mimi kama mwanamke nitajuaje kwamba kazi ya hotel haitaniitaji nivue nguo zangu?

Rafiki yangu jana alinipigia simu, Akiwa na wasiwasi mkubwa. Ikabidi niulize shida ni nini akasema maisha yamekuwa magumu upande wake ikabidi aombe kazi, akatuma Maombi kadhaa kwenye mahotel makubwa ya kitalii akafanikiwa kuitwa hotel X. Shoga yangu aliishia form 4 hana ujuzi wowote wa hotel zaidi ya stationery. Alifanyiwa usaili siku hiyo Ila bahati mbaya ni kuwa walimwambia sehemu iliyopo ni mafunzo kwa miezi 3 chakula kipo pia sehemu ya kulala ipo lakini hatolipwa kitu mpaka miezi 3 itimie. Sasa nikamuuliza mbona unahofu akasema hotel Ile ni kubwa na ya kifahali vipi akifanishwa kazi za ngono wakati anajitolea? WanaJF nimewaletea hili nataka ushauri ili nimpe shoga yangu aone mawazo yetu yatamsaidia kiasi gani.

Udivue. Uwe unaoga nazo na kulala nazo tu. Ni maamuzi yako
 
Rafiki yangu amepata kazi hotel nyingine. Watampa marupurupu na atakuwa analipwa nusu ya msharaha kipindi Cha mafunzo kwaiyo anashukuru. Asilimia kubwa ya shauri zenu nilimpa na ameahukuru. Kwaiyo nawashukuru kwa niaba yake. Asanteni wakuu.
 
Back
Top Bottom