Mimi mkataa ndoa naangamia rohoni: Nishaurini ili nipone

Mimi mkataa ndoa naangamia rohoni: Nishaurini ili nipone

Sikai kwetu nipo kazini..
Kwetu ni DSM na kazini ni mkoani.

Sina mpango wa kuoa na wala sina MPANGO WA KUOA.

Sijaona sababu ya kuoa
Sina nia ya kuoa

NA SIHITAJI KUOA.

#YNWA
Mkuu ukitaka kupata mziki wachukue watoto uwalee mwenyewe utanyoosha maelezo mikwara ya vijana ambao mnasema hamtaki kuoa ni kulelewa watoto mko mbali na wazazi wenzenu Kaa nao mwaka uwalee na utengeneze tabia unazotaka wanao wakue nazo sio kumpeleka Kwa bibi au boarding alafu utupe mrejesho hapa
 
Kama huna sababu ya kuacha kazi usiache.
Pili Ili uwe na mafanikio ya kifedha lazima uwe na multiple income sources, unaweza acha kazi, mabadiliko ya kiuchumi yakatokea, biashara zikafa, ukashindwa kujihudumia pamoja na watoto wako.
Usiache kazi, ajiri mfanyakazi, kama unaogopa, weka CCTV camera, then ajiri mtu wa kusimamia biashara yako.
 
Mkuu ukitaka kupata mziki wachukue watoto uwalee mwenyewe utanyoosha maelezo mikwara ya vijana ambao mnasema hamtaki kuoa ni kulelewa watoto mko mbali na wazazi wenzenu Kaa nao mwaka uwalee na utengeneze tabia unazotaka wanao wakue nazo sio kumpeleka Kwa bibi au boarding alafu utupe mrejesho hapa
Huyo wa kwanza nilishawahi kukaa nae mwaka mzima.

Changamoto ni mazingira ya Kazi (kijijini) sanaaa, hayakufaa kukaa na mtoto.

Kwani hata nyie mnaokaa na watoto huwa mnaelea nyie au mama zao?
Au unaposema "malezi" umemaanisha nini?

#YNWA
 
Broh nimejifunza vitu kutoka kwako
Lakin swala la kuacha kazi bado sikuungi mkono two source of income inapendeza sana panga mambo yako vizuri

La mwisho mwaka huu nasaliti slogan ya kukataa NDOA ,mwaka huu naoa alafu ndo nijute zaidi

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Una wenge kinoma, huwezi kusaidiwa kwa wenge lako. Punguza wenge calm down. Angalia mambo katika angle zote. Biashara ina faida na hasara na kazi ina faida na hasara. Watu wana biashara kumi huko na bado wametulia wewe duka sijui frame ya nn unaona mpaka kazi ni mzigo ?? Acha kiburi cha vijipesa hivyo. Unataka kuhama tengeneza mazingira mazuri watu wa sign uhamisho. Wewe unaonekana umejaa jazba kiburi na majivuno, jishushe wahi kazini alafu tengeneza mipango fasta tu unahama. Mambo ya ndoa sijui watoto sio muhimu kama uko mbali nao.
Very true
 
Hapo kwenye kuchukua watoto ulee utaweza peke yako huku unakimbizana na biashara ama kazi? Lazima uwe na mweza kama msimamizi wa nyumba, mwangalizi wangekua wakubwa sawa lakini kwa sasa wadogo mno pamoja na kua wako boarding but wanahitaji uangalizi

Pengine waweza kusema mbona kuna watu wanalea watoto mama ama baba wako katka wajibu wakazi zao jua jambo dogo kua mama hua akirejea nyumbani ni rahisi kuona badiliko lolote la mtoto kama hutaki kuoa bora waache kwa mama zao ibaki kuja mara moja moja kwako.
 
Uko sahihi
 
Nakushauri usiache kazi, maana ukiiacha utakuja kujuta baadae
 
Hahaaa umenikumbusha mtu mwenye mchepuko na mke mara nyingi akiacha mke na mchepuko wanaachana, bora kuacha mchepuko ila ukigusa mke tu na mchepu kwa heri.

Hapo labda aache biashara ila akiacha kazi na biashara ndio kwa heri, hataamini
Acha uoga, mshahara haujawahi mtajirisha binadamu yeyote hapa chini ya jua. Faida itokanayo na biashara utajirisha
 
Mkuu,wasikutishe mkuu,hata mm niko ktk mpango kazi wakuhakikisha naacha kazi kwenye local government hizi,muajiriwa tamisemi,mbona wapo wengi tu wameacha kazi serikalini nawanaendelea na biashara zao binafsi au kazi zao binafsi???,,,ningumu kuwatumika mabwana wawili ukatoboa,kazi nabiashara kwa wkaati mmoja ukafanya vyote kwa ufanisi mkubwa ningumu,angalia kama biashara imechukua asilimia kubwa ya attention yako ,wekeza huko mda wako akili yako na ubunifu wako nae Mugu wa mbinguni atakubariki,fikiria mbona kuna wastaafu wengi ambao hawakuacha kazi still wamepigika tu kimaisha licha ya kuaminishwa wakati wa ujana wao kua kazi za serikali ndio kila kitu, still napension wamepokea lkn bado wnaaishi maisha dhalili sana tena maafisa wakubwa tu!!!????,,,kingine nikua nimara chache sana kupata msimamizi wa jambo lako ambalo unalihusudu (biashara yako) akafanya vilevile kama ambavyo ww mbeba maono ungefanya,mara nying huboronga nahua hawajali ,ndipo anguko lawatumishi wengi wauma kuharibikiwa biashara zao huku wao wakiwa makazini,wasimamizi wao hua hawana machungu au maono walionao wenye biashara husika.acha kazi kama utapata amani ya moyo,nenda kaifanye kwa moyo wako wote nakwanguvu zako zote,nae Mungu wambinguni ataibariki kazi ya mikono yako mkuu.barikiwa sana ur not alone in this world of dillema.kazi hizi za serikali hasa ktk jamii za watanzania zimekua kama ni IS unit ktk maisha ya watanzania walio wengi lkn still hazitoi majibu ktk maisha ya watumishi .watumishi wengi waumma hadi anafikia umri wa kustaafu unakuta analalamika tu,mara hajalipwa hiki mara hajafanyiwa hiki,asilimia ndogi sana ya watumishi wa umma sio walalamishi ktk shuguli zao.
 
Back
Top Bottom