Mimi mkataa ndoa naangamia rohoni: Nishaurini ili nipone

Mimi mkataa ndoa naangamia rohoni: Nishaurini ili nipone

Mkuu kuna maswali ukitaka upate majibu yake kutoka kwa jamii ambayo asilimia kubwa ni either watumwa wa ajira au wa wanatamani kua kwenye huo utumwa huwezi ukapata majibu ya kile moyo wako unataka. As long as kiu yako kuu ni freedom basi ajira kwako sio option lakini zingatio ujapo kwenye biashara miguu yote ukubali kujitumikisha kweli kweli na kukubali kukosa huo uhuru kwa muda kutokana na stresses za biashara. Miezi 7 ni michache sana kujihakikishia utam wa biashara hasa ukizingatia biashara muzianzishazo wafanyakazi zinatokana na hela ambayo siyo ya jasho kiivo tofauti na mjasiliamali alieanza from the scratch, in short kuna process (price for success) nyingi ambazo unakua umeziruka and you must pay them ahead and they are there to shape and strengthen you to became strong mentally and emotionally kwa sababu personalities za mfanyabiashara na mwajiriwa ziko tofauti kabisa. Kama uko tayari kukabiliana na changamoto za biashara karibu (and its possible kwa aliye na nia na pia ni kutam sana ukikuweza na hasa ukijifunza kuenjoy ups and downs zake) ila kama utakua umehadaika na mafanikio ya miezi 7 tu ya biashara au na mkopo uliochukua nakushauri baki tu kazini kwa sababu stages za mwanzo wa biashara kupoteza hivo vyote vinavyokuhadaisha ni jambo la kawaida sana you have to be fit enough kuweza kucome back again. Mazingira yako yalikuaga km yangu utofauti ni kwamba sikuomba ushauri kwa yoyote kwa sababu wote walikua against wazo la kuacha kazi but I decided it na sasa ni mwaka wa6 sijawahi kujuta though miaka mi3 ya mwanzo it was the toughest moments ever in my life kutoka kua mwenye kazi yenye mshahara+viposho vya hapa na pale hadi kufikia hatua ya kusaka vibarua kwa siku ili ufund biashara, na mbaya zaidi ukiacha kazi upatapo changamoto no one cares about you wakidai ulijitakia. Fuata moyo wako hasa ktk maamuzi yanayoinvolve maisha. Take a calculated risk, mfano jenga hata vijumba/vifrem vya kupata walau chochote ili familia isije ikaadhirika unapoikua kwenye hardship moments kwa sababu hazikwepeki

Amen.
Nimekuelewa sanaa

Me too soma hii

#YNWA
 
Bado sio margin nzuri kwa maoni yangu. Faida ya 40k per day kwa maisha ya sasa bado ni ya kawaida sana, walau iwe mara mbili yake ndio naweza kusema youre good to go, risks za biashara pia ni kubwa. Endelea kukuza biashara yako huku ukiendelea kufanya kazi, tafuta uhamisho, punguza ego kwa bosi wako ili upate unachokitaka.

Mwisho, haya mashauri ungekuwa na mama watoto mngeyamaliza wawili tu tena kwa muafaka mkubwa huku ukipewa happy ending, endelea kukataa ndoa tu!!
.... Amen.

Na nitaikataa mpaka kifo.

#YNWA
 
Najihoji sana kuhusu elimu yako.

Yaani una kitu kinaitwa MAKUSUDI halafu unataka tukushauri.

Andika barua kuacha kazi uendelee na biashara zako kwa sababu uzembe wako unaoufanya makusudi unatutia hasara kodi zetu na unaziba nafasi za watu wanaoweza kuwa na tija kwenye nafasi yako.

Mkuu. omba kuacha kazi
Kuacha kazi HAKUMBWI.

Unatakiwa kuondoka ili wakufukuze ili iwe advantage kwako.

#YNWA
 
Pole sana .
Bwana mdogo , nakupa pole kwa maana nahisi bado wewe ni mdogo na ujana unakudanganya ila nahisi tutaelewana vyema .Naomba nijibu haya .

Vipi kwenda kusomea doctorate ulighairi ?
Vipi biashara imepanda tena faida maana kuna kipindi ulisema imeporomika ?

Ndugu kuacha kazi sio kufeli maisha wapo wengi walioacha kazi na maisha yakaenda kawaida hivyo sikukatazi kuacha kazi .

Ila sasa nakuona na matumizi mengi kiasi kuwa biashara italemewa .
Mkurugenzi kagoma kusaini barua zako ndugu hujui jinsi ya kuitafuta haki yako na masters degree kwel?

Be seriuos man naomba simama kidete tafuta haki yako maana kuhama sio uamuzi wa mkurugenzi ni haki yako .

Hivyo tafuta haki yako juu ya huyo mkurugenzi , ila pia ukifeli basi hamisha biashara yako hapo mkoani ulipo .

Pole sana ila usiache kazi kwanza jiweke sawa kiuchumi usikurupuke kuacha kazi sio rahisi ila ni rahisi .

Pole sana .
 
Najihoji sana kuhusu elimu yako.

Yaani una kitu kinaitwa MAKUSUDI halafu unataka tukushauri.

Andika barua kuacha kazi uendelee na biashara zako kwa sababu uzembe wako unaoufanya makusudi unatutia hasara kodi zetu na unaziba nafasi za watu wanaoweza kuwa na tija kwenye nafasi yako.

Mkuu. omba kuacha kazi

Mbona una hasira sanaa...
Kodi zako wewe na nani?, Kwani Mimi SIKATWI KODI?

#YNWA
 
Pole sana .
Bwana mdogo , nakupa pole kwa maana nahisi bado wewe ni mdogo na ujana unakudanganya ila nahisi tutaelewana vyema .Naomba nijibu haya .

Vipi kwenda kusomea doctorate ulighairi ?
Vipi biashara imepanda tena faida maana kuna kipindi ulisema imeporomika ?

Ndugu kuacha kazi sio kufeli maisha wapo wengi walioacha kazi na maisha yakaenda kawaida hivyo sikukatazi kuacha kazi .

Ila sasa nakuona na matumizi mengi kiasi kuwa biashara italemewa .
Mkurugenzi kagoma kusaini barua zako ndugu hujui jinsi ya kuitafuta haki yako na masters degree kwel?

Be seriuos man naomba simama kidete tafuta haki yako maana kuhama sio uamuzi wa mkurugenzi ni haki yako .

Hivyo tafuta haki yako juu ya huyo mkurugenzi , ila pia ukifeli basi hamisha biashara yako hapo mkoani ulipo .

Pole sana ila usiache kazi kwanza jiweke sawa kiuchumi usikurupuke kuacha kazi sio rahisi ila ni rahisi .

Pole sana .

PhD NILIGOMA kwasababu, nilishindwa kuacha mambo yangu ya pesa halafu kwenda nje miaka 3, Akili iligoma.

Biashara, Kuna mtu alinishauri jambo, nikalifanya na biashara IMEKUWA changamfu Tena (binadamu wabaya sanaa).

#YNWA
 
PhD NILIGOMA kwasababu, nilishindwa kuacha mambo yangu ya pesa halafu kwenda nje miaka 3, Akili iligoma.

Biashara, Kuna mtu alinishauri jambo, nikalifanya na biashara IMEKUWA changamfu Tena (binadamu wabaya sanaa).

#YNWA
Pole sana .
Usiache kazi pambana uwezavyo ila kazi pambana nayo jiweke sawa kiuchumi theb maamuzi ni yako .

Kila la kheri.
 
Mkuu life is too short to waste time doin what you hate.
Hata hivyo jipange sana kabla ya kuacha hiyo kazi.
Kwa sasa pambania uhamisho uwe karibu na hiyo biashara unayoipenda.

Huwa siwaelewi team KATAA NDOA ila usiwasikilize wanaokushauri eti uoe ili mke asimamie duka.Atakayeolewa na wewe team KATAA NDOA atateseka sana.
 
GREETINGS.
Haloo wananchi wote wa JF, hamjambo?

Baada ya salamu twende kwenye mada.

INTRODUCTION:
Mimi ni mtumishi wa umma niliye ajiriwa 2012 na fani x (diploma) kwa level za kata (Afisa wa katani @ SIO MTENDAJI KATA).

2013 nikaenda chuo na kurudi 2018 na masters (niliunga) ya fani y.

Nikiwa na furaha na niite bahati, kurudi tu kazini nikapewa ofisi ya fani y, yaani nilimaliza chuo na kurudi kazini November 2018 na January 2019 nikahamishiwa halmashauri.

Niite bahati kwasababu, imekua ngumu kwa watumishi wengi kutoka Shule tu na ofisi zao za Utumishi wakawabadilishia Kazi zao (rectegorization au kuwahamishia kwenye vitengo walivyosomea).

Nilifanya Kazi kwa furaha na juhudi sana na 2019 nikapokea barua ya kubadilishiwa muundo (recategorization).

Niliona zile ndoto zangu za kuwa mkubwa kama zinaanza kutimia hivi na nilifanya Kazi kwa juhudi sana.

Fani y ndio niliyokuwa naipenda.

Fani x nilisomea tu kwa vile nilikuwa yatima na nilikosaga ada ya kusomea fani y miaka hiyo.

Ila hiyo fani x ndio iliniingiza serikalini.

SCENARIO:
2020 likatokea jambo kazini, mara TAKUKURU hao, mara CAG huyo, mara kamati ya kutuchunguza hiyo, mara usalama wa taifa huo.

Kifupi vitu vilikuwa vingi, ila iliamriwa tusimamishwe Kazi.

Tukiwa tumesimamishwa Kazi niliamua kufungua biashara.

Baada tu ya kusimamishwa Kazi nilitumia wiki 2 kutafuta frame na kuanza biashara.

Baada ya miezi 7 nikarudishwa kazini na mambo yakaendelea.

Ila biashara yangu ilikuwa ya moto sanaa (inauza sanaa).

PROBLEM
Baada ya kurudi kazini Kuna mambo nikaona yamebadilika.

1. Upendo na ile Kazi ukapoteaaa kabisaa

2. Nilikuwa mtoro balaa mpaka Mkurugenzi aliandika barua kwenda Utumishi ya Mimi kuvuliwa madaraka na kupewa mwengine.

Yaani aliyekuwa kijana wangu wa chini sasa hivi ni boss wangu.

3. Kuona hii ajira siipendi Tena, nikaona nitafute uhamisho, changamoto sasa, Mkurugenzi kagoma kabisaa kusaini barua zangu za kuniruhusu nikatafute post kwengine.

Anasemaga "bado nakuhitaji sanaa na siwezi kukuruhusu uondoke"

4. Nakiri; kunivua madaraka hata sijamlaumu, kiukweli kabisa nimekuwa mtoro balaa, siipendi Kazi Tena (kwasasa napenda sanaa biashara yangu na wanangu).

5. Yaani kazini naweza pitisha wiki sijasaini daftari la mahudhurio maana naingia saa 3 au 4 asubuhi na "ole wako uniulize lolote juu ya hilo..!!""

6. Yaani kwasasa siipendi Tena hii halmashauri, siipendi Tena hii Kazi (niliyokuwa naiwaza kuifanya miaka hiyo), kifupi HII OFISI NA KAZI YA SERIKALI SIVIPENDI KABISAAA.

BIG PROBLEM
Kuona nawaze kujiharibia future kazini nikaona nishirikishe wakubwa.

Hao wakubwa nao wamenipa ushauri ambao HATA SIJAUKUBALI.

Ninachonipa "Huu ukichaa wa kutopenda Kazi" ni kwamba NAHITAJI KUWA HURU.

Nahitaji kuwa kwenye biashara zangu masaa 24,
Nataka chochote kinachotokea kwenye biashara nikione, KIFUPI BIASHARA IMENIMEZAA HASAA yaani ROHONI na NAFSINI NAWAZA BIASHARA ZANGU.

Naweza kuwa ofisini kuanzia asubuhi mpaka jioni ila nikaishia ku-google na kusoma mambo ya biashara hiyo, nikaishia kupiga simu dukani na Kwa wateja badala nifanye Kazi za watu..!!!

Ushauri..
1. Shangazi yangu aliniambia "NIOE" halafu mke ndio asimamie halafu Mimi niendelee kupambana na ajira.
HUU USHAURI NILIGOMA KABISAAA

2. Boss mmoja, aliniambia nitafute uhamisho ili niwe karibu na biashara yangu.
Nikaona hili wazo ni sahihi, kwa maana biashara yangu ipo mkoa wa jirani na niliko.
Ila sasa tokea 2021 nianze harakati za kuhama basi Mkurugenzi kagoma kabisaaa kunisainia barua ya uhamisho ili nikatafute post kwengine (mkoa ilipo biashara yangu), hili swala LIMEFANYA NIMCHUKIE KABISA.

Nikawaza kuacha Kazi.

Nina watoto wawili mmoja darasa la 3 mwengine la 2.
Hawa watoto nawaelewa sanaa, nawasomesha Shule ada Mil 2.7 *2 (Mil 5.4, WANASOMA SHULE MOJA).

Wapo Dar kwa mama zao (kila mmoja na mama ake), ila tunawasiliana kila siku.

Nahitaji kuhama niende kwenye biashara zangu halafu niwavute wanangu ili niishi nao.
NAWAPENDA SANAA WANANGU.

Nawaza kuacha Kazi ili nikakomae na biashara yangu.

CONCLUSION.
Sina wazo la kuoa na wala sitaki kuoa, hivyo sihitaji kuwa na mtu wa kusimamia biashara sijui kunisaidia kulea.

Nikiangalia Kazini napata hela na biashara napata pesa.

Kwahiyo nipo dilema, nikisema niache Kazi Kuna pesa itapwaya tu kwenye maisha yangu, sasa naona kama duka litahelemewa na majukumu.

NIA YA KUACHA KAZI NINAYO, ILA SABABU SINA.

Ukicheki nilisoma sanaa kwasababu ya hii Kazi ila SIIPENDI TENA.

Mpaka muda mwengine nawaza KWANINI SASA NALISOMA SANAAA HIVI?

Ushauri wenu na MSAADA WENU MUHIMU SANAA.

Asanteni.

#YNWA
hapo angalia tu jinsi ya kuacha kazi yako taratibu maana kama unavyosema yalishatokea maseke na wazee wa takukuru walikuja ina maana mpaka now bado mpo kwenye rada za wazee wa kazi wanawaangalia.

na kama unavyosema kuwa biashara inatembea vizuri siku ukiacha ghafla jamaa wakikufatilia na kugundua una mamilioni kadhaa alafu mshahara wako mdogo jiandae kufilisiwa
 
Kwahiyo nikutafutie wewe Kazi ila sio kunitafutia Mimi Kazi?

#YNWA
Expand kipato chako ili ukiacha uwe umeacha na visima vya vipato vyengine sio kimoja tu.So hata hapo unaweza fungua huoni kuna maduka ya discount centre kwenye majiji makubwa.
 
Ninyi wakataa ndoa,wengi wenu mnakuwa mna tabia Mbaya!(Ushoga) ! Kwanini unakinzana na kusudi la Mungu ilihali hauwezi kujizuia?? Ukiamua kuikataa Ndoa ni Vyema Ukaacha Ngono pia!
Kama Hauna Mpango wa kuoa,tafadhali usiwachukue Hao watoto kwa Mama zao! Kesi za kulawitiwa watoto na Baba zao zimekuwa nyingi sanaa! Ni Vyema uendelee kuwatunza wakiwa hukohuko
Mmekosa hoja sasa, wewe ameshakwambia amewalawiti watoto wake au unafikiri wanawake hawafanyi mabaya kwa watoto wao. Ninaendelea kusema wanawake mkikosa hoja mpotayari kutusi au kumkejeli mtu ili tu ujionee mshindi hasa kwakulitumia hilo neno ulilolitaja huku mkiwa mnapiga vita hayo mambo yasiendelee sasa sijui kwanini midomo yenu hilo neno limewajaa. Uoe nani wakati kizazi kimezaa uzinzi na uasherati balaa.
 
Kama umevuka 35 kaa kwa kutulia kwenye 9-5, biashara konyo dakika sifuri unajikuta on the trenches, bado familia huku energy ishakata
 
Usije ukathubutu kuacha kazi ndugu yangu, tafuta mtu mwenye kujielewa muweke kwenye biashara akusaidie ikiwa wewe unaendelea na kazi labda wakufukuze, lakin kama Bado wanakuitaji piga kazi.
 
Mmekosa hoja sasa, wewe ameshakwambia amewalawiti watoto wake au unafikiri wanawake hawafanyi mabaya kwa watoto wao. Ninaendelea kusema wanawake mkikosa hoja mpotayari kutusi au kumkejeli mtu ili tu ujionee mshindi hasa kwakulitumia hilo neno ulilolitaja huku mkiwa mnapiga vita hayo mambo yasiendelee sasa sijui kwanini midomo yenu hilo neno limewajaa. Uoe nani wakati kizazi kimezaa uzinzi na uasherati balaa.
Yeye haufanyi?? Mkiamua kutokuona,acheni pia Uasherati na Uzinzi!!!
 
Jibu unalo fanya maaumiz ambayo unaona kwako ni sahihi
 
Yeye haufanyi?? Mkiamua kutokuona,acheni pia Uasherati
Sasa tatizo lako nini maana nothing changes kama hamna tofauti ya ndani ya ndoa na nje ya ndoa. Kote ni yaleyale, so achana na maneno pamoja na matusi yasiyo na tija. Believe me, angeandika kuwa ni kapuku hamna mtu angesuggest aoe na wanawake ndio mngekejeli balaa. Hivyo acheni kuwa motivational speakers.
 
Back
Top Bottom