Mimi mkataa ndoa naangamia rohoni: Nishaurini ili nipone

Biashara inaweza kukupa moyo miaka mitano ya mwanzo lakini baada ya hapo ikakupiga mbaya.

Nakuunga mkono kuhusu suala lako la kuacha kazi lakini sio leo, sidhan kama biashara yako imesimama kiasi kwamba ikitokea umeumwa miezi 6 biashara haiyumbi. Biashara moja sio ya kuacha kazi. Sidhan kama majukumu yako mazito kiasi cha kushindwa kufanya kazi. Kuna watu wana majukumu mazito kushinda wewe, mabalozi nje ya nchi, makatibu wakuu, wakurugenzi, wana biashara zao na kazi hawajaacha na hawana mpango wa kuacha, wewe na fremu moja tena ya kupanga unawaza kuacha kazi, kazi yako inaweza kukusaidia upenye kwa urahisi katika misukosuko ya kibiashara, najua bado hujakutana na mikikimikiki ya kibiashara.

Kuna jamaa alichukua mkopo benk akaomba na likizo ya mwezi, kaingia mtaani kusanya mazao ingia nayo kongo hapo, mzigo wa 10m karudi na zaidi ya m100, jamaa kapagawa kaona biashara ndio hii, alivyorudi kuenda kwa mwajiri wake na barua ya kuacha kazi mkononi, kaenda kukopa hela nyingine tena kwa watu ili aondoke na mzigo mkubwa zaidi na hela aliyopata huko mwanzo kaitia yote kwenye mzigo,

Wateja walionunua mzigo mwanzo walimwambia aje na mzigo kadiri ya uwezo wake kwani makuta/faranga/dorari zipo za kutosha, kumbe bwana wale walikuwa ni madalali wa waasi, na mwanzoni walimpa hela nyingi ili kumtia jamaa tamaa, ili alete mzigo mkubwa wayeyuke nao kimasta.

Jamaa kaingia kichwakichwa na mzigo kongo, fika eneo la tukio wazee wa kazi wanapakua mzigo wake chini ya ulinzi mkali kama raisi wa marekani alivotembelea yukreni, kisha walee wakasepa bila kuacha hata thumni. Kazi ikawa juu ya kazi, wenye malori hajawalipa, mzigo umetekwa, makoli hayana mafuta, hela za watu kakopa, benki ana deni, kazi ameshaicha, alichakaa ndani ya masaa machache.

Kufipisha stori alifanikiwa kurudi, lakini brek ya kwanza ikawa kwa GEORGE HURUMA MKUCHIKA, kipindi hicho ni waziri wa utumishi.
 
Usiache kazi mkuu unaweza kuomba likizo bila malipo ata miaka mitatu ukaenda kwenye biashara zako kwa huo mda then ukiwa huko naamini akili itakukaa vizuri tu
 
Kifupi huijui career path yako btn formal job and self employement (business) bado unajitafuta. Na hii ni sababu tosha ya wewe kutokuwa na maamuzi ya kuoa. Bado hujui unawezaje kuwa mume na baba wa familia. Hujui ipi ni kazi sahihi itakayokuongoza kuendesha maisha yako, unaichukia kazi kisa boss kakuudhi? Ukiudhiwa tena kwenye biashara unafanyaje? Vyote vinaenda sambamba.
Ushauri
1. Onana mwana saikolojia akusaidie ku reset your mind.
Humu wamo lakini hutakuwa na stage sessions. Maana ushauri unahatua.

2. Tafuta business consultant ongea nao kuhusu biashara yako wakupe mwanga ufanye maamuzi.
3. Achana na ujinga wa kufuata mkumbo wa mitandao ya kijamii kuhusu champain chafu za kuzuia muungano wa familia (Ndoa).
Hii champain ya kataa ndoa inaenda sambamba na rainbow rights ni sehemu ya kuharibu akili za vijana wetu ili nchi za daraja la 3 tusinyanyuke kamwe. Break the chain anza kufanyia kazi utu wako.
 
Mrejesho vipi sasa 🤔
 
unataka tukushauri nini?
 
Pole kwa changamoto. Kwa mazingira hayo lazima kazi uichukie sababu ulisimamamishwa kwa tuhuma lkn umerudi ktk mazingira yaleyale . Kisaikolojia tu lazima ari ya kufanya kazi ipungue au ishuke kabisa.

Pili kama ulikopa mkopo mrefu na biashara bado haijaanzaa kuzaa matunda na huku mshahara unamakato pia lkn kazi uione changamoto.

Biashara ni rahisi kufanikiwa kama tu utaweka nidhamu katika pesa. Na kama huna tegemezi wanaokutegemea. Changamoto kwa familia zetu za kiafrika tuna ndugu jamaaa wadogo zetu. Sasa kama.

Kama inawezekana jaribu kuomba uhamisho japo wa ndani ya mkoa uende halmashauri nyingine. Usiache kazi kwanza ilihali hujapata uzoefu ktk biashara. Ukishapata uzoefu wa kujua changamoto,,,na mambo mengine. Ndipo ufanye maamuzi ya kuacha.

Siku zote simamia kile unachokiamini kwa maana hata ukikosea huwezi mlaumu mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wafanyakazi wa serikali ni waogaa Jamani [emoji119]

Imagine anaogopa mpaka ndoa

Nani kakwambia kuwa naogopa kuoa?
Lini nimekwambia kuwa naogopa kuoa?

Kifupi:-
Sioni Sababu ya kuoa
Sina Nia ya kuoa
SIHITAJI KUOA.

Sio wote tuwe wanamuziki, wengine tubaki mashabiki.

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…