Mimi mtu akinifanyia ubaya lazima apate matatizo makubwa ikiwemo kifo na magonjwa je hii imekaaje ?

Wakuu Mimi sio mtu wa dini Sana wala ndumba.

Mimi huwa naabudu mizimu na Mungu.

Ila kitu ambacho huwa sikielewi Mimi mtu akinitapeli , kuniibia basi lazima apate matatizo ikiwemo kifo.

Hivyo watu wamekuwa wakiniogopa Sana.
Kifo ni kitu cha kawaida kwa binadamu wala hata wewe utakufa, sasa wewe ukifa unakua umemfanyia nani mabaya kama kifo ni adhabu ya kufanyia mtu mabaya?
 
Wewe ni kama mimi. Huwa najiuliza ni kwa nini. Yaani nikisha mchukuia mtu na Kawa nawaza namna ya kulipiza kwake na kujiona simuwezi huwa nashangaa anapata jambo baya ambalo sijulitegemea. Nimeshawafelisha wengi japo na mimi sinyanyuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…