Zehoes
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 512
- 352
Mimi, mwalimu katika Shule ya Sekondari Likongowele, Wilaya ya Liwale, kwa heshima kubwa napenda kuwasilisha malalamiko haya kwa mamlaka husika kuhusu hali ya usalama wangu pamoja na familia yangu.
Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukikabiliwa na tishio kubwa la usalama (hata kuuwawa) kutokana na tuhuma za uongo zinazodai kwamba mimi na mke wangu tunaendeleza vitendo vya ushoga. Tuhuma hizi si za kweli kwa asilimia mia moja (100%) na zimekuwa zikitumika kutuchafua hadharani na kuharibu heshima yetu mbele ya jamii, ilhali sisi tumejitunza kwa misingi ya imani yetu na kwa kusudi la utumishi wa Mungu.
Nina sababu za kuamini kuwa baadhi ya viongozi ndani ya Halmashauri ya Liwale, kwa kushirikiana na watumishi fulani wa Idara ya Utumishi wa Umma, wamekuwa wakieneza upotoshaji huu kwa makusudi ili kuhalalisha tuhuma hizo. Taarifa za uchunguzi pia zimekuwa zikigeuzwa na kupotoshwa ili kuendeleza jambo hili.
Zaidi ya hayo, tarehe 30/08/2025, kulikuwa na mpango wa kuniua, mpango ambao kwa uwezo wa Mungu haukufanikiwa. Hata hivyo, bado kuna dalili za njama zinazoendelea dhidi yangu. Baadhi ya walimu wenzangu wa Shule ya Sekondari Likongowele ninaowafahamu, wanahusishwa moja kwa moja na mipango hii ya kutaka kuniangamiza.
Kutokana na hali hii, naomba:
1. Mamlaka husika zichukue hatua za haraka za kulinda usalama wangu na familia yangu.
2. Uchunguzi wa kina ufanyike ili ukweli ujulikane na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
3. Nipo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote ili kusaidia katika uchunguzi huu.
Naomba malalamiko haya yashughulikiwe kwa uharaka na kwa haki.
Nawasilisha kwa heshima kubwa.
Imetolewa na:
Mwalimu – Shule ya Sekondari Likongowele
Wilaya ya Liwale