DOKEZO Mimi na Mke wangu tunatishiwa kuuawa kwa tuhuma za uongo

DOKEZO Mimi na Mke wangu tunatishiwa kuuawa kwa tuhuma za uongo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Zehoes

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
512
Reaction score
352
Mimi, mwalimu katika Shule ya Sekondari Likongowele, Wilaya ya Liwale, kwa heshima kubwa napenda kuwasilisha malalamiko haya kwa mamlaka husika kuhusu hali ya usalama wangu pamoja na familia yangu.

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukikabiliwa na tishio kubwa la usalama (hata kuuwawa) kutokana na tuhuma za uongo zinazodai kwamba mimi na mke wangu tunaendeleza vitendo vya ushoga. Tuhuma hizi si za kweli kwa asilimia mia moja (100%) na zimekuwa zikitumika kutuchafua hadharani na kuharibu heshima yetu mbele ya jamii, ilhali sisi tumejitunza kwa misingi ya imani yetu na kwa kusudi la utumishi wa Mungu.

Nina sababu za kuamini kuwa baadhi ya viongozi ndani ya Halmashauri ya Liwale, kwa kushirikiana na watumishi fulani wa Idara ya Utumishi wa Umma, wamekuwa wakieneza upotoshaji huu kwa makusudi ili kuhalalisha tuhuma hizo. Taarifa za uchunguzi pia zimekuwa zikigeuzwa na kupotoshwa ili kuendeleza jambo hili.

Zaidi ya hayo, tarehe 30/08/2025, kulikuwa na mpango wa kuniua, mpango ambao kwa uwezo wa Mungu haukufanikiwa. Hata hivyo, bado kuna dalili za njama zinazoendelea dhidi yangu. Baadhi ya walimu wenzangu wa Shule ya Sekondari Likongowele ninaowafahamu, wanahusishwa moja kwa moja na mipango hii ya kutaka kuniangamiza.

Kutokana na hali hii, naomba:

1. Mamlaka husika zichukue hatua za haraka za kulinda usalama wangu na familia yangu.

2. Uchunguzi wa kina ufanyike ili ukweli ujulikane na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

3. Nipo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote ili kusaidia katika uchunguzi huu.

Naomba malalamiko haya yashughulikiwe kwa uharaka na kwa haki.

Nawasilisha kwa heshima kubwa.

Imetolewa na:
Mwalimu – Shule ya Sekondari Likongowele
Wilaya ya Liwale
 
Huko Liwale ndio home. Mimi ni mdogo wake Sheikh mkuu wa Liwale.
Liwale kuna watu wakatili sana ukizingua. Watanganyika wanapenda sana uzushi.
Mungu akuokoe .
Karipoti polisi, kuna dogo nimesoma naye hapo uliza afande Denis. Anaweza kukusaidia.
Ila kwa vichwa vya Liwale huyo sheikh ndo atakusaidia kwa haraka kuliko vyombo vya usalama. Maana huko sheikh ana nguvu sana
Naomba tuwasiliane mkuu PM
 
1. Kuna mtu mkubwa anataka kumtafuna au ameshamtafuna na sasa anataka kumiliki sababu ameona ni mtamu.
2. Inaonekana unapiga kazi na unakubalika kiasi cha kuwafunika wenzako.
3. Kuna mjuba mmoja aidha umekula mkewe au unakula demu ambaye yeye aliomba akakataliwa.
4. Unafanya shughuli nyingine za kukuingizia kipato mashambani ama kwenye biashara nyinginezo na inaonekana unapiga bingo na hauhangaiki na wakuda kwenye vijiwe vyao na hata ushauri wa kijinga wanaokupa.
Nakushauri omba uhamisho baada ya kufanya michongo vingine utauliwa mchana kweupe na shemeji tutammiliki na alivyo na macho mazuri atachezea tango usiku kucha kwa vumbi la kongo
 
Huko Liwale ndio home. Mimi ni mdogo wake Sheikh mkuu wa Liwale.
Liwale kuna watu wakatili sana ukizingua. Watanganyika wanapenda sana uzushi.
Mungu akuokoe .
Karipoti polisi, kuna dogo nimesoma naye hapo uliza afande Denis. Anaweza kukusaidia.
Ila kwa vichwa vya Liwale huyo sheikh ndo atakusaidia kwa haraka kuliko vyombo vya usalama. Maana huko sheikh ana nguvu sana
Si kweli,Niko liwale shule ya msingi Mpigamiti kwa zaidi ya miaka 20 ,watu wa huku ni wakarimu sana,huwezi sikia mauaji kama Kanda ya ziwa,kasikazini na kusini kama njombe.

Huyu mwalimu atakuwa na msongo wa mawazo,maana kiutumishi Kuna taratibu za kufuata na ikiwa anachotuhumiwa nacho si kweli,Kuna uwezekano wa kumhamisha nje ya wilaya.


Hivyo tatizo ni la mwalimu na si jamii,jiulize Kuna CWT,TSC,Afisa elimu, Mkurugenzi nk.wote hawa hawawezi msaidia hadi aje mitandaoni!?


By the way yeye kataja majina ya wale anaowatuhumu huku la kwake akilificha
 
Back
Top Bottom