Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Thanks and God bless🙏🙏
 
Nimesoma story yako yote hata sijaona kosa alilofanya mzee wako.
Kosa lipo kwenye ubongo wako kutafsiri vitu kiutofauti.
Inawezekana tu sababu ikawa ni msoto wa maisha uliopitia ukatafuta root cause kisha ubongo wako ukakupa jibu kwamba sababu ni mzee wako lakini si kweli maana vijana watu wengi wanapitia kwenye hiyo stage kabla ya kufanikiwa.
Mzee wako alisimamia jukumu lake kama mzazi katika kuwashepu watoto wake ila wewe ulikuwa unatamani life la kudekezwa kama wanavyolelewa watoto wa single mother.
Halafu kitendo cha wewe kuhama nyumbani kwenda kujitegemea na kupambana kwa kufanya vibarua vya kulipwa elfu 5 huo ni ujasiri ambao ni matunda ya malezi ya mzee wako,mtoto aliyelelewa kimayaimayai hawezi kujiongeza hivyo atatafuta shortcut ambayo inampeleka pabaya either awe chawa au shoga kwa hiyo hapo wewe inabidi kwanza umshukuru mzee wako kwa kukufanya uwe mwanaume kamili na pia ubadilishe mindset yako ya uadui uigeuze iwe urafiki kwa mzee wako.
 
We ni mhuni tu stori zenyewe umeaandika kihuni
 
Mzazi ni mzazi.
Kitu kikubwa ulichozungumzia ni kua baba yako alikua anakuendesha! Lakini ukiwa mzazi utaelewa kua hakuna kitu kigumu kama kumlea mtoto ili aje kua mwema.

Labda balehe ilichangia ugomvi kati yako na baba.
Nashauri uende kwa baba yako na umwambie kila kitu unachojisikia kuhusu past yenu.
Kama utashindwa kuongea kwa mdomo basi mpe barua.

Mkikaa mkiongea kila mtu atajua alikosea wapi na mtarudisha upendo kati yenu.

Baba yako anakupenda sana! Kuna sacrifices alizifanya mbele na nyuma ya macho yako ili wewe uwe bora na imara.
 
Mzazi anayeshape mtoto wake hususan wa kiume, huwa mtoto hampendi. Nakiri, kama baba yangu asingenitandika, ningekuwa sijui wapi.

First born wangu, aliamini nampenda siku ya graduation yake -degree ya kwanza.

Last but one, tangu form one nilimweleza kuwa Nahitaji 4 As katika Mtihani wake wa form four za PCMB ili ajihakikishie kwenda MUHAS! Kwa vile ili kijana ajihakikishie MUHAS lazima form six awe na A au B ya Physics. Niliumia alipopata zote A isipokuwa Physics form four. Kutokana na ukali wangu aliweza kujiongeza na sasa amemaliza MD ila MUHAS haikuwa riziki.

Mzazi lazima ukomae na mtoto ili baadaye achomoze.
 
Nimejaribu kusoma huu uzi na comment zote sijaona kosa kubwa la mzee wako mpaka kuandika maneno makali kuwa HAMPATANI....

Malezi yana changamoto sana na bila kusimama IMARA kama mzazi unajikuta mpaka una staafu watoto hawaeleweki. Mzazi bila kuwa imara ni kuzalisha kizazi kingine cha hovyo.

Kitu kimoja nimeona ni kuwa mama yenu alikua MPOLE sana na ALIWADEKEZA na alikua ndio mtetezi wenu pale mnapokaziwa na mtoto.

Kitendo cha wewe kusema unapenda DRAMA ni aina ya malezi umepata kutoka upande wa pili. At the age of 29 unapenda DRAMA kama mwanaume. Mzee asingekaza tungekupoteza.

Anyway we are not here to blame you au mzee wako.

Cha kufanya
1. Achilia moyo wako fanya mapatano na mzee wako. Hakuna jambo muhimu km hili. Fanya kabla haijawa too late. You arenold enough kuface hiyo kitu.
2. Anza kujenga familia yako upate majukumu ili upunguze hizo drama uingie kwenye majukumu uone mbilinge la watoto. Nina mtoto wangu now ni standard 7 nilikuja kushtuka darasa la 3 hajui kusoma. Mbugi alilopata hataacha kusimuliana ni wa kike. Now ni yupo atleast ishirini bora...
3. Usipange kudekeza watoto wako.
4. Punguza kuangalia movie za ulaya ukafikiri maisha ni sawa.
5. Get busy.
 
Pole sana kwa kutokua sawa na mzee, ushauri tu vyovyote uliyopitia jaribu sana kuwa naye sawa/utoe kinyongo kwani mzazi ni mzazi na ikitokea ametangulia basi itakutesa sana.
Kwa sasa unajitegemea hivyo nafasi ya wewe na yeye kukwaruzana haipo au ni nadra sana,piga simu mjulie hali&ukiweza fika nyumbani unapoweza ila usikae muda mrefu ukatengeneza nafasi ya mikwaruzano.
Ushauri mdogo tu usipende kuchanganya sana lugha mbili kwenye bandiko moja binafsi imenifanya nisimalize kusoma bandiko lako,maneno mawili matatu si mbaya ila umechanganya sana
 
Thanks brother umeongea kitu uzima sana

I will make more efforts to make him see my point of view, japo nimejaribu mara nyingi na ilikuwa fruitless.. Maybe approach haikuwa more consize..

Ila uliyo sema yote yako sahihi kabisa.

Kwao ilikuwa upendo, ila zama huwa Zina badilika..

Will work on your advice mkuu🙏
 

Ukishakuwa chini ya Mamlaka nyingine kudhibitiwa, kuamrishwa na kuwekwa chini ya ulinzi ni jambo la kawaida kabisa.

Ukiwa na himaya yako utaelewa.

Unachojaribu kueleza ni kuwa hujakua bado
 
Sijaona kosa kubwa la mdingi, nilichoona kwa ufupi tu ni aina fulani ya wazazi wanaopenda kuwalea watoto wao katika ile misingi mikali na migumu wakiwa na lengo la kuwaweka watoto katika mstari wanaoona ni sahihi kwao, wengi wanapenda kusema mzee fulani ni mkoloni kweli kutokana na strictness yake kwenye upbringing ya watoto, na kiufupi hii huweza kuwa na negative na positive side kwa mtoto hasahasa kisaikolojia, ila haipaswi kukufanya ushindwe kuweka mambo sawa na mzazi wako mbali na yote yaliyotokea still yeye ni mzazi wako na alikuwa analenga ustawi wako
 
I never said I dislike my Dad..

He taught me resilience and discipline, he's given his all to provide a life for me. I never dismissed that. We just have nothing to put us together for now, Atleast that's what I can say.

And, I'm not saying you dislike him. I'm simply saying you don't even have to like him to meaningfully connect with him. Talk to him frequently about different subjects. You will find something you both agree on. Then use that to cultivate a positive relationship with him. You obviously also have your own psychological issues. Work on those separately with the help of a professional or religious therapist.
 
Watu wengi hawakupaswa kuwa wazazi ila huwa wanalazimisha tu.
Sidhani hii kauli ni nzuri kuitumia
Hakuna asiyependa kuwa mzazi. Na kila mtu ana uhuru wa kuwa mzazi...

Nobody wanna do bad things but they just do it for lack of love, they come from a place of insufficiency
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…