Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Ukija kupata watoto wako na kuwa na familia yako ndiyo utaelewa Mzee wako alikuwa namna hiyo kwa sababu zipi. Licha ya kuwa umeshaanza kutambua msingi wa maisha yako na nidhamu alikujengea imetokana na hayo malezi. Bado utajua zaidi

Kwa umri wako uliyotaja wewe ni Gen Z, mikumbo ya wenzako wa umri hup isikupoteze mwelekeo ukamuona Mzee ni mbaya. Ana upendo mkubwa sana kwako na angekuwa hakupendi hata kukuhudumia na kukusomesha asingefanya.

Unatakiwa ujue baba zetu wanaficha mengi sana vifuani mwao na pia ni wagumu kuonesha hisia zao za waziwazi aa upendo kama mama zetu. Hadi unapewa huduma muhimu, ukiumwa unatibiwa na umesomeshwa mpaka unatoka home. Unaona kayafanya hayo yote sababu gani? Yaani unaona msaada wake kama mtoto kaumaliza ndiyo unaapa usirudi nyumbani hata kumsalimia.

Ndugu nikwambie kama ni upweke wa mzee wako na kutaka walau urudi, kugoma ni utamtia msongo wa mawazo uje kumfanya augue na kupoteza maisha mapema. Huwezi jua uwepo wako wewe kwake una maana gani.

Wanaume hatutamki nakupenda ndiyo ujue mzee wako anathamini vipi. Usisubiri mpaka uje kumpoteza ndiyo uone ana umuhimu gani kwenye maisha yako. Wakati huo una majuto makuu moyoni mwako, utatamani muda urudi nyuma huwezi.

Kuhusu suala la mama yako naomba nisiliguse sana. Ila nikwambie tu yanayotokea ndani ya kuta nne za chumba cha wazazi waachie wenyewe. Huwezi ukawa unajua kila kitu kuhusu mambo yao na hakuna hata mmoja ambaye atakuwa tayari kukueleza kila kitu kuhusu maisha yao. Kujifanya kuchukua upande na kulaumu mmojawapo ni kufanya makosa sana. Na wewe utakuja kuwa na watoto utayaona hayo pia.

Muda ambao utayajua kuwa ya wazazi ni ya kubaki nayo wenyewe. Ndiyo utajikuta ukijuta. Sasa nakushauri usije kusubiri uje kuishi maisha ya majuto kisa mihemko ya hisia zako. Tulia


Hatukuzaliwa na kulelewa na malaika, bali na wanadamu kama sisi. Wana mapungufu na kukosoea kama sisi..... Mzazi mmoja hisia zake ni ngumu hata kama mwenza wake ana mapungufu hawezi mwambia mtoto, mwingine ana hisia dhaifu huweza yasema yote. Chukua mazuri ya kila mzazi yawe mfano, mapungufu jifanye hayakutokea

Baba yako hawezi kukwambia mapungufu ya mama yako, sababu atakuwa anajitukana mwenuewe kukuonesha alikuwa mzembe hakuchagua mama bora. Anakaa kimya kumpa heshima mama na wewe pia... mama ni tofauti sana ingawa wapo wachache wanaficha pia.
​
 
Mkuu katika hiki ulichokiandika mfano nikisema unioneshe convincing part inayoelezea ubaya wa mzee wako, unadhani unaweza ku point maelezo gani?
 
Yote kwa yote tafuta hekima ya kuwa sawa na mzee wako kuwa na bifu/kuwa na kinyongo na mzee wako wont do any good to you.either way kisaikolojia ama kiroho..

Hata kama baba mzazi alimuacha mama yako akiwa na mimba yako na akakukataa ya i alikutelekeza hakukutunza hakukulea,bado ni BABA yako,ni afya kiroho na kisaikolojia ukatafuta nafasi ya kusamehe ,KINYONGO hakimsaidii aliyebeba,ila ni mzigo wa msumari ni sawa na kukumbatia moto kadiri unavyoukimbatia moto kwa muda mrefu ndio unavyosababisha madhara zaidi kwako uliobeba kinyongo/moto.KIROHO,KIAFYA.--haina afya kiroho wala kimwili.
 

Attachments

  • images - 2026-05-10T233420.347.jpeg
    11.7 KB · Views: 9
  • FJWGvWaVQAI2GZ7.jpg
    68.3 KB · Views: 9
NELSON MANDELA aliwasamehe waliomtesa.
Mtego wa Siri wa Kinyongo na Kukwazika (Offense)

Eneo kubwa la tahadhari katika ujumbe huu ni mtego wa kiroho wa kukwazika au kubeba kinyongo moyoni, ambao shetani anautumia kama silaha ya siri kuzuia baraka.

Maana ya "Scandalon": Neno la Kigiriki la kukwazika (offense) ni scandalon, ambalo linamaanisha kichocheo au kifyatulio cha mtego wa mnyama unaoshikilia chambo. Kubeba kinyongo ni kuingia mwenyewe kwenye mtego wa adui.

Kuzuia Ustawi na Upambanuzi: Kinyongo kinapooza uwezo wa mtu wa kusikia sauti ya Mungu na kinazuia upambanuzi wa kiroho. Hata kama mtu ana karama kubwa, hawezi kuvuka kutoka kipindi cha upweke/majaribio kwenda kwenye kipindi cha kudhihirika kwa baraka kama hajakatisha/hajaondoa kinyongo moyoni mwake.


Kujaribiwa kwa Imani:
Mungu anaruhusu majaribu kupitia watu au mazingira ili kusafisha na kuimarisha imani ya mwamini (1 Petro 1:6-7), na si kwa ajili ya kumharibu.

Mtego halisi sio yule aliyekukwaza, bali ni kile ambacho kinyongo hicho kinatengeneza ndani ya moyo wako

yani ule uovu ama maumivu ambayo adui yako amekutendea au amekukusudia ukupate,USIAMUE jinsi wewe utakavyoishi,utakavyopokea.

MFANO YOSEFU alitendewa mabaya na ndugu zake walimkusudia mabaya lakini ,moyo wa Yosefu haukuweka KINYONGO juu ya ndugu zake wale waliomtendea mabaya

Mwanzo 50:20
Nanyi kweli mlinikusudia mabaya ,bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.

kama Joseph angeweka kinyongo angelipa mabaya kwa ndugu zake kumbe Mungu aliwakusudia kuwaokoa.

Ni sawa na STEPHANO alipigwa mawe na miongoni mwq waliompiga mawe alikuwepo SAULO ambaye baadae alikuja kugeuka moyo na kuwa mtu maema na kuwa PAULO..kama Saulo angweka kinyongo na kuwalaani waliomkosea angelaani mtu ambaye amebeba kusudi la Mungu.

Yesu aliwasamehe wale waliomsulubisha waliomtundika msalabani ambao ni mimi na wewe kwa dhambi zetu

Kupitia kuwaombea wale waliokuwa wanamcheka AYUBU akapona uteka wake /ugonjwa wake.
Mt 5:44
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi

BE KIND to UNKIND people they need it the most.
Apostle Miz Mzakweh Tancredi
Mt 6:14-15

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
 

Attachments

  • Screenshot_20260816-163343.jpg
    40.3 KB · Views: 7

View: https://youtu.be/S2yvp8KgjWw?si=MTzWKBgVsrKEWnXT
 
Nashangaa sana mnao waheshimu wazaxi wapumbavu na washenzi .... mtu yoyote anaye taka kuheshimiwa ni lazima yeye awe wa kwanza kuwaheshimu hao anaotaka wamweshimu na si vinginevyo ...
 
yani mtu kabisa anasesema ana BIFU NA MZAZI WAKE,...duh..!!..Mungu atusaidie.,mwingine anatangaza kabisa kwenye vuombo vua habari..hamtaki mzazi wake,ukiuliza kwanini anasema mama yake kamwambia baba yako alikuwa mbaya alinitekeleza mimi mama yako na wewe alikukataa...kwa hiyo mama anamwambia kijana wake..AMCHUKIE BABA YAKE.

mzazi ni mzazi tu hata awe mlemavu,awe kichaa ,hata kama alikutelekeza..HUTAPATA BABA MWINGINE.. huwezi kumfuata baba wa mtu mwingine useme ,wewe utakuwa baba yangu..baba yako ni MMMOJA ..unaweza wewe ukawa na watoto wengi ila baba yako ni MMOJA tu baba yako mzazi.

na kuna maana yake na faida yake KUWAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO...kuna faida yake na MUNGU AMEAGIZA HIVYO.

kuwa na bifu na wazazi wako haitakusaidia hata kama unajipa matumanini na kujifariji kwa muda ila that thing will hunt you for the rest of your life...

kuna siku unaweza ukamtafuta mzazi wako umuombe msamaha na utamuona siku ukimature kiroho uko mbeleni...KINYONGO NA HASIRA..hupofusha macho..siku macho yakifunguka unaweza ukamtafuta na asiwepo ,ukatamani umuombe msamaha usimuone.
 
Hayo ni mawazo yako. Hujui kitu kuhusu my mom.

Bro, hapa umejibu ww?. ☺☺☺
Hongera.

Hakuna mtu anaweza akaumiza feelings zako bila ruhusa yako.
pamoja na positive comments kuwa nyingi, ila bado ziko zenye negative aspects.

And so far umeweza kuzimudu. Na ndio inatakiwa interaction zilizozo hasi udeal nazo kwa namna hiyo.

Stay calm and do not let mean comments hurt your feelings. Don't panic, they know nothing about you. Choose to ignore unkind comments and protect your peace of mind.
 
bifu na mzazi wako hiyo kitu itakutafuna kiroho milele,..
that thing will hunt you down for the rest of your life..

it is not normal kiroho mtu kuwa na bifu na mzazi wake.. hapo kuna roho ya shetani imeingia ..mpango wa Mungu watoto waheshimu wazazi wao..na waishi kama familia takatifu ya kumuabudu Mungu,mzazi na watoto wamuabudu Mungu.Wakae kwa amani na wakipendana la familia..
 
We jamaa ungekua karibu na huyo chalii ushamlamba makofi. Umeushambulia uzi fasta fasta imagine ungekua unaongea naye live😀😀
 

Umejimaliza sana Mtumishi.

Hana bifu na mshua wake.
Bali hana mahusiano mazuri.

Heshima na vyovyote anavyostahili kumpa Mshua wake anampa kama inavyopaswa.
 
Mkuu umeongea kitu sensitive sana ambacho hata wengi humu wamekuwa wakikwepa.. You're so wise mkuu.. Pole kwa kupotelewa na mzazi, najua maumivu ya kutoa kuwa na mahusiano mazuri na wazazi, yanaumiza gradually na huwa ni ngumu kupona... Na ukweli ni kuwa kunapokosekana amani upendo hukosa maana tena.

Just try to resolve old wounds, anza hata kujenga mazoea upya na wanafamilia.. It will get better.
Na wazungu wametuzidi hapo, sisi emotions huwa tunazitupa pembeni kabisa. Ila ndo chanzo cha kila kitu... Wengi wanaona addicts mitaa I wanadhani ili anza to without any reason.. Huwa kuna deep emotional and psychological wounds zinapelekea watu kuwa vile
Na hata Michael Jackson aliwahi kusema "my childhood was stolen away from me"

No wonder alikuwa na mazoea sana na watoto. Ili a cope au kuheal kile mzee wake alimwibia utotoni

Thanks brother, it will get better
 
Umejimaliza sana Mtumishi.

Hana bifu na mshua wake.
Bali hana mahusiano mazuri.

Heshima na vyovyote anavyostahili kumpa Mshua wake anampa kama inavyopaswa.
Naona jamaa anaquote Bible kama njugu mawe aisee..

Ila ni sawa tu, maana vitu kama hivi huwa ni very sensitive na vina trigger sana watu
 
Wa

Waafrika hawana matatizo mengi ya kisaikolojia kama Wazungu wazungu ni waoga wa sheria tu ila wengi wana matatizo ya akili kuliko sisi.
Sio waoga wa sheria ila wanaheshimu sheria, wanaishi kwa mifumo na wanafuata mpangilio.

Sisi ambao mnasema "tumelelewa vizuri" Lakini vitu vidogo hatuwezi inakuwaje
 
Katika hilo uko sahihi,
I never want to have kids nije niwa treat like how my dad did. Thanks for your comment🙏
ww una tatizo la kutaka kulelewa kimayai mayai....ndio kizazi cha sasa jinsi mlivyo yaani hamtaki muwe ndani ya sheria, typical rebellious kids.

Haya malezi yanachangiwa na kina mama aka Wake zetu. Utakuta mtoto akifanya kosa badala ya kumdiscipline au kumkanya hapohapo , hafanyi anakusubiri mwanaume urudi kutoka kazini ndio akupe kesi za wanao. Hii inajenga picha kuwa baba ndio mkali wa kuadhibu na wa kuogopwa ila mama ndiye mwenye huruma na mpole anayepasea kukimbiliwa na watoto.

Haya ni malezi ya kinafiki ambayo binafsi niliyakataa kwa wanangu mara baada ya kuona mama yao anataka kuniletea pigo za mimi nionekane mkali sana,mtu wa kuadhibu na kufokea ovyo wanangu ili saikolojia na mapenzi yao yawe mbali nami.

Baada ya kulijua hili nikaanza kumwambia kuwa chukua fimbo na wewe uwachape ili nisionekane mbaya peke yangu kwa wanangu.

Hii age ya 0-10 kwa watoto ndio muda wa mtoto kujenga mapenzi na mzazi wake...akivuka hapo kama hajawa na ukaribu au mapenzi nawe basi usitegemee ukubwani kuwa karibu nawe.

Mtoa post subiri ukishakuja kuoa na kupata watoto ndio utakuja kumuelewa baba yako. Hakuna baba anayetaka watoto wake wawe mayai viza. Baba ndiye mchungaji wa familia.
 
Nashukuru Nimesoma yote na Nitafanyia kazi🙏🙏
 
📌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…