Mimi naamini kila dhambi lazima uilipie

@To yeye unajua kwamba kuna KARMA NA FATE?

Karma tafsiri yake ni kuwa yanayomtokea binadamu ni matunda ya matendo yake ya nyuma.

Fate ina maana kwamba yote yalishapangwa. Kila hatua ambayo mja huipiga ilishaamuliwa kabla hajazaliwa.

Ni ufafanuzi; kwamba mja hana uchaguzi mbele ya Fate (hatima). Kwamba umwonavyo mja na maisha yake, ndivyo alivyopangiwa kuishi kabla hajazaliwa. Anafuata rasimu iliyoandikwa kwa ajili yake.

Anavyoishi binadamu leo ni matokeo ya aliyoyatenda jana. Hiyo ndio Karma. Mantiki ni kuwa mja anaweza kuamua kesho yake iweje kulingana na matendo yake ya leo.

Hapo kwenye Karma na Fate kuna mifano mingi sana ambayo hata nikiifugulia thread itafikirisha sana akili za watu.
Mimi kwa upande wangu nitafanya yale mambo ambayo hayapo kinyume na imani za kidini pamoja na sheria na taratibu zilizowekwa na mamlaka. Sitafanya jambo kwa ajili ya kuwafurahisha au kuwakasirisha watu japo hii ni ngumu sana.
 
Hakuna kitu kama hicho sijui Karma hizi ni myth kutafuta sympathy na ukiwa unafikiria sana kuhusu karma utakuja kuwa mnyonge na dhaifu nimekuelewa sana Mkuu. Tujitahidi kufanya yaliyo mema tu. Tumeshasaidia sana watu na walipofanikiwa wakatu dharau na kutuona hatufai tena ni ndugu. Sasa kama utaisubiri application ya karma na yule aliyekufayia ubaya yeye bado anazidi kufanikiwa tu. Tuachane na hizi mambo ni kitu cha kawaida tu. Nitaanzisha uzi na kuweka mifano ili watu waelewe waondokane na mambo ya kusubiri karma ifanye kazi yake.
 
Ukitegemea Karma, utasubir sanaaa !!


Uje ulete huo uzi Mkuu ,watu wengi Sasa hawana skills za Maisha.
 
Nimeandika hapo kama kuna karma basi kuna fate pia. Mfano DiamondPlatnumz kamkataa baba yake hakuna lolote inalomtokea na anazidi kuvumbua ideas kibao na anawapa watu safari za kwenda chooni na Familia zao. Ndugu zangu hii ishu ya kusema Karma na blah blah nyingi ni kwa sisi ambao bado tupo katika safari za kutengeneza ile life tunayoitaka. Tuachane na mambo ya karma jamani. Mfano Nabii Mwamposa kule Moshi watu kibao walikufa je kuna karma gani inayompata. Nitaanzisha thread yenye mifano hai na inayoeleweka kabisaa.
 
ushapigwa tayari
 
Tunakufanyia ubaya na malipo hatuyapati wala nini, wafanya ubaya wengi ndo wametoboa kwenye hii maisha, wafanya wema wameishia kudhulumiwa na kuteseka Hadi mwisho.

Maisha hayahitaji roho nzuri kwa kias kikubwa yanahitaji watu wenye roho mbaya
 
Kila mtu anakinywea kikombe kwa namna yake, ndio maana wenye mali nyingi ndio wanaongoza kwa ukatili. Leo hii kuna wenzetu wamezikwa wapo kivyao kaburini.

Kila mtu atapatilizwa kwa mda wake. Do good or bad, you'll face it for shizzle!!
Hii sijui mnaita karma

Ni kujilisha upepo

Hakuna hiyo kitu

Sent from my TECNO BD4h using JamiiForums mobile app
 
Kimekukuta Nini? Pole sana mkuu ndo maisha
 
Tunakufanyia ubaya na malipo hatuyapati wala nini, wafanya ubaya wengi ndo wametoboa kwenye hii maisha, wafanya wema wameishia kudhulumiwa na kuteseka Hadi mwisho.

Maisha hayahitaji roho nzuri kwa kias kikubwa yanahitaji watu wenye roho mbaya
Time will tell
 
Diamond yupo sahihi coz alianza yeye kukataliwa anachokipata baba ndo alichokipanda
 
Mi naamini muda unaongea mkuu
 
Yote kheri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…