Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
@To yeye unajua kwamba kuna KARMA NA FATE?Mi naamini kila dhambi lazima uilipie.....ulipaji unaweza chelewa ila lazima muda ufike uwajibike.
Usichopenda kutendewa usimtendee mwenzio.... Usipende kuvuruga amani ya moyo ya MTU Mwingine kwa kumkomoa tu huku wewe ukiendelea kuenjoy.
Unadanganya kibiashara, kifedha, kifamilia, kijamii na kimapenz....pesa unakopa hulipi, unafanya biashara na MTU unadhurumu, unadanganyia pipi na kutishia visu watoto unawabaka, unamwahidi kumwoa unamwachia mimba unasepa, unaua wazazi kwa tamaa za Mali...
Unatelekeza familia sababu ya anasa.....unamwaminisha MTU mpo safari moja kumbe umeaminisha wengi-wastage of time(hili limenipata but time will tell).......Karma is real tusipojirekebisha wapendwa.
Karma tafsiri yake ni kuwa yanayomtokea binadamu ni matunda ya matendo yake ya nyuma.
Fate ina maana kwamba yote yalishapangwa. Kila hatua ambayo mja huipiga ilishaamuliwa kabla hajazaliwa.
Ni ufafanuzi; kwamba mja hana uchaguzi mbele ya Fate (hatima). Kwamba umwonavyo mja na maisha yake, ndivyo alivyopangiwa kuishi kabla hajazaliwa. Anafuata rasimu iliyoandikwa kwa ajili yake.
Anavyoishi binadamu leo ni matokeo ya aliyoyatenda jana. Hiyo ndio Karma. Mantiki ni kuwa mja anaweza kuamua kesho yake iweje kulingana na matendo yake ya leo.
Hapo kwenye Karma na Fate kuna mifano mingi sana ambayo hata nikiifugulia thread itafikirisha sana akili za watu.
Mimi kwa upande wangu nitafanya yale mambo ambayo hayapo kinyume na imani za kidini pamoja na sheria na taratibu zilizowekwa na mamlaka. Sitafanya jambo kwa ajili ya kuwafurahisha au kuwakasirisha watu japo hii ni ngumu sana.