“Mimi naiba tu sina kazi nyengine mjini, ukinipiga ukiniuwa utajua mwenyewe…” 😂

Ukimsikikiza dogo kwa kutumia moyo utaelewa dogo anasema hisia Kali zenye kuonesha kukatishwa tamaa na kusalitiwa na nchi pamoja na mifumo dhalimu.

Elimu duni ambayo haijampa SULUHU la kupata ujuzi Ili ajipatie mkate

Mfumo wa ajira kandamizi ambao haumtambui asiyekuwa na vyeti Wala kutambua kipaji chake.

Umaskini na kutengwa na wenye mamlaka ambao wako bize kuchuma na kuwatengenezea watoto na vijukuu zao, huku kwangu pakavu kama yeye wakitelekezwa kama mbwa Koko jalalani kujitaftia kwa namna ambayo lazima wale kwa jasho ama wafe kwa njaa Kali.

In short kama taifa tumefeli pakubwa sana.

Mungu wetu utupaye uhai na mkate wa kila siku lione taifa lako. Waone vijana wako ambao taifa ulilowapa limewatelekeza, wenye mamlaka wananeemeka wao na watoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…