Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Sawa ndoa ni kama nchi lakini bado kuna mambo mengi sana yanayotofautisha taasisi ya familia na taasisi ya urais kuna masuala ambayo unaweza ukafananisha hizi taasisi mbili na ikaonekana ni sawa kabisa, ila kwenye masuala mengine kama hii mada kufananisha urais na familia inakuwa irrelevant kwa mfano rais akiwa dikteta huwa ni kwa maslahi ya wananchi wake na si maslahi yake binafsi, haya unaweza ukaniambia mume anapokuwa dikteta huwa ni kwa maslahi ya nani yani mwanaume anapomtendea mkewe kosa kubwa kisha kutaka mkewe asimuulize wala asikasirike hilo ni kwa maslahi ya nani
 
Yaani huo udikteta unaouona kwenye ngazi ya juu ya uongozi(nchi), unahitajika hivyo hivyo katika ngazi ya chini kabisa ya uongozi (familia). Mume anakuwa dikteta kwa maslahi ya familia yake, kama mke anakuwa kizuizi cha maendeleo lazima amuweke sawa ili familia ikue kiuchumi, kama watoto wanaleta shida ni lazima(kwa namna yoyote) wawekwe sawa kwa maslahi ya familia.

Uongozi mbovu unaleta broken families and hence broken society.
 
Ndio maana nikasema tofautisha kati ya uongozi na unyanyasaji lakini naona umekwepa swali langu, kuna mambo unaona kabisa mwanaume anafanya kwa maslahi ya familia ila kuna mambo mengine unaona kabisa anafanya kwa maslahi yake binafsi, huku akiiumiza familia (hasa mke) ila as long as yeye yanampa furaha hajali anaona ni sawa tu sababu ni mwanaume
 
Mwanamke akiuona kama ni unyanyasaji anaruhusiwa kuomba kuachana, ila dhana ya 50/50 haipo na haiwezekani coz dunia ilipewa mtawala ambae ni mwanaume.
 
Mwanamke akiuona kama ni unyanyasaji anaruhusiwa kuomba kuachana, ila dhana ya 50/50 haipo na haiwezekani coz dunia ilipewa mtawala ambae ni mwanaume.
Na anapoomba kuachana inatakiwa jamii isimsimange wala kumdhalilisha kama inavyofanya sasa, yani inatakiwa mwanamke akiachana na mumewe ionekane ni kitu cha kawaida tu na maisha mengine yaendelee, kuhusu 50/50 bila shaka hujasoma mada umesoma kichwa cha habari tu maana niliandika kama wanaume hawataki 50/50 basi watimize majukumu yao kikamilifu ikiwemo kuhudumia wanawake
 
Tunarudi kulekule, mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe...

Hakuna mahali mwanaume anavunja nyumba yake. Kwa hivyo pointing fingers wala haitaisha.
 

Nimesema hivi;
Changamoto KUBWA iliyopo kwenye jamii ni kuwa; watu wanapigania mfumo ambao hawaja jiandaa kukabiliana na matokeo yake. Mfano: wanawake hawajawa tayari kulipa mahari, kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya familia na kuacha kujiona kuwa, wao wanasaidia tu nk nk nk
 
Tunarudi kulekule, mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe...

Hakuna mahali mwanaume anavunja nyumba yake. Kwa hivyo pointing fingers wala haitaisha.
Mkuu unaweza kunifafanulia ni kwa namna gani mwanamke ndio anavunja nyumba sijui ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe na siyo mwanaume, kwa mfano mwanaume ni mlevi mnyanyasaji na mzinzi wa kupindukia kisha huyo mwanamke akaomba talaka waachane hapo ni nani anakuwa kaivunja hiyo nyumba au ndoa kwa mikono yake mwenyewe, jibu lolote utakalotoa ningeomba liwe na ufafanuzi kama hutojali
 
Wanawake wana uhakika na wanachokipigania, ila ni wanaume ndio ambao hamtaki kuachilia mfumo dume, hivyo matokeo yake nao wanasita
 
Kama mmoja anataka awe fahari basi lazima amhudumie huyo anayemtawala na huo ndio msingi wa hii mada, huwezi kutaka kutawala halafu hutaki wajibu juu ya huyo unayemtawala ukianza kutaka kusaidiwa majukumu automatically unapoteza yale mamlaka, na kwa mwanamke ni heri awe single mother kuliko kuwa kwenye ndoa ya namna hiyo ndio maana siku hizi wale wanawake wa "natafuta wa kunizalisha nitalea mwenyewe" wamekuwa wengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…