Mimi ndiye niliyefanya soda iuzwe shilingi 500 badala ya shilingi 600

Mimi ndiye niliyefanya soda iuzwe shilingi 500 badala ya shilingi 600

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mwaka 2013 Agosti nilipewa kazi ya MBR (Marketing Representative Body) mkoa wa Lindi.

Kipindi hicho soda ya chupa ilikuwa ikiuzwa sh. 600 kwa kampuni zote za COCA-COLA na SBC/ Pepsi almaarufu.

Kipindi hicho kampuni ya coca-cola ilikuwa na mauzo makubwa zaidi ya Pepsi nikapendekeza mapendekezo kadhaa ikiwemo soda ya chupa iuzwe sh. 500 tu na nikatoa sababu.

Wazo likafika HQ Dar es salaam likapita, kampuni ya SBC /Pepsi ikapunguza soda na kuanza kuuza soda kwa sh. 500 tu huku coca-cola wakiendelea kuuza soda kwa sh. 600, hali ikawa ngumu kwao wakanyoosha mikono, wakabadili bei na kuuza soda ya chupa kwa sh.500 mpaka leo.

Majuzi ndio nimekumbuka, nilishasahau kuhusu hili jambo.

Haya mnishukuru basi ili niwafanyie jambo jingine zuri.

Sasa siko huko kwenye masoda tafadhali.
 
Back
Top Bottom