Mimi ndiye niliyefanya soda iuzwe shilingi 500 badala ya shilingi 600

Mimi ndiye niliyefanya soda iuzwe shilingi 500 badala ya shilingi 600

Kumbe wewe ndio ulishusha bei ya sumu?Soda ilipaswa kuwa ghali ili watu wasizinunue kabisa!Kama ni wewe nakutumia risala za Lawama!
 
Umeacha kaz ya ulinzi??
Nitaachaje huku inaniweka mjini na life linasonga?
Swali lako ni sawa na kumuuliza mhasibu umeshaacha kazi uhasibu?
Ulinzi sio alternative way ya kuingiza income, it's a career that pay
 
Hongera sana kwa hilo, umeonyesha uwezo wako, ila sasa kuna naoni ya wadau kuwa upambane ishuke hadi 150, mi naona 150 haijakaa kibiashara, pambana bei iwe 100.
 
Mwaka 2013 Agosti nilipewa kazi ya MBR (Marketing Representative Body) mkoa wa Lindi.

Kipindi hicho soda ya chupa ilikuwa ikiuzwa sh. 600 kwa kampuni zote za COCA-COLA na SBC/ Pepsi almaarufu.

Kipindi hicho kampuni ya coca-cola ilikuwa na mauzo makubwa zaidi ya Pepsi nikapendekeza mapendekezo kadhaa ikiwemo soda ya chupa iuzwe sh. 500 tu na nikatoa sababu.

Wazo likafika HQ Dar es salaam likapita, kampuni ya SBC /Pepsi ikapunguza soda na kuanza kuuza soda kwa sh. 500 tu huku coca-cola wakiendelea kuuza soda kwa sh. 600, hali ikawa ngumu kwao wakanyoosha mikono, wakabadili bei na kuuza soda ya chupa kwa sh.500 mpaka leo.

Majuzi ndio nimekumbuka, nilishasahau kuhusu hili jambo.

Haya mnishukuru basi ili niwafanyie jambo jingine zuri.

Sasa siko huko kwenye masoda tafadhali.
Hangaya waziri mwingine huyu hapa.
 
Kwa kuwa umeamua kujisifia ngoja nami nijisifie kidogo.
Mimi ndiye niliyependekeza bando za simu zisiwe zinaisha,ndiyo mitandao ya simu kama Tigo na Voda wakaja na kitu kinaitwa HALICHACHI bando.
 
Back
Top Bottom