Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Sijui kwako ndoa ina maana gani lakini kwangu Mimi ndoa ilinipotezea Muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu.

Sikuwahi kuwaza chochote kuhusu ndoa wala kuitamani, lakini siku moja nilikua natoka sokoni Mabibo naelekea nyumbani Magomeni Usalama, niliposhuka kwenye daladala kwa bahati mbaya niliteleza na kuanguka wakati navuka barabara. Mfuko wenye vitu nilivyonunua sokoni uliangukia pembeni.

Nilihisi aibu sana siku ile na kibaya zaidi mvua ilikua imenyesha majira ya asubuhi, lilijaa tope lililoniharibia Baibui langu. Eneo nililoangukia palikua na kijiwe cha Bodaboda. Kama uwajuavyo walianza kushangilia anguko langu kitu kilichozidi kunipa hasira lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kujiokotanisha pale.

“Pole sana Dada” niliisikia sauti hii nikiwa nasimama, aliyenipa pole alinipatia na mfuko wangu akiwa ameokotanisha vitu vyangu. Alikua kijana mzuri mtanashati sana, nilijikuta nikiwa na kigugumizi kumjibu

“Unaelekea wapi?”

“Nyuma ya sheli, usijali” nilisema nikiwa najipangusa tope kutoka kwenye Baibui langu jeusi, akanipa mkono wake

“Naitwa Salehe Mwinyimkuu” Alijitambulisha kwangu, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha nilimjibu

“Naitwa Saida”

“Nimefurahi kukufahamu, wacha nikusogeze” alisema, kwa msaada alionipa isingelikuwa hisani kukataa alichokiomba. Taratibu tuliikanyaga ardhi kuelekea karibu na nyumbani kwetu. Kwa muda mchache nilihisi kumjua kidogo, niligundua ni mpole, mwemye hekima na busara tele licha ya kuniambia ana Miaka 27 tu.

“Mimi nina Miaka 23” nilijitanbulisha kwake huku nikianza kunogewa na mazungumzo yake. Tuliongea mengi hadi kubadilishana namba za simu kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwa Mtu nisiyemjua.

Tulizidi kuwasiliana kwa zaidi ya mwezi mzima huku tukiwa marafiki wa kawaida tu lakini baadaye Salehe alinitongoza.

Nisiwe mwongo wala mnafiki hata kabla ya kunitongoza nilianza kumpenda hivyo kunitongoza alikua anatimiza wajibu wake kama Mwanaume kwani nisingeliweza kumwambia Nampenda isitoshe Mimi nilikua Bikra kwa wakati ule.

Tulianza mahusiano ya Kimapenzi lakini nilimwambia Salehe kuwa Mimi nimelelewa kwenye familia ya Dini sana, Baba yangu ni msaidizi wa Shekh Mkuu wa Msikiti wa Magomeni hivyo kama ananipenda kweli basi awaone wazazi wangu kwanza. Sijui tuseme alikua na kiu sana au alikua anahitaji Mke sana maana alilifanya hilo siku tatu tu baada ya kumwambia

Baba yangu alifurahi sana, Mama pia alifurahi zaidi akaniambia

“Mwanangu ndoa ni Nusu ya Dini, sisi Wazazi wako tunakutakia kila lililo jema, Mungu akuongoze” Daima Mama yangu alikua Mtu wa karibu sana kwangu, alisimama na Mimi kwenye kila jambo hata ambalo Baba yangu alipingana na Mimi.

Salehe hakutaka kuchelewesha alilipa Mahali siku iliyofuata.

“Wewe Kijana ni Mtu wa wapi?” Baba alimuuliza Salehe wakiwa katika mazungumzo ya kawaida, kama Mzazi ni lazima ahakikishe usalama wa Binti yake

“Kwetu Rukwa lakini nipo Hapa Dar Likizo” alisema Salehe

“Ooh! Unajishughulisha na nini?”

“Nimeajiliwa, Mwalimu wa Shule ya Msingi Rukwa Mjini”

“Utamtunza Binti yangu?”

Kwanza Salehe alicheka kidogo kisha akamwambia Baba

“Nisipomtunza Mke wangu nitamtunza Nani, wanasema Mbuzi unayemlisha ndiye utakaye mkamua maziwa” Basi Baba na Salehe wakaishia kuangua vicheko, ilileta raha sana.

Ndugu wa Salehe walifika tena waliazimia kuwa ndoa ipite kabla likizo ya Salehe haijaisha ili tuondoke wote kuelekea Rukwa, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitaolewa na kwenda mbali kama Rukwa. Kidogo nilipata huzuni, nilimzoea Mama yangu

“Usijali, hata Mimi niliwaacha Wazazi wangu Morogoro nikaja kuishi na Baba yako Saida. Umri ukifika hakuna la kukuzuia kuanzisha Familia yako” Mama yangu hakuacha kunitia Moyo. Baba aliachia tabasamu maana tulikuwa wote sebleni

“Ngoja niwaache muongee maongezi yenu ya kike” alisema Baba akaelekea zake Msikitini, zilipita siku kadhaa hadi siku ya ndoa ilipowadia. Ndoa ilipita salama, Siku ya pili tulianza safari ya kuelekea Rukwa Mimi na Mume wangu Salehe.

Bado nilikua Bikra wala hakunigusa usiku wa kwanza wa ndoa yetu hotelini kabla ya Kuanza safari, kwakua nami nikikua mgeni wala sikudai chochote kile. Tulifika Rukwa Usiku sana tena nikiwa ninasinzia, tulichukua Taxi hadi nyumbani kwa Salehe

“Karibu nyumbani Mke wangu, jisikie uko nyumbani kabisa na hapa ndipo tutakapoishi” alisema tukiwa tunashuka kwenye taxi, tulisimama mbele ya nyumba moja iliyo giza sana, sikushangaa sababu mwenye nyumba hakuwepo kwa muda mrefu. Nilijiegemeza kwenye bega la Salehe nikamwambia

“Mume wangu, ulipo nipo na nitaendelea kuwepo siku zote” lile Taxi liliondoka, kazi ya kuhamishia mabegi ndani ilianza. Salehe alikua ametangulia nami nilibakia nyuma nikikokota begi. Sijui ni mawazo yangu au nilisikia kitu halisi kabisa, nilisikia sauti za Watoto wakiomba Msaada

“Subhannah‼” nilishtuka, sikuisikia tena ile sauti maana mwanzo ilitokea ndani ya ile nyumba ambayo tulikua tukielekea. Mapigo ya moyo yalinienda mbio, niliposikiliza vizuri wala sikuzisikia tena nikajua ni fikra zangu tu. Basi niliendeelea kuvuta begi hadi ndani, taa zikawashwa

Palikua kimya sana, uzuri sikua na njaa wala hamu ya kula zaidi ya Kulala kutokana na Uchovu wa safari. Nilisimama kusuburia Salehe anioneshe chumba chetu, akaufunga mlango kisha akaniongoza hadi chumbani, nilipofika nilijitupa Kitandani na kujilaza kama pono bila kujali kuwa kitandani palikua vumbi tupu.

Nililala Usingizi wa nusu kifo hadi mapambazuko, sauti ya jogoo kuwika niliisikia ikiniamsha na kuniambia ni muda muafaka wa kuanza majukumu ya nyumbani. Macho yalijawa na Ukungu usio kifani, nilijinyoosha kama Kinda la ndege halafu nikajikuta nikipigwa na Butwaa zito sana ambalo kiukweli nilishangazwa mno na nilichokiona

“Nipo wapi hapa?” Nilijiuliza swali hili, niliipapasa akili yangu inikumbushe jambo lakini haikua tayari kufanya hivyo, Salehe hakuwepo Kitandani. Moyo ulinienda hali Jojo, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani.

Nitakueleza kwanini nilipigwa na Butwaa la ajabu, kwanza harufu ya Udi wenye harufu mbaya ilizagaa kote ndani, pili nilisikia sauti ya Mtu akitwanga na kwa hakika alikua akitwangia ndani halafu sauti ya Mtoto Mchanga anayelia nilizidi kuisikia. Taratibu nilitaka kujuwa nipo wapi haswa maana tayari nilianza kupata hofu fulani

Nilipiga hatua za taratibu hadi mlango wa kutokea chumbani, ile sauti ilitoweka na palikua kimya sana. Moyo wangu haukutulia kabisa licha ya ukimya wa ghafla niliousikia, jua lilikua tayari limeshatoka

Nyumba ilikua safi sana. Ilikua na korido ndefu yenye vyumba kadhaa japo kwa wakati huo sikuhesabu kutokana na hali niliyokua nikiihisi. Basi Mimi Saida nilijiuliza

“Ah ni mawazo gani haya Jamani, Ewee Allah niepushie Mbali” nilisema kisha nilirudi Chumbani kutafuta simu yangu nimpigie Salehe aniambie alipo si unajua maisha ya Ugeni yanavyoanza. Nilikumbuka mara ya mwisho simu niliiweka kwenye mkoba wangu

Sikuwa na shaka sana kuhusu simu yangu, niliikuta lakini kwa bahati mbaya ilikua imeisha chaji. Niliketi kitandani nikiwaza mambo kadhaa lakini niliona ni bora niweke simu chaji niwasiliane na Salehe

Nilipomaliza kuweka chaji na kuhakikisha simu yangu inaingia chaji nilipata nafasi ya kukiangalia kwa uzuri chumba, kilipangwa vizuri sana hadi nilijikuta nikitabasamu, nilijuwa ni Mume wangu Salehe alikua ameamka mapema na kuweka mazingira sawa. Nilijiona ni mwenye Bahati sana kuitwa Mke wa Salehe, nilikua na nguo zangu zilezile nilizokuja nazo hivyo wazo la kubadilisha nguo lilinijia lakini kabla ya kufanya hivyo nilisikia Mlango wa nje ukigongwa.

Sikujua naanzia wapi kuitikia wito huo, nilisogea hadi mlango wa chumba na kusikiliza vizuri. Mgongaji wa mlango alikua ni Mwanamke na sauti yake ilikua karibu sana hivyo kwa haraka niliamini anagonga mlango wa Nyumba ya Salehe. Hakuna aliyeitikia ile hodi hadi pale nilipoamuwa kumkaribisha nikiwa ndani tena kwa sauti ambayo aliisikia vizuri, nilijiangalia kama nilikua nipo sawa kutoka ndani kisha nilianza safari mara moja kutembea kwenye korido kuuelekea Mlangoni.

Niliufungua mlango wa kwanza kwa kutekenya kitasa tu kisha nikauelekea mlango wa Uwani ambao ndio mgongaji alikua hapo, nilipoufungua nilikutana na Mama Mmoja aliyebeba tenga la mboga mboga kichwani, alikua ameshakata tamaa alikua akiondoka nikamwita

“Mamaaa‼” alipogeuka alirudi hadi Mlangoni

Shikamoo Mama” nilimsalimia kwa adabu, ndivyo nilivyofundishwa kwetu kwa wazazi wangu, yule Mama alitabasamu kisha akaniuliza

“Hauchukui Mboga leo?” Nilitabasamu maana aliuliza kana kwamba alishawahi kuniuzia mboga ila nilielewa Lugha ya Kibiashara huwa hivyo mara zote

“Mimi ni mgeni hapa Mama, labda kesho nikiwa nimeyafahamu vizuri mazingira naweza kuchukua. Usiache kupitisha” nilisema kisha yule Mama aliondoka huku akiitikia

“Napita kila siku Mtaa huu, Wahiiii mboga mboga” alienda mbele zaidi kisha alitokomea machoni pangu. Kuzungumza na yule Mama ni kama kulinisahaulisha kuhusu Salehe lakini alipoondoka nilijiuliza

“Salehe ameenda wapi mbona hajaniaga?” Niliufunga mlango kisha nilirudi ndani, Nyumba ilikua kubwa ya Kisasa lakini ilikua kimya sana sikusikia hata sauti ya ndege kuruka. Uwani

palikua na sehemu ya kukaa nikaona ni bora nikae hapo kwanza nipate upepo, nilijikuta nikipitiwa na Usingizi wa ghafla tu.

Ndoto za hapa na pale zilinifuata usingizini na kunipa hekaheka hadi nikashtuka. Niliposhtuka nilikutana na sura mbili, moja ilikua ya Salehe na nyingine ni ya Mzee mmoja mweusi aliyevalia Baraghashia nyeupe na kanzu nyeupe. Macho yao yalikua kwangu

“Eeeh imekuaje umelala hapo Mke wangu?” aliniuliza Salehe, nilijitabasamisha kidogo kama Mtu anayezuga ili asinione kuwa mvivu

“Hewa ya hapa inavutia, kaupepo nikajikuta nasinzia tu”

“Sawa, huyu ni Baba yangu anaitwa Mzee MwinyiMkuu. Ni Baba yangu Mzazi” alisema Salehe, nilimsalimia yule Mzee kwa heshima sana hata naye alifurahia na kuona ni namna gani nina heshima.

“Marhaba Mkwe wangu mzuri, hakika Mwanangu hakukosea’’ akasema kwa Utani tukajikuta tukicheka kidogo

“Samahani, najua umenitafuta ila nilienda kumpokea Baba maana aliniambia nikirudi tu atakuja kwa ajili ya kukusalimia wewe Mke wangu” alijielezea Salehe, ni kweli Mzee MwinyiMkuu alikuja na begi dogo la Mgongoni lililochakaa sana.

Aaaah! Nimefurahi sana kumuona Baba yako Salehe, karibu Baba.” Nilisema kisha nilisimama na kulishika begi la Mzee MwinyiMkuu ambalo lilikua sakafuni, kabla sijaliinua yule Mzee alinishika mkono kwa nguvu sana hadi nilishtuka, nikamtazama Usoni alikua amenikazia sura yake

“Hili begi halishikwi na kila Mtu, Salehe unajua pa kulipeleka” alisema Mzee MwinyiMkuu, nilihemwa maana sikutegemea lakini hata kama ningelichukua ningelipeleka wapi wakati na Mimi ni Mgeni pale. Nilishusha pumzi, kilinishuka nikarudi kukaa, Salehe akaniambia

“Mzoee Baba yangu ana utani sana Saida, wacha nikaweke begi lake nakuja” Mara moja alipomaliza kusema alinyanyuka Salehe na kuelekea ndani, yule Mzee hakuacha kunitazama kwa jicho kali kama vile kuna kitu nimeharibu hadi nilianza kumwogopa, ikanilazimu kumwomba Msamaha

“Samahani Baba sikujua”

“Siku nyingine uwe unauliza, umeelewa?”

“Ndiyo Baba” Nilipomjibu alinikata jicho fulani la husda kisha akatoa mguno fulani wa kicheko cha dhihaka halafu akanyanyuka na kuiburuza kanzu yake akaingia zake ndani,nilishusha pumzi zote kama Mgonjwa wa Pumu. Niliusikia moyo wangu namna ulivyoamka nakuanza kudunda tena, hata koo ilianza kupitisha mate kwa kasi. Yaani sijui nikueleze vipi unielewe namna nilivyokua nimeshikwa na woga kupitiliza, sura ya yule Mzee niliyona imekaa kikatili sana

Wakati naendelea kujiuliza mara Mume wanu Salehe alirudi kutoka ndani, akaketi mahali alipokua ameketi Baba yake

“Baba yako ni Mkali sana Salehe hadi nimeogopa. Nimefanya kipi kibaya, kumsaidia Begi ni vibaya eti?” Nilimuuliza Mume wangu, yeye akanishika bega akaniambia

“Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizo kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaa hapa.

“Ina maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?”

“Ndiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?” Basi kuzungumza na Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Salehe akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo huku dimpozi zangu zikionekana
Title imekaa vizuri sana ila kinachosikitisha ni story ya kutunga
 
Ilipoishia “Shiii‼” Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisu kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia

“Leo utajuwa ni kwanini uliolewa Binti” Alisema halafu akayaongea maneno fulani nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lugha nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaenda kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi. Endelea

SEHEMU YA NNE

Nilikua kama naangalia filamu vile, hata wewe msomaji unaweza fikiria ilikua ni filamu na ninakusimulia hapa. Hapana ni Simulizi ya kweli, simulizi hii ikusaidie kufanya chaguo sahihi wakati wa kuolewa au Kuowa ili usije pitia kama Mimi, haya mambo siyo tu kwa Mwanamke hata Mwanaume anaweza tendewa hivi. Tuendelee sasa

Mate hayakumezeka wala pumzi hazikutulia, yule Mzee alikua amenikata jicho kali kisha kaniambia kwa maneno yenye vituo vingi kuashiria kuwa anamaanisha anachokisema, akaniambia

“Umeolewa ili uje kuishi na Misukule hapa, huu ndiyo utajiri wangu. Wewe siyo wa kwanza kuolewa na Salehe, walioenda kinyume walifia humu na kupotea kabisa wao pamoja na Familia zao” Yaani nilizidi kuishiwa nguvu, Mungu wangu jasho lilinitoka kama nimemwagiwa maji. Kisha Mzee akaendelea

“Hii ni nyumba yangu Mimi siyo ya Salehe, yule ni Mtoto wangu na ndiye anayenisaidia Mimi. Utakua unafanya mapenzi na Msukule mmoja mmoja Kila baada ya Siku tatu. Usijaribu kutoroka ndani ya nyumba hii wala kutoa siri popote, narudia kwa Msistizo ili uelewe ninachomaanisha. Utawaponza Wazazi wako kwa Ujinga wako mwenyewe” Chozi lilizidi kunitoka kisha yule Mzee akasimama akaninyooshea Kidole

“Utafanya niyatakayo ili kuilinda familia yako, hutaruhusiwa kutumia simu na hutatoka nje isipokua kwa maagizo maalum kutoka Kwangu” kisha yule Mzee aliondoka zake na kunicha ndani ya kile chumba, wala hakunifungia kuonesha kuwa anajiamini na anachokisema. Kiukweli Nililia sana kwa kwikwi, nililia Mno sababu niliona wazi kuwa ili wazazi Wangu wawe salama napaswa kutumikia Misukule ya yule Mzee na kama nataka kuwa huru basi nitawapoteza Wazazi wangu ambao hawakuwa na Hatia yoyote ile.


Katika Maisha yangu niliutunza usichana wangu kwa ajili ya Mume wangu lakini nililazinika kuutoa kwa Misukule, nilijilaumu kwa kumwamini Salehe, nilimlaani sana. Nikiwa ninalia akaingia tena yule Mzee akiwa amehamaki akaniuliza

“Simu yako ipo wapi?” alishikilia kisu mkononi, sikupepesa maneno nilimpa simu mara moja kisha akaondoka nayo. Wala hakufunga mlango aliuwacha wazi ikiwa ni ishara ya kuniruhusu kuwa huru ndani ya nyumba lakini siyo kuondoka, ndiyo kwa mara ya kwanza katika Maisha yangu niliushuhudia Uchawi wa waziwazi.

Basi, nilirudi chumbani nikiwa ninalia, nilikua mwenyewe kwenye Maisha yangu. Sikuwa na Mtu wa kumueeleza ninayopita, sikuwa na msaada na pengine kaburi langu lingekuwa ndani ya ile nyumba. Kitu cha kwanza kufanya kilikua ni kufuta chozi langu, kwanini niliruhusu lidondoke chozi langu lenye thamani kubwa. Hata ningelia vipi isingelisaidia Mimi kupona

Nilijiegemeza kwenye Mto nikatafakari mengi, nikapata jibu la uhakika kabisa kuwa siku ile nilifanya mapenzi na Msukule na ndiye aliyenitoa Usichana wangu kwa mara ya kwanza nikifikiria ni Salehe. Kitu fulani cha uchungu kilijaa kifuani pangu, hakika nilitendewa unyama sana na Salehe na Baba yake. Nilijua Baba na Mama wangekuwa na wasiwasi na Mimi kama nitakaa kwa siku nyingi pasi na kuwasiliana nao lakini ningefanya nini sasa na ilinibidi nikae nao mbali ili kuokoa Maisha yao.

“Eeh Mungu, umeniptisha kwenye Mtihani gani sasa. Hukuona mitihani mingine rahisi kwangu isipokua huu?” Nilituma lawama ma maswali kwa Mungu wangu, kumbe ukiona Mtu anamkufuru Mungu si kwa kutaka bali kwa kukosa majibu sahihi ya kuondoka kwenye matatizo.

***

Masaa yalienda, sikupata hata lepe la kuusingizia Usingizi yaani nilikua na kichwa kizito sana japo Usiku ulikua umeenda. Hakuna sauti ya kutisha niliacha kuisikia Usiku huu, yaani Mzee Mwinyimkuu alinionesha Uchawi dhahiri kabisa. Sauti za Watoto Wachanga nilizisikia bila kificho, nyimbo za ajabu ajabu ziliimbwa na kuchezwa nikajiona kama nimeshafika kuzimu. Nikazikumbuka Riwaya kadhaa nilizokua nazisoma mtandaoni na stori za hapa na pale juu ya Uchawi, nilikua siziamini lakini hatimaye nilijikuta ndani ya moja ya Riwaya ya kutisha sana.

Mimi Saida nilikosa majibu ya maswali yote hata yale madogo niliyojiuliza. Bundi walisikika Usiku kucha, hadi kuna pambazuka nilikua macho hata taa sikuizima kwa kuhofia kuingiliwa tena na yule Msukule. Kukesha macho usiku mzima haikua rahisi, macho yalivimba hasa ukizingatia nililia sana

Niliogopa kutoka chumbani, sikuwa na amani kama siku ya kwanza. Nilikaa kitandani nikipiga Mihayo, mara Mlango uligongwa, nilishtuka nkasema moyoni sasa naenda kupelekwa kwa Misukule, hofu ikaamka upya ndani yangu lakini nikamsikia Mzee Mwinyimkuu akisema

“Amka uandae chai haraka” alisema kwa jazba fulani baada ya kugonga kwa kitambo kisha nikayasikia makubhasi yake yakifanya safari kutoka mlangoni kwangu. Moyo ulinidunda sana kiukweli, sikuwa na raha wala amani yoyote ile. Ningefanya nini zaidi ya kuamka na kwenda kumwandalia chai yule Mzee, Binafsi sikuhisi njaa kabisa licha ya kutokula jana kutwa nzima.

Niliufungua Mlango taratibu sana, nikasikia kama Mtu anafanya Usafi hivi, nilipoangalia vizuri niliona tu ufagio pekee ukifagia bila kumwona aliyeushikilia ule ufagio, nusura nizame tena ndani kwa woga lakini nikapata kiu ya kuona zaidi. Huuu‼! Uchawi unatisha sana na nimeushuhudia laivu bila chenga, niliporudisha macho tena sikuona chochote isipokua nyumba ilikua safi sana

Basi nikaanza safari fupi ya kupita koridoni na kuelekea jikoni kuandaa chai ya Mzee Mwinyimkuu. Ile naingia tu nikakutana naye ndunda ndunda.

“Muda wote ulikua unafanya nini wewe?” aliniuliza kwa hasira sana kama vile tulikua tumegombana. Hofu ilinianza upya hata sikuweza kutoa sauti yoyote ile, nikainamia chini, Jamani nilikuja kushtukizwa na kibao cha shavu la kushoto hadi nikahisi giza. Alinipiga kibao kizito hadi nikapepesuka pembeni, mateso makali yalianza kwangu

Sikuweza kutoa sauti yoyote ile isipokua chozi na maumivu yaliyojaa ndani ya Moyo wangu.

“Usiniletee upumbavu, hukuja kulala hapa wala kutembea. Kumbuka maneno yangu, Utafia humu ukileta kiburi, pesa hii hapa Nunua chapati urudi haraka” alisema Mzee Mwinyimkuu, akanipa Elfu tano mpya kabisa. Kisha yeye aliondoka zake akaelekea sebleni, alionekana anajiamini na maneno yake ndiyo maana aliniruhusu nitoke nikamnunulie Chapati, wakati nataka kutoka akapaza sauti yake akaniambia ninunue chapati za hela yote

Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule Mchicha nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku moja tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yule Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.

Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikua wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. Nilitamani nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na Mzee Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha……….
Kuna uwongo fulani humu
 
Back
Top Bottom