Mimi ni Mkristo mlokole, nimeanza kukosa Imani na ukristo nahisi Uislam ndiyo dini ya kweli

Kokote uendeka uzushi ni uleule hakuna cha siku ya mwisho wala mwanzo ni kujiliwaza tu kama binadamu.
 
Na wengi wa viongozi ni ukimwi tu
 
Mkakati ni ule ule haujawahi badilika,

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Marko 16:15-16
Aliyewahi kuona hiyo hukumu ni nani?
 
Hapo umenena, naamini uniuia kufanya kitu kitakuwa pasipo kwenda kwenye hayo majumba.
 
Kwahiyo mke zaidi ya mmoja kuna athari gani?!
Kwamba bora mke mmoja 'na vimada?
Mzee ukitaka battle hatutafika mimi naandika fact siandiki nisiyoyajua screenshot uliyoweka hapo sijui inahusiana nini na ulichoni-quote.

Tanzania hii wengi wetu ni maskini wa kutupwa ni wangapi wenye uwezo wa kulisha wake wanne na watoto kumi na mbili?(assuming kila mke atakuwa na watoto watatu) akawapa malazi ya uhakika na elimu bora ya kueleweka?mnajifanya kufuata dini kuoa wake wengi huku mkiishia kuwapa wake zenu mitaji ya kuuza vitumbua chapatti na maandazi vibarazani kwenye nyumba za kupanga ili kulisha watoto mnaowazalisha mwisho taifa linazidi kuwa la kipopoma.

Inabidi akili zenu zirudi normal ili mjue kwamba nguvu za kiume ni zaidi ya kusimamisha uume na aliyekudanganya wenye wake wengi hawana vimada nani?usijifiche kwenye kichaka cha dini kufikiri upo smart kuliko wengine.
 
Allah ameweka wazi

Koran 9;23. Enyi mlio amini!(waislamu) Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu ukafiri (wasio waislamu)kuliko Imani (uislam)....
Sawa! Na vilevile ikaweka wazi kwenye hizi aya surat Luqman. Nikakuuliza; unaelewaje? Unafafanuaje?


14. Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. 14


15. Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda
 
Sasa hapo wewe huelewi nini wakati kila kitu kimeshabainishwa apo
 
Pole sana. Inaonekana ulikuwepo tu kwenye hayo makanisa kama kwa mkumbo fulani, kama muumini wa dini ya kilokole, lakini hujawahi kuupata wokovu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Yaani, Yesu hajawahi kuingia ndani yako, wala wewe haujawahi kuwa ndani yake.
Mtu akiisha kuijua kweli na kumpokea Bwana ndani ya moyo hawezi kuwaza hayo unayoyawaza.
Wokovu sio dini, wala sio kuwa muumini wa dhehebu au dini fulani. Wokovu ni Kristo kuwa ndani yako na wewe kuwa ndani yake.
Nikushauri tu, utafute wokovu, mtafute mwokozi, mtafute Yesu Kristo.
Mtu akihitaji msaada zaidi juu ya kuufahamu wokovu, karibu sana inbox.
 
...Badili. Kila la Heri. Mungu ni yule yule TU. Kanuni za Kumuabudu ndio zinatofautiana...!
 
Inamaana shia hawaamini Muhammad na Allah wapo sawa

Soma
Koran 33:36. Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allah na Muhammad wanapo kata shauri katika jambo lao.
Kawaulize hao mashia unowatetea mtume wao ni yupi? Na Qur-an yao ni ipi?
 
kwamba shia hawaamini katika Allah na muhammad mtume wake!!!!
Ndio Mashia hawamuamini Muhammad wao mtume wao ni mwingine kabisaa

Wanamkubali Allan ila Muhammad hawamkubali na wanamzushia mengi tu

Ukitaka Elimu kaa chini Usome kwa wenye Elimu Sahihi

Niishie hapa
 
Unataka kusema hata kwenye Kanisa lako la miaka hiyo ya 80 nalo limebadilika?
 
Ndio Mashia hawamuamini Muhammad wao mtume wao ni mwingine kabisaa

Wanamkubali Allan ila Muhammad hawamkubali na wanamzushia mengi tu

Ukitaka Elimu kaa chini Usome kwa wenye Elimu Sahihi

Niishie hapa
Unao udhibitisho??
 
Mimi kwetu Mzee kaoa wake watatu watoto 12 tulohai mpka sasa na sote tumesoma wengine bado wanasoma vzr tu

Maisha ni mipango tu ukishazoea uzinzi ndoa hutoitaka

Tena afadhali ya Mzee wangu wapo wengine zaidi yake na watoto wanasoma private schools
 
Mimi kwetu Mzee kaoa wake watatu watoto 12 tulohai mpka sasa na sote tumesoma wengine bado wanasoma vzr tu

Maisha ni mipango tu ukishazoea uzinzi ndoa hutoitaka

Tena afadhali ya Mzee wangu wapo wengine zaidi yake na watoto wanasoma private schools
Majority Tanzania hii wangapi wana uwezo huo?na siyo kila mtu mwenye ndoa moja ni mzinzi nimemwambia mwenzako hapo juu wapo wenye wake zaidi ya mmoja and still ni wazinzi.

Usizungumzie mtu mmoja mmoja hata hao wenye mke mmoja kuna ambao nanga zinapaa watoto wanalala njaa elimu hawapewi etc maisha mabovu kama wengine tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…