Mimi ni mlevi wa kutazama vipindi vya wanyama ila huyu mnyama simpendi

Mimi ni mlevi wa kutazama vipindi vya wanyama ila huyu mnyama simpendi

Ni kweli, kuna milima mirefu kuliko hata ya duniani, kuna barabara, kuna misitu na misitu minene, kuna sehemu hakuna oxygen na kuna viumbe wanaishi, kitu kinachonivutia zaidi ni kua wanasayansi wameisoma na kuijua bahari kwa asilimia chache sanaa, hua nasisimka sana nikipata habari za baharini
Dahh, kumbe. Basi bahari imeficha vingi, na ndo maana Watafiti kuna kina hawafiki, hasa kule kwenye dark water
 
Pia vitu vya baharini ukiambiwa barabara usiweke picha ya barabara zetu hizi za lami na changarawe au misitu basi ukajua ni mamiti makubwa yenye mzizi ya kutisha la hasha vinakua vimekaa kibahari bahari,
Jisomee elimu hii adimu ya bahari uburudike, ustaajabu na kujifunza mazito.
Kajisomee zaidi usifungwe fungwe, unafahamu seamounts? nenda kajisomee kuhusu mlima Mauna Kea, misitu umekubali pia ipo? taarifa zote zipo kiganjani mwako tena mmerahisishiwa kuna akili mnemba unauliza tu kwa lugha yako unashushiwa nondo zote.
Baharini kuna miujiza mingi sana na ukiambiwa kwa akili ya kawaida waeza usiamini lakin ndo ukweli wenyewe
 
Fisi ana tamaa sana jamaa, yaan wao kuhusu msosi utawaua ila hawaezi kubali predator mwengne ale mbele yao. Kuna moja hiyo kuna kiboko alikuwa Kasizi kwenye maji kwa muda mrefu, fisi siwakajua kuwa ameshakufa ni mzoga, wakachomoka wawili wakaanza kupiga mbizi kuusogelea, kufika wanamnusanusa sindo kiboko anashtuka, akawageukia... Aweee fisi acha wapige mbizi kurudi nchi kavu huku kiboko naye anakuja katanua domo lake🤣 fisi wakigeuka wakiangalia lile domo nguvu za kuogelea zinaongezeka🤣, hadi wanafanikiwa kutoka pale mimi mbavu sina maana ni kama walikuwa wanawatukana wenzao kuwa "simlisema kafa, au mlitaka tukafe sisi?"🤣🤣
Hahaahah wewe jamaa mbona kama ni balozi wa hiari wa kiboko, maana naona kila comment unampa ushindi sasa naona fisi wamefikiwa.
 
Kwahyo mmeamua kunivua nguo, kulikuwa na haja gani ya kutaja hiyo idadi ya miguu ya hao wadudu.
Hapana. Pole kama umejisikia vibaya- sio nia au lengo la kutaja idadi ya miguu bali lengo (kwa nia njema kabisa) lilikuwa ni kuhabarishana na kupeana uzoefu kama ilivyo kawaida ya maGT hapa Jf.
 
Hapana. Pole kama umejisikia vibaya- sio nia au lengo la kutaja idadi ya miguu bali lengo (kwa nia njema kabisa) lilikuwa ni kuhabarishana na kupeana uzoefu kama ilivyo kawaida ya maGT hapa Jf.
Hakuna neno kabisa mkuu wangu tuko pamoja sana.
 
Back
Top Bottom