Mimi ni mtaalamu wa kilimo, natafuta mtu mwenye mtaji (fedha) ili tuwekeze kwenye kilimo mkoani Katavi

Mimi ni mtaalamu wa kilimo, natafuta mtu mwenye mtaji (fedha) ili tuwekeze kwenye kilimo mkoani Katavi

Hakuna mtu wa kukuamini huko kukukodisha shamba kwa makubaliano kuwa utamlipa ukishavuna na kuuza? Au shamba unalo?
Wa kukukodishia shamba wote wanataka cash mkuu ili nao waingize pesa hio kwenye kutatua shida zao zingine zinazowakabili.
 
Kukodi shamba heka moja (shamba lililokaribu na chanzo cha maji/mto) 150,000/=
Mbegu 300g 220,000/=
Kulima shamba heka 50,000/=
Kufanya palizi heka 30,000/=
Kununua water pump 320,000/=
Mbolea (samadi, na za viwandani) = 300,000/=
Madawa ya wadudu+ magonjwa 200,000/=
Kuvuna heka 50,000/=

Kununua pipe za kumwagilia (150m) = 180,000/=

Gharama ya petrol (Lita 5/siku/acre)

Roughly itagharimu 650,000/=

Hela inayobaki ni ya DHARURA +CHAKULA+ NAULI
Hapa utakuwa umelima zao gani?
Kea magesabu haya niamni kuna shida sehemu kama pesa ya dhalula na mengineyo inazidi ya uwekezaji kea asilimia 220%

But still toa nipe namba yako
 
Hapa utakuwa umelima zao gani?
Kea magesabu haya niamni kuna shida sehemu kama pesa ya dhalula na mengineyo inazidi ya uwekezaji kea asilimia 220%

But still toa nipe namba yako
Umesrma roughly 650K au ulimaanisha nini hapo?
 
Umesrma roughly 650K au ulimaanisha nini hapo?
Hiyo 650,000/= ni jumla ya Gharama za mafuta yatakayotumika kwenye mashine ya kumwagilia pamoja na services ndogo ndogo za kila mara za mashine kama vile kubadilisha oil na filter zake n.k

Maana kwa wastani water pump inatumia lita 5 mpaka 7 za petroli kwa kila siku unapo mwagilia mimea.
 
Gunia la karanga likimenywa linatoa kilo 25-30. Kwa hiyo bei wakati wa mavuno inakuwa juu; ukijumlisha Nauli hamna kitu hapo, bora mtu anunulie Dar
Hiyo bei niliyokuwekea ni ya kununulia kwa sokoni sio bei ya karanga kutoka kwa wakulima wazalishaji.
 
Habarini za mchana ndugu zangu na poleni kwa majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.

Mimi ni kijana wa kiume na Mtanzania mwenye umri wa miaka 28. Nina Elimu ya chuo kikuu katika ngazi ya shahada ya kilimo na katika hali ya ndoa mimi bado sijaoa na wala sina mtoto kwasasa.

Hivi sasa ninapatikana katika mkoa wa Katavi, Wilaya ya mlele, kata ya usevya na mtaa wa kasunzulu. Ila makazi yangu ya kudumu ni Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Ndugu zangu, nipo hapa kutafuta mtu yeyote ambaye ana mtaji (Rasilimali fedha) ili tuanzishe mradi wa kilimo biashara katika mkoa huu wa katavi maana ni miongoni mwa mikoa ambayo bado ina fursa kubwa za uwekezaji katika kilimo biashara.

Miongoni mwa fursa hizo ni kama ifuatavyo:-

1) Uwepo wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba (matumizi/mahitaji ya mbolea za viwandani katika uzalishaji yapo chini sana).

2) Gharama za kukodi/kununua mashamba zipo chini sana.

3) Uwepo wa mito na schemes za umwagiliaji (mfano, KILIDA irrigation scheme na KASHISHI irrigation scheme) unatoa fursa kubwa kwa uanzishwaji wa miradi ya kilimo cha umwagiliaji.

4) Kwa upande wa kilimo biashara bei za mazao huku ziko chini sana hivyo kutoa fursa ya kununua mazao ya huku kwa bei ndogo na kusafirisha kwenye masoko ya walaji wakubwa mikoa mingine ili kutengeneza faida maradufu.

5) Gharama za kuishi katika mkoa huu zipo chini pia.

6) Urahisi wa upatikanaji wa nguvukazi (vibarua) ukilinganisha na mikoa mingine maana asilimia kubwa ya vijana wa huku wana mapenzi (passion) na kilimo.

Hivyo basi, Jukumu kubwa la muwezeshaji litakua ni kuwekeza fedha zake katika miradi pendekezwa na kujipatia faida zitakazo zalishwa na miradi pendekezwa huku mimi nikiwekeza mtaji wangu (Rasilimali muda na ujuzi) katika usimamizi wa shughuli zote za miradi pendekezwa.

Kitendo cha kutokua na mke na mtoto kwasasa kitanipa fursa kubwa ya kuelekeza focus yangu yote katika kazi na vilevile kuwa na uwezo wa kuzunguka mikoa mbalimbali katika shughuli za uendeshaji wa miradi na biashara kwa ujumla.

Penye nia pana njia, mgaagaa na upwa hali wali mkavu na mtembea bure si sawa na mkaa bure pasipo kujishughulisha.

Nakaribisha maswali, maoni na mapendekezo yeyote kutoka kwenu wakuu.

Mtu yeyote atakaye guswa na mwenye nia ya dhati ya kuisaidia serikali katika kupanua "Wigo" wa uwezeshaji vijana katika kujiajiri namkaribisha hapa au PM kwaajili ya mazungumzo ya kina.

~Nawasilisha~ [emoji120][emoji120]
Mkuu unatafuta mwekezaji,Weka facts and figures,

Unatka uwekezaji wa kiasi gani kwa ajili ya nini na projected return ni nini na faida inagawanywaje.na kwa muda gani.Ukiweka Hesabu katika namba ni rahisi kueleka na kuvutia mtu
 
Kukodi shamba heka moja (shamba lililokaribu na chanzo cha maji/mto) 150,000/=
Mbegu 300g 220,000/=
Kulima shamba heka 50,000/=
Kufanya palizi heka 30,000/=
Kununua water pump 320,000/=
Mbolea (samadi, na za viwandani) = 300,000/=
Madawa ya wadudu+ magonjwa 200,000/=
Kuvuna heka 50,000/=

Kununua pipe za kumwagilia (150m) = 180,000/=

Gharama ya petrol (Lita 5/siku/acre)

Roughly itagharimu 650,000/=

Hela inayobaki ni ya DHARURA +CHAKULA+ NAULI
Hizi 300gm ni mbegu za zao gani? Hivi uliwahi kufanya kilimo cha umwagiliaji physically. Bado nina maswali nijibu kwanza hilo la mbegu na hilo la kulima
 
Hizi 300gm ni mbegu za zao gani? Hivi uliwahi kufanya kilimo cha umwagiliaji physically. Bado nina maswali nijibu kwanza hilo la mbegu na hilo la kulima
Mbegu za tikiti.... uzoefu ninao wa kutosha katika shughuli hizi
 
Back
Top Bottom