Mawasiliano :
kwanzakilimo73@gmail.com
Kwa anayehitaji namba za simu aje PM.
Habarini za mchana ndugu zangu na poleni kwa majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.
Mimi ni kijana wa kiume na Mtanzania mwenye umri wa miaka 28. Nina Elimu ya chuo kikuu katika ngazi ya shahada ya kilimo na katika hali ya ndoa mimi bado sijaoa na wala sina mtoto kwasasa.
Hivi sasa ninapatikana katika mkoa wa Katavi, Wilaya ya mlele, kata ya usevya na mtaa wa kasunzulu. Ila makazi yangu ya kudumu ni Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Ndugu zangu, nipo hapa kutafuta mtu yeyote ambaye ana mtaji (Rasilimali fedha) ili tuanzishe mradi wa kilimo biashara katika mkoa huu wa katavi maana ni miongoni mwa mikoa ambayo bado ina fursa kubwa za uwekezaji katika kilimo biashara.
Miongoni mwa fursa hizo ni kama ifuatavyo:-
1) Uwepo wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba (matumizi/mahitaji ya mbolea za viwandani katika uzalishaji yapo chini sana).
2) Gharama za kukodi/kununua mashamba zipo chini sana.
3) Uwepo wa mito na schemes za umwagiliaji (mfano, KILIDA irrigation scheme na KASHISHI irrigation scheme) unatoa fursa kubwa kwa uanzishwaji wa miradi ya kilimo cha umwagiliaji.
4) Kwa upande wa kilimo biashara bei za mazao huku ziko chini sana hivyo kutoa fursa ya kununua mazao ya huku kwa bei ndogo na kusafirisha kwenye masoko ya walaji wakubwa mikoa mingine ili kutengeneza faida maradufu.
5) Gharama za kuishi katika mkoa huu zipo chini pia.
6) Urahisi wa upatikanaji wa nguvukazi (vibarua) ukilinganisha na mikoa mingine maana asilimia kubwa ya vijana wa huku wana mapenzi (passion) na kilimo.
Hivyo basi, Jukumu kubwa la muwezeshaji litakua ni kuwekeza fedha zake katika miradi pendekezwa na kujipatia faida zitakazo zalishwa na miradi pendekezwa huku mimi nikiwekeza mtaji wangu (Rasilimali muda na ujuzi) katika usimamizi wa shughuli zote za miradi pendekezwa.
Kitendo cha kutokua na mke na mtoto kwasasa kitanipa fursa kubwa ya kuelekeza focus yangu yote katika kazi na vilevile kuwa na uwezo wa kuzunguka mikoa mbalimbali katika shughuli za uendeshaji wa miradi na biashara kwa ujumla.
Penye nia pana njia, mgaagaa na upwa hali wali mkavu na mtembea bure si sawa na mkaa bure pasipo kujishughulisha.
Nakaribisha maswali, maoni na mapendekezo yeyote kutoka kwenu wakuu.
Mtu yeyote atakaye guswa na mwenye nia ya dhati ya kuisaidia serikali katika kupanua "Wigo" wa uwezeshaji vijana katika kujiajiri namkaribisha hapa au PM kwaajili ya mazungumzo ya kina.
Niko tayari kufanya kazi mkoa wowote ambapo mfadhili atapendekeza.
~Nawasilisha~ [emoji120][emoji120]