Mimi ni mtaalamu wa kilimo, natafuta mtu mwenye mtaji (fedha) ili tuwekeze kwenye kilimo mkoani Katavi

Kaka hzo ni hesabu za ekari au hekta?

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Hivi unajua bei ulio iweka haina tofauti na ya Dar? Kuna shida mahali katika utoaji wako wa taarifa.
Mkuu nimekuwa interested na hii comment yako, kama hutojali unaweza nijuza ni Dar sehemu gani wanauza gunia la karanga 40000?

Na pia hizo karanga ni nyeupe au zile nyekundu? Kwa mazingira ambayo yupo mdau nahisi yeye anaongelea karanga nyeupe, je hizo unazoongelea wewe ni zipi?
 
Anaposema gunia la karanga hamaanish zilizo pukuchuliwa.

Gunia la karanga za maganda hutoa kilo 20 hadi 30 kama zimekomaa vizuri. Ukichukulia kiwango cha chini cha kilo 20 inamaana utakuwa umenunua kila kg elf 2 hapo hujaweka gharama za kubungua na Nauli ya kufukisha unapopeleka. Ukijumlisha vyote hivyo utagundua bei hiyo iko juu mno.

Kea halo hiyo bora uende Mpwapwa ambapo unapata kilo ya zilizokobolewa kwa 1200-1500?
 
Sawa mkuu nashkuru Kwa maelekezo yako, hasa hapo kwenye kwenda mpwapwa ni kweli Kwa bei hiyo ni nzuri Kwa karanga ambazo zishamenywa

ila nadhani bado hujajibu swali langu la sehemu gani Dar wanauza Hilo Hilo gunia ambalo bado halijabanguliwa Kwa 40000, kuna kitu nataka kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi, na je hilo gunia ni karanga nyeupe au nyekundu
 
Usevya haipo wilaya ya mlele, ipo wilaya ya mpimbwe.
Alafu pia tofautisha Kati ya hekari(Hectare) na ekari(acre). Unatuchanganya sana
 
Kaka maelezo yako yanavutia lakini hujazungumzia sana kuhusu soko la hayo mazao ukishalima,wapi unategemea kwenda kuuuza?,gharama zake kama utabidi usafirishe usafiri ukoje mpaka ufike sokoni pamoja na uhakika wa uuzaji hayo mazao.unaweza kufafanua kidogo ndungu yangu.
 
Kila la kheri, ngoja waje kukupa muongozo...
 
Mtoa maada katoa andiko zuri ila limekosa nyama kabisa.Kwanini ulime horticultural crops mkoani Katavi, ambapo hayo mazao ni very perishable kama tikiti,nyanya, tango etc...?Je,target ya soko lako ni wapi?Maana kusafirisha hizo horticultural crops kutoka katavi mpk Dar ambako kuna soko la uhakika lazima mzigo uoze au kuharibika njiani.

USHAURI:

1.Kama lengo ni ulime horticultural crops (mazao ya mbogamboga) katavi siyo sehemu sahihi kwa nature hiyo ya mazao, ndio maana hata wenyeji wanalima most cereal crops like mahindi,maharage,Mpunga,karanga etc...

2.Ni vema ufanye hicho kilimo mkoa wa Pwani au Morogoro ambako ni jirani na soko,kwa maana target kubwa ya soko la horticultural crops ni masoko ya Dsm.

3.Pia ni vema ujue crop calendar vizuri na ufahamu pia ni msimu gani supply ya horticultural crops ni ndogo na demand ni kubwa,huo ndio msimu wa kupiga pesa nyingi kwenye horticultural crops,Market target ni muhimu sana na ndio uhai wa project yako.

4.Tumia drip irrigation & green houses for the better results,nje ya hapo unatafuta kesi ya kupoteza mitaji ya watu.

5.Andaa business plan nzuri yenye input,Agronomical activities,cost analysis and profit.Japo profit ya kilimo siyo guaranteed,na hapo ndio utaonyesha ukomavu wako ndugu Mwanasuaso kuwa unaweza kupata excepted profit kwa facts gani?
 
Drip and green houses farming ni investment inayohitaji mtaji wa maana mkuu.
 
Uaminifu uko kiasi gani? Kuna mwanasheria tunaweza kuandaa mkataba?
Dawa ni kufungua kampuni na kumgawia share za kampuni au kumwajiri kutokana na utaalam/mchango wake then ajiri Meneja, atafanya kazi tuu maana kazi zaidi na bidii zaidi atakayoweka atafaidika zaidi na hasara mtagawana sawasawa, pesa hataiona mpaka siku ya mshahara au gawio
 
Huu Uzi uliishaje? Je, ulifanikiwa?
 
Shida ya vijana ni uaminifu. Kuna watu wana hela huku maofisini wangefanya partinership
 
wazo lako zuri sana tunatofautiana kwenye kuwekeza pesa mm na vifaa vya kilimo kuanzia Tractrors vifaa vya kumwagilizia kupanda na kuvuna kama Drons kwajili ya kumwagilizia dawa mifumo ya umwagilizia mbegu mbolea na madawa kama uko tayari tuanze kazi pesa sina
 
Hivyo vyote ulivyovitaja hapo umavyo ola pesa huna. Hapo sijakuelewa kabisa
 
Tutafutane nipo kijiji cha Ikuba naweza fanya kitu kikakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…