Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Bashe kafanya Retaliation ambapo kimkakati hakutumia busara. Kwa ujumla amekurupuka kama kijana aliyekuwa kwenye balehe.

Baada ya Malawi kufanya alichofanya. Bashe kwa kushirikiana na wizara za viwanda, mambo ya nje na wanadiplomasia wangekaa chini na kufanya tafakuri ya kina na kuja na mkakati madhubuti ambao ungeinufaisha zaidi Tanzania bila kuleta athari au mgogoro na jirani yetu.

Njia aliyotumia ya jino kwa jino haina afya kwetu Wala kwao sababu tunategemeana. Sina uhakika ila nahisi ametumia mihemuko zaidi kuliko weledi. Bashe ni mmojawapo wa mawaziri ambao wapo smart ila kwa hilo la Malawi amepuyanga pakubwa.
 
Hayo kasema yeye ila kwa umuhimu wa mteja wetu malawi kwa bandari ni ngumu kutekelezeka maana watatafuta arkernative root in a long run maana wataona sisi siyo reliable partner kibiashara
Umegonga kichwa cha msumari katika thread hii. Malawi hawatakaa waione Tanzania kuwa nchi ya kuaminika tena katika suala la kutimia bandari ya Dar es Salaam. Huko Bashe hakupasa kugusia kabisa.

Ni sawa na jirani yako, ambae anapita mbele ya nyumba yako kwenda sokoni. Sasa eti kwa sababu amekataa kununua vitumbua vya mkeo ameagiza mkewe apike vyake unamwambia kama hutaki kununua vitumbua vya mke wangu unapoenda sokoni kuuza vitumbua vyako usipite mbele ya nyumba yangu. Kama hiyo sio akili ya kitoto si ya kiuendawazimu?
 
KUna watu humu kwa akili waliyonawo kuelewa hili hadi mwisho wa dunia uje, kwa sababu hawawezi kuona mbali zaidi ya mwisho wa pua zao.

Bashe kavunja sana uaminifu wa Tanzania kwa Malawi, na si Malawi tu, kwa nchi zote zinazotegemea bandari zetu. Kutumia bandari kama fimbo ni jambo la kijinga ambalo Tanzania inaweza kutumia. Kumbuka kwamba, japo Zambia waliwapinga Makaburu, bado walitumia bandari yao. Kaburu alipoanza kiutumia kama fimbo ndicho kilichozaa TAZARA.

Siku Malawi wakipata pesa basi kutakuwa na mradi wa reli kwenda Msumbiji ili waachane na bandari ya Tanzania. Malawi hawatakaa wasahau ujinga huu wa Bashe.
 
F
Familia ya kambale mama shalubu, mtoto shalubu,mjukuu shalubu.
 
Na kwa sababu ya yote haya kuwaambia msipitishe vitu vyenu kwenye bandari yetu mkitaka kuvipeleka nje unaona ni sahihi? Tumetangaza vita na Malawi?

Hebu niambie unaona ni jambo la akili kumwambia Malawi umekataa kununua mchele wetu basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe Tanzania?
 
Kuna watu wagumu sana kusoma na kuelewa, na wewe ni mmojawapo. Who said it is not a perfect move ku-recoprocate imports za mazao ya Malawi kwa ajili ya kuuza Tanzania, kama wao wanazuia exports za mchele wa Tanzania kwa ajili ya kuuza Malawi?
Itakuwa nyie ndo wapinga maendeleo ( chadema)

Iko hivi ....Kila mtu anaangalia silaha ya kumdhibiti mpinzani.....hakuna anayekucgagulia silaha

Bashe yupo sahihi 100% ......ni mzalendo sana

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Akili ndogo!!
"Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania"

Unamkomoa nani? Kwani hiyo mbolea ikitoka Tanzania, wanapewa bure kwa kuwanyima wakulima wa Tanzania? Na kama Malawi wameinunua toka nje na kuipitisha Tanzania, hawalipii kutumia bandari yetu na huduma za malori ya mizigo yanayoipeleka Malawi?

Kweli akili ndogo, na tunajua nani mwenye akili ndogo hapa
 
Itakuwa nyie ndo wapinga maendeleo ( chadema)

Iko hivi ....Kila mtu anaangalia silaha ya kumdhibiti mpinzani.....hakuna anayekucgagulia silaha

Bashe yupo sahihi 100% ......ni mzalendo sana

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Ndio maana kwa namna ya kufikiri kwenu nyie CCM hadi leo hatuendelei japo tuna rasilimali kibao! Halafu bado mnauliza kwa nini Tanzania ni masikini duniani, Least Developed Country, LDC, wakati jibu mnalo - ni kwa sababu CCM ndio chama tawala!
 
Bashe kazingua inabidi asichukue hatua Kali zaidi ya waliochukua wao
 
Ndio maana kwa namna ya kufikiri kwenu nyie CCM hadi leo hatuendelei japo tuna rasilimali kibao! Halafu bado mnauliza kwa nini Tanzania ni masikini duniani, Least Developed Country, LDC, wakati jibu mnalo - ni kwa sababu CCM ndio chama tawala!
Watu kama nyie mna mchango mdg Kwa taifa .....hamna faida Bora mngekuwa kasongo. ....tuwale kitmoto

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Bashe kazingua inabidi asichukue hatua Kali zaidi ya waliochukua wao
Kwa kifupi, hajawa fair. Tunaelewa kufanya ushindani wa kibiashara kwa kuchukua hatua kama zao, lakini kwa hapa he is bullying Malawi. In fact, Malawi wanaweza hata kutushitaki WTO.
 
Yupo sawa kabisa,
Nakazia hapa
 
Kwamba unaju kulio wazir wa kilimo

Kenya walifanya uhuni huu tukawafanyia reciplocal sahivi hawa malawi wanajidai wajuaji

Malawi wana bifu na sisi toka zamani tu
Hivi wewe unafikiri mtu akiwa waziri basi ana akili kuliko wengine? Yaani wewe unaamini Raisi Samia ana akili kuliko Watanzania wote kwa sababu yeye ndio raisi wa nchi? Na Dr. Tulia ana akili kuliko wabunge wote?

Sasa hapo unajionyesha una akili kiasi gani
 
Mkuu vita haichagui silaha, ikibidi tumia silaha zote ulizonazo ili ushinde vita.
Malawi wanafaidika na mengi ya Tanzania waache unyanyapaa dhidi yetu vinginevyo tutakabiliana nao.
 
Mkuu vita haichagui silaha, ikibidi tumia silaha zote ulizonazo ili ushinde vita.
Malawi wanafaidika na mengi ya Tanzania waache unyanyapaa dhidi yetu vinginevyo tutakabiliana nao.
Sasa kwa mentality kama hii hatuwezi kujadili jambo kama hili tukaelewana, kwa sababu hiyo ni lojiki ya mtu ambae hajaenda shule, anaetafuta solution ya haraka iliyokaribu nae. Mtu aliesoma akaelimika, anaejua kuwa katika biashara kuna changamoto kama hizi, haweza kukubaliana na alichofanya Bashe. Bashe anaweza kuwa kasoma kwa kiasi, lakini ni wazi hajaelimika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…