Wamalawi wamejazana kila kichochoro na hawabugudhiwi na Uhamiaji.Sisi ndo tunafaidika na Malawi kwasababu Malawi ni wateja wa bandari zetu
Nimekumbuka tulipokuwa watoto tukicheza soka mtaani. Kulikuwa na mtoto mmoja wa kishua ambaye alikuwa ana mipira mingi mizuri.KUna watu humu kwa akili waliyonawo kuelewa hili hadi mwisho wa dunia uje, kwa sababu hawawezi kuona mbali zaidi ya mwisho wa pua zao.
Bashe kavunja sana uaminifu wa Tanzania kwa Malawi, na si Malawi tu, kwa nchi zote zinazotegemea bandari zetu. Kutumia bandari kama fimbo ni jambo la kijinga ambalo Tanzania inaweza kutumia. Kumbuka kwamba, japo Zambia waliwapinga Makaburu, bado walitumia bandari yao. Kaburu alipoanza kiutumia kama fimbo ndicho kilichozaa TAZARA.
Siku Malawi wakipata pesa basi kutakuwa na mradi wa reli kwenda Msumbiji ili waachane na bandari ya Tanzania. Malawi hawatakaa wasahau ujinga huu wa Bashe.
CrapKuna watu wana uwezo wa kufikiri na tofauti na wanaosema ni pinga pinga tu hapa. Usiwe mtu wa kusukumwa tu katika maisha yako - sycophant. Ukiambiwa tunauza bandari sawaaa! Tunagawa maliasili - sawaaa! Tunapunguza kikokotoo - sawaaa! Hatubadili utaratibu wa uchaguzi - sawaaa! Tunaleta kodi za miamala - sawaaa! Tunanunua umeme toka Ethiopia hauna losses kama wa kwetu unaotoka mbali kusini - sawaaa! Tunanunua drealiner japo hatuna business plan ya Air Tanzania - sawaa! Mkurugenzi Tanesco amekufa kwa aksident wakikwepa baiskeli saa nane usiku - sawaaa! Wewe ni mtu kweli, au msukule wa Kisukuma?
Na watanzania waliojazana Malawi pia wapoWamalawi wamejazana kila kichochoro na hawabugudhiwi na Uhamiaji.
Wanaishi kama wako kwao Chitipa.
Tumeamua kuwachukulia kama ndugu zetu.
Waache kidomodomo.
Baada ya uzushi wenu kuwa anaumwa saaana kubuma, mmekuja na ujinga mwingine Sasa. Nyumbu wengi mmekimbilia tu Uzi bila kuelewa lolote kwa undani. Hii minyumbu hii mipumbavu sana, natamani JPM angelikwepo.....angekuwa ameshavifutilia mbali hivi vipumbavu viovu.Bashe ni mpuuzi sana aisee.
Sikutegemea hayo yatoke kwake.
You really think Malawi will change their policy position because of Bashe's stance? If that happens nidaiCrap
Hii ni trade war and the one who blinks…. Loses it
Bashe has widen the scope na hapo ndipo ushindi ulipo
Hii si mara ya kwanza
Warudishwe nyumbani kisha tuone nani atafaidika na nani ataathrika.Na watanzania waliojazana Malawi pia wapo
Mhm iweje wawe mashoga kwenda kinyume na tamko lake?Wanaopinga tamko la Waziri Bashe wote ni mashoga
And you think they won’t?You really think Malawi will change their policy position because of Bashe's stance? If that happens nidai
Sisi ndo tutaathirika kwasababu tutapoteza soko la bidhaa zetu za viwandani, bandari pamoja na malori yetuWarudishwe nyumbani kisha tuone nani atafaidika na nani ataathrika.
Muda kuchekeana umeisha, weka niweke mpaka tuelewane.
pengine kuna nafuu fulani tanzania tumewapa malawi bandarini, ila wao hawatambui mchango wetu.Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.
Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.
Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.
Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi
Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,
2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.
3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.
Sasa najiuliza
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?
- Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
- Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?
Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kuitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?
Kwanza haya matamshi ya Bashe sio mambo ya wizara yake; wanaohusika ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Mambo ya Nje, sasa kimbelembele cha nini, kumshawishi Raisi Samia kwamba yeye ni tough guy?
Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.
If they didn't change their policy, who cares?? Bashe abane hapo hapo mpaka waje mezani. Moja ya mambo ambayo Nyerere alikosea ni hili la ujamaa na kuwatia upole wabongo, uwa hata wakionewa wanacheka cheka tu hawajui kua kuna kipindi lazima wawe ngangari . Hongera sana Waziri Bashe hivi ndio inatakiwa kufanywa ili tuheshimiane huko mbele.You really think Malawi will change their policy position because of Bashe's stance? If that happens nidai
Akili kama ya Bashe.Vita ya kiuchumi hiyo ndg yangu...
Unatakiw uwe smart kupigana nayo.. adui mnyime uhuru...
Bashe pigilia hapo hapo...
Ipo,lakini ni katika kuwavutia watumie bandari yetu. Kumbuk sio lazima watumie bandari yetu. Malawi wanahitaji mkakati mdogo sana kujitoa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Wanaweza hata kuamua mradi wa kimkakati wa kujenga barabara kuu kutoka Blantyre hadi Beira Mozambique, ambapo ni karibu sana ukilinganisha na kuja Dar. Wanasema tatizo ni rebels eneo hili. Wanaweza hata kuwa na joint military operation na Mozambique ili kuwasafisha rebels eneo hili.pengine kuna nafuu fulani tanzania tumewapa malawi bandarini, ila wao hawatambui mchango wetu.
Ndio nasema, ni watu wasioona mbali ndio wana mawazo kama hayo, ya ki-Trump. Kwa nini uwazuie katika mikakati yao ya kujitegemea kwa chakula? Mbona tunamshangilia Traole anaposema anataka Burkina Faso ijitegemee kwa chakula, na tunalaani Malawi wakichukua hatua hizo na kuwanyima access ya bandari yetu ili waendelee kututegemea kwa chakula? Sisi ni wanafiki sana basi. Traole safi sana, Malawi hapana, na tunaimba nyimbo za kujitegemea kwa chakula, eeeh!Binafsi Mimi naona Bashe Yuko sawa
Haiwezekani Malawi anufaike na rasimali zetu kama bandari, miundo mbinu na soko halafu sisi atunyime soko la bidhaa na njia za kusafirisha bidhaa za TANZANIA kwenda kusaini mwa Africa
Huyo tunakufa nae kila mtu abakinna chake