Mimi ni mwajiriwa mpya, ninahitaji mkopo

Jifunafu

Senior Member
Joined
May 25, 2020
Posts
182
Reaction score
693
Ndugu wanajamvi, natumaini mu wazima katika harakati za hapa na pale za kusaka mkate.

MIMI ni muajiriwa mpya kada ya ualimu msingi. Naombeni kusaidiwa abc kuhusu ni vipi nitapata MKOPO wa kifedha na ni wapi wanatoa kwa riba nafuu. Pia ni nyaraka zipi zinaitajika kupata MKOPO huo, maana sijapata barua ya kuthibitishwa kazini.

Asanteni na pia majibu yenu ni muhimu.
 
Jaribu NMB.

Hawa naona wanatoa mikopo kwa Watumishi wa serikali hata wale ambao bado hawajathibitishwa kazini.

Muhimu uwe na barua ya uteuzi ( letter of appointment ), kitambulisho cha kazi ( kama huna inabidi uende kwa Afisa Utumishi akuandikie barua ya utambulisho ) pamoja na salary slip zako za miezi mitatu nyuma.

ONYO:

Epuka kukopa kwenye vitaasisi. Narudia KOPA BANK tu.
 
Inawezekana mtumishi wa serikali akalipwa miezi mitatu bila kuthibitishwa kazini?
 
Nakupa ushauri

Umeajiriwa una muda gani? Angalia Saccos yenye sifa nzuri katika eneo ulilopo, Kisha jiunge huko (hakikisha ni Saccos nzuri yenye sifa zote za kifedha) riba zao huwa ni nafuu sana na hutojutia.

Banks nyingi bado Wana riba kubwa unaweza kopa mil.5 na ukalipa milion 8/9 huko.
 
Zipo Saccos nzuri na nyingine za kiboya tu.

Pili , Saccos siyo taasisi ambazo unaweza kuamka tu ukaenda kuchukua mkopo.

I'll ukopesheke SACCOS inabidi kwanza ujiunge uwe Mwanachama.

Halafu uweke akiba, then kupitia hiyo akiba ndio utakopesheka pesa Mara tatu ya hiyo akiba yako.

Vile vile, mikopo ya SACCOS inahitaji uwe na mdhamini ( Mwanachama mwenzio wa SACCOS ) tena Saccos nyingi huwa zinahitaji uwe na Mali isiyohamishika.

Kwahiyo, unaweza kuona kukopa Saccos siyo kitu cha kuamka asubuhi tu na kukopa.
 
Ushauri huu ni mbaya mleta uzi usijaribu
 
Mkuu unakopa iliiweje. Ishi kulingana na kipato chako. Jikaze ufanye savings, uwe na subra. Usitumie pesa ambayo hujai-earn
Mikopo siyo mibaya ila fuata kanuni:

1. Usikope kwenye vitaasisi vyenye riba ya zaidi ya asilimia 2 kwa mwezi.

2. Usikope mkopo wa muda mrefu sana. Kama unahitaji mkopo wa muda mrefu sana, usizidishe miaka mine (4).

3. Usikope pesa kama huna uhakika wa kitu unachoenda kufanya.

4. Usikope kununua liabilities ( Vitu vya ndani, pikipiki, gari, radio, kulipa madeni mengine )

5. Linda sana Check No. Yako. epuka sana. Kutaoa Access ya Check No yako kukatwa katwa pesa na vitaasisi uchwara.
 
Asipo fuata huu ushauri imekula kwake..

#MaendeleoHayanaChama
 
Asipo fuata huu ushauri imekula kwake..

#MaendeleoHayanaChama
Walimu wanna matatizo sana. Yaani sijui wametupiwa jini, hata sielewi.

Juzi hapa nilikuwa na mwalimu fulani, amekopa 8.5M NMB kwenda kununua gari.

Gari lenyewe hajanunua na pesa sijui kapeleka wapi. Mwenyewe anadai ana biashara, lakini muda wote kafulia.

Juzi tu hapa, nimemkuta tena anataka kukopa CRDB kwa kile kiasi kilichobaki.

Kumbuka ,huyu mwalimu hata kuthibitishwa kazini bado, na hata Bodi ya Mikopo hawajaanza kumkata.

Ina maana kwa kiasi cha pesa anachpata sasa hivi, akikikopea CRDB na Loan Board wakianza kumkata atakiwa hapati mshahara πŸ˜€

Na kama atapata, basi itakuwa labdaTsh 50,000
 
Utakuwa uliwahi kupitia same experience sio kwa kudadavua hukoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…