Walimu wanna matatizo sana. Yaani sijui wametupiwa jini, hata sielewi.
Juzi hapa nilikuwa na mwalimu fulani, amekopa 8.5M NMB kwenda kununua gari.
Gari lenyewe hajanunua na pesa sijui kapeleka wapi. Mwenyewe anadai ana biashara, lakini muda wote kafulia.
Juzi tu hapa, nimemkuta tena anataka kukopa CRDB kwa kile kiasi kilichobaki.
Kumbuka ,huyu mwalimu hata kuthibitishwa kazini bado, na hata Bodi ya Mikopo hawajaanza kumkata.
Ina maana kwa kiasi cha pesa anachpata sasa hivi, akikikopea CRDB na Loan Board wakianza kumkata atakiwa hapati mshahara [emoji3]
Na kama atapata, basi itakuwa labdaTsh 50,000