Mimi ni mwajiriwa mpya, ninahitaji mkopo

Mimi ni mwajiriwa mpya, ninahitaji mkopo

Ndugu wanajamvi, natumaini mu wazima katika harakati za hapa na pale za kusaka mkate.

MIMI ni muajiriwa mpya kada ya ualimu msingi. Naombeni kusaidiwa abc kuhusu ni vipi nitapata MKOPO wa kifedha na ni wapi wanatoa kwa riba nafuu. Pia ni nyaraka zipi zinaitajika kupata MKOPO huo, maana sijapata barua ya kuthibitishwa kazini.

Asanteni na pia majibu yenu ni muhimu.
Kaka ulifanikiwa hii ishu? Mwenyewe ni Kama wewe icpokuwa nilikosa ujasiri wa kuanza mchakato sababu bado sijamaliza mwaka, vipi Naweza nikapata mkuu?
 
Jaribu NMB.

Hawa naona wanatoa mikopo kwa Watumishi wa serikali hata wale ambao bado hawajathibitishwa kazini.

Muhimu uwe na barua ya uteuzi ( letter of appointment ), kitambulisho cha kazi ( kama huna inabidi uende kwa Afisa Utumishi akuandikie barua ya utambulisho ) pamoja na salary slip zako za miezi mitatu nyuma.

ONYO:

Epuka kukopa kwenye vitaasisi. Narudia KOPA BANK tu.
Ok boss
 
Mwalimu Jifunafu nipe taarifa Mwalimu mwenzio nataka niingie bank, VP ulifanikiwa
 
Mikopo siyo mibaya ila fuata kanuni:

1. Usikope kwenye vitaasisi vyenye riba ya zaidi ya asilimia 2 kwa mwezi.

2. Usikope mkopo wa muda mrefu sana. Kama unahitaji mkopo wa muda mrefu sana, usizidishe miaka mine (4).

3. Usikope pesa kama huna uhakika wa kitu unachoenda kufanya.

4. Usikope kununua liabilities ( Vitu vya ndani, pikipiki, gari, radio, kulipa madeni mengine )

5. Linda sana Check No. Yako. epuka sana. Kutaoa Access ya Check No yako kukatwa katwa pesa na vitaasisi uchwara.
Ushauri mzuri huu.
 
Tulia soma fursa za eneo kwanza naamini mpaka ukipata uthibitishe tayari utakuwa ushajiweka sawa kimtazamo na fursa
 
  • Thanks
Reactions: Yhy
Nyongeza tu;

1) Usikope kuanzisha biashara mpya, utajuta. Najua hamasa ya kiu ya mafanikio uliyonayo na hali ngumu kutokana na mshahara mdogo usiolingana na mahitaji, ila narudia tena, tafadhali sana usikope ili kuanzisha biashara mpya. Utanikumbuka.

2) Kwakuwa huna barua ya kuthibitishwa, kuna jamaa flani wa taasisi (siyo bank), herufi ya kwanza ni B na herufi ya mwisho ni T, tafadhali sana usije shawishika kukopa huko. Utalia machozi ya damu kwa riba zao.

3) Kopa tu endapo ni shida ya kutatua kifo cha mtu au unataka kumwokoa mtu asifungwe.

4) Endapo utalazimika sana kukopa kwa hao jamaa maana wana ushawishi mkubwa na wanapenda sana walimu, basi chukua mkopo wa muda mfupi sana kutatua hiyo shida, let's say mkopo usiozidi miezi mitatu tu.

5) Utanikumbuka. Narudia tena, utanikumbuka.
 
  • Thanks
Reactions: Yhy
Jaribu NMB.

Hawa naona wanatoa mikopo kwa Watumishi wa serikali hata wale ambao bado hawajathibitishwa kazini.

Muhimu uwe na barua ya uteuzi ( letter of appointment ), kitambulisho cha kazi ( kama huna inabidi uende kwa Afisa Utumishi akuandikie barua ya utambulisho ) pamoja na salary slip zako za miezi mitatu nyuma.

ONYO:

Epuka kukopa kwenye vitaasisi. Narudia KOPA BANK tu.
1. Hongera kupata ajira
2. acha njaa, mpaka upate barua
 
Ndugu wanajamvi, natumaini mu wazima katika harakati za hapa na pale za kusaka mkate.

MIMI ni muajiriwa mpya kada ya ualimu msingi. Naombeni kusaidiwa abc kuhusu ni vipi nitapata MKOPO wa kifedha na ni wapi wanatoa kwa riba nafuu. Pia ni nyaraka zipi zinaitajika kupata MKOPO huo, maana sijapata barua ya kuthibitishwa kazini.

Asanteni na pia majibu yenu ni muhimu.
Kakope kote! Ila ukijiroga tu kuingia kwenye 18 za Bayport, Platinum credit, Finca, Faidika, au taasisi yoyote ile ya kifedha! Badala ya benki kama crdb, nmb, nbc, tpb, nk basi ujiandae kuishi kama shetani.
 
Wewe jamaa unaweza kubishqna na picha kabisa.

Sasa nidanganye, Kuna mashindano ya kudanganya humu watu wanapwa pesa au ???

In short, jamaa mimi ndio nimemtengezea Account ya salary slip portal na kumprintia kwasababu alifikia kwangu wakati anafuatilia huo mkopo kwasababu wakati huo shule zilikuwa zimefungwa.

Slip yake hiyo Happ [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

View attachment 2118471
Mkuu mbona naona kama Mshahara kiduchu?
Huyo ni Mwl wa Level ipi?
 
Walimu wanna matatizo sana. Yaani sijui wametupiwa jini, hata sielewi.

Juzi hapa nilikuwa na mwalimu fulani, amekopa 8.5M NMB kwenda kununua gari.

Gari lenyewe hajanunua na pesa sijui kapeleka wapi. Mwenyewe anadai ana biashara, lakini muda wote kafulia.

Juzi tu hapa, nimemkuta tena anataka kukopa CRDB kwa kile kiasi kilichobaki.

Kumbuka ,huyu mwalimu hata kuthibitishwa kazini bado, na hata Bodi ya Mikopo hawajaanza kumkata.

Ina maana kwa kiasi cha pesa anachpata sasa hivi, akikikopea CRDB na Loan Board wakianza kumkata atakiwa hapati mshahara [emoji3]

Na kama atapata, basi itakuwa labdaTsh 50,000
Dah!
Kuna watu huwa hawajionei huruma kabisa.
Huyu itakuwa ni wale watu akiona tu hela mate yanamtoka hatakama hakuwa na ulazima wa kukopa atakopa ilimradi tu uwezeiano wa kukopesheka upo.
Mtiti unakuja hela zikiisha halafu bado anatumikia madeni anavyotia huruma sasa.
Halafu hawakomagi atarudia tu.
Mungu niepushie
 
Walimu wanna matatizo sana. Yaani sijui wametupiwa jini, hata sielewi.

Juzi hapa nilikuwa na mwalimu fulani, amekopa 8.5M NMB kwenda kununua gari.

Gari lenyewe hajanunua na pesa sijui kapeleka wapi. Mwenyewe anadai ana biashara, lakini muda wote kafulia.

Juzi tu hapa, nimemkuta tena anataka kukopa CRDB kwa kile kiasi kilichobaki.

Kumbuka ,huyu mwalimu hata kuthibitishwa kazini bado, na hata Bodi ya Mikopo hawajaanza kumkata.

Ina maana kwa kiasi cha pesa anachpata sasa hivi, akikikopea CRDB na Loan Board wakianza kumkata atakiwa hapati mshahara [emoji3]

Na kama atapata, basi itakuwa labdaTsh 50,000
Hahaha ila sheria hawez kattwa ziaid ya robo tatu ya mshahara wake akifika hapo Wana goma Wana Sema hakatiki labda akope kwa watu wa kulipa kesh ila kwa kutumia check no haita wezekana
 
Hahaha ila sheria hawez kattwa ziaid ya robo tatu ya mshahara wake akifika hapo Wana goma Wana Sema hakatiki labda akope kwa watu wa kulipa kesh ila kwa kutumia check no haita wezekana
Wewe ni mtumishi?
 
Hujawahi miliki 1m au Hata kumiliki Asset yenye thamani ya 1m hujawahi

unataka kukopa 3m hiyo pesa utailipa lipaje? siwezi shauri mtu akope wala

shauri mtu namna ya kutumia mkopo,MO anakopa ila anakopa pesa ambayo

hata leo waseme tupe hela yetu anaweza rudisha pesa ya watu,Usikope kwa

kuangalia unataka kufanyia nini hiyo hela, kopa kwa kujiuliza Je! nina uwezo wa

kurudisha hii pesa ya watu incase things goes viceversa?! ukikopa kwa kutegemea

unachotaka kukifanyia baada ya kukopa ndio kirudshe mkopo Umepotea/umeumia.

Mikopo ni ya Matajiri TU wenye Stable income not otherwise, Tuna ambiana ukweli hapa.
Amen , huwa nakopa pale tu najua kuna deal flani hela imechelewa ila imo inakuja.
Vingine najifiaga na tai shingoni.
 
Mkuu mbona umeongea point mbofumbofu sana leo? Huwa nakuaminia sana lkn leo umeniangusha. Kukopa kupo, hata akina mo wanakopa. Cha msingi mshauli mtu namna ya kuutumia mkopo.
Sio kila mtu ana mali ambazo anaweza kuuza akapata hela nzuri.
Matajiri wote duniani wana mikopo.

Sisi matajiri tuna msemo wetu wa mikopo" use other people's money to create your wealth'

Hizo za mikopo ndio pesa za wengine wanahifadhi benki.Benki wamekuwa watu wa kati tu yaani middlemen.

Ukikopa ukafanya anasa na kununu la liabilities imekula kwako unajiweka kwenye utumwa.

Ukikopa ukaweka kwenye investment utakuja jishukuru baadae.

Mwaka jana nilikopa hela ndefu nikaweka kwenye investment fulani na mwezi huu naanza pata returns zangu. Ni lifetime returns unless otherwise.

Kopa wekeza somewhere utajirike, au kopa kat.om.bee.eee ndio utajiua kuwa hujui.[emoji2][emoji3577]
 
Ndugu wanajamvi, natumaini mu wazima katika harakati za hapa na pale za kusaka mkate.

MIMI ni muajiriwa mpya kada ya ualimu msingi. Naombeni kusaidiwa abc kuhusu ni vipi nitapata MKOPO wa kifedha na ni wapi wanatoa kwa riba nafuu. Pia ni nyaraka zipi zinaitajika kupata MKOPO huo, maana sijapata barua ya kuthibitishwa kazini.

Asanteni na pia majibu yenu ni muhimu.
Ukishapata barua ya kuthibitishwa nenda NMB watakuelekeza.

#YNWA
 
Matajiri wote duniani wana mikopo.

Sisi matajiri tuna msemo wetu wa mikopo" use other people's money to create your wealth'

Hizo za mikopo ndio pesa za wengine wanahifadhi benki.Benki wamekuwa watu wa kati tu yaani middlemen.

Ukikopa ukafanya anasa na kununu la liabilities imekula kwako unajiweka kwenye utumwa.

Ukikopa ukaweka kwenye investment utakuja jishukuru baadae.

Mwaka jana nilikopa hela ndefu nikaweka kwenye investment fulani na mwezi huu naanza pata returns zangu. Ni lifetime returns unless otherwise.

Kopa wekeza somewhere utajirike, au kopa kat.om.bee.eee ndio utajiua kuwa hujui.[emoji2][emoji3577]
Sentensi ya mwisho inaonyesha wazi wewe ni kula kulala kwa shemeji yako tena graduate usiyekuwa na ajira ya kueleweka mzee wa vizinga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom