Mimi ni mwajiriwa mpya, ninahitaji mkopo

Walimu wana QI ndogo sana...wananuka mikopo..bado chama chao kina walamba hela kila siku.

#MaendeleoHayanaChama
 
Igwee igwee igwee hapo umemaliza mkuu
 
Nilikopa nikaweka hela kwenye mchanga/ujenzi ukaishia boma tu tofauti na matarajio. Huku nakatwa mkopo huku kodi ya nyumba inaendelea huku magufuli kaongeza makato bodi ya mkopo. Take home ikabaki laki 1.5 nina mke na mtoto mmoja. Unaweza kuongea peke yako barabarani
 
Sababu ya kukopa? kama unaona kbs uwezo wakupotezea hiyo sababu upo

potezea,ila kama unakopa ili upate pesa zaidi ya hiyo "go ahead" lakini tofauti

na hapo fanya uwezalo usikope,mara 100 uuze vitu/mali zako upate kiasi ukitakacho

Kama huna mali ya kuuza ukapata kiasi cha pesa unayoitaka kukopa,asee Usikope maana

ni dhahiri kbsa unakopa pesa iliyo juu ya uwezo wako,itakutesa sana kwenye kuirudisha,utanyooka!
 
Walimu wana QI ndogo sana...wananuka mikopo..bado chama chao kina walamba hela kila siku.

#MaendeleoHayanaChama
Lakini kuhusu kukopa mbona wafanyakazi wote wa serikali wanakopa ?, hapa nawaona manurse ,bibi afya,kilimo na mifugo ,watendaji wa kata na mitaa,madktari,na wengne wote naona wote wanakopa .Sasa nashangaa unavyosema walimu wana IQ ndogo kisa wanakopa.
 
Kuna jamaa yangu mmoja, ile taasisi ya mkopo ya mke wa Mkapa- siikumbuki jina walimfanya hamna yani
 
Walimu wana QI ndogo sana...wananuka mikopo..bado chama chao kina walamba hela kila siku.

#MaendeleoHayanaChama
Kuhusu kuwa na IQ ndogo Mimi sijui.

Ila kwenye makato ya vyama vya wafanyakazi wote hawachekani.

Vyama vyote vinakata.
 
Halafu huyo huyo ndio amfundishe mwanao apate ufahamu.

Shule za umma ni changamoto
 
Mkuu mbona umeongea point mbofumbofu sana leo? Huwa nakuaminia sana lkn leo umeniangusha. Kukopa kupo, hata akina mo wanakopa. Cha msingi mshauli mtu namna ya kuutumia mkopo.
Sio kila mtu ana mali ambazo anaweza kuuza akapata hela nzuri.
 
Uongo kunogesha genge, NMB hakuna mkopo mkubwa hivo kama hujathibitishwa kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…