Mimi ni mwajiriwa mpya, ninahitaji mkopo

Kaka ulifanikiwa hii ishu? Mwenyewe ni Kama wewe icpokuwa nilikosa ujasiri wa kuanza mchakato sababu bado sijamaliza mwaka, vipi Naweza nikapata mkuu?
 
Ok boss
 
Mwalimu Jifunafu nipe taarifa Mwalimu mwenzio nataka niingie bank, VP ulifanikiwa
 
Ushauri mzuri huu.
 
Tulia soma fursa za eneo kwanza naamini mpaka ukipata uthibitishe tayari utakuwa ushajiweka sawa kimtazamo na fursa
 
Reactions: Yhy
Nyongeza tu;

1) Usikope kuanzisha biashara mpya, utajuta. Najua hamasa ya kiu ya mafanikio uliyonayo na hali ngumu kutokana na mshahara mdogo usiolingana na mahitaji, ila narudia tena, tafadhali sana usikope ili kuanzisha biashara mpya. Utanikumbuka.

2) Kwakuwa huna barua ya kuthibitishwa, kuna jamaa flani wa taasisi (siyo bank), herufi ya kwanza ni B na herufi ya mwisho ni T, tafadhali sana usije shawishika kukopa huko. Utalia machozi ya damu kwa riba zao.

3) Kopa tu endapo ni shida ya kutatua kifo cha mtu au unataka kumwokoa mtu asifungwe.

4) Endapo utalazimika sana kukopa kwa hao jamaa maana wana ushawishi mkubwa na wanapenda sana walimu, basi chukua mkopo wa muda mfupi sana kutatua hiyo shida, let's say mkopo usiozidi miezi mitatu tu.

5) Utanikumbuka. Narudia tena, utanikumbuka.
 
Reactions: Yhy
1. Hongera kupata ajira
2. acha njaa, mpaka upate barua
 
Kakope kote! Ila ukijiroga tu kuingia kwenye 18 za Bayport, Platinum credit, Finca, Faidika, au taasisi yoyote ile ya kifedha! Badala ya benki kama crdb, nmb, nbc, tpb, nk basi ujiandae kuishi kama shetani.
 
Mkuu mbona naona kama Mshahara kiduchu?
Huyo ni Mwl wa Level ipi?
 
Dah!
Kuna watu huwa hawajionei huruma kabisa.
Huyu itakuwa ni wale watu akiona tu hela mate yanamtoka hatakama hakuwa na ulazima wa kukopa atakopa ilimradi tu uwezeiano wa kukopesheka upo.
Mtiti unakuja hela zikiisha halafu bado anatumikia madeni anavyotia huruma sasa.
Halafu hawakomagi atarudia tu.
Mungu niepushie
 
Hahaha ila sheria hawez kattwa ziaid ya robo tatu ya mshahara wake akifika hapo Wana goma Wana Sema hakatiki labda akope kwa watu wa kulipa kesh ila kwa kutumia check no haita wezekana
 
Hahaha ila sheria hawez kattwa ziaid ya robo tatu ya mshahara wake akifika hapo Wana goma Wana Sema hakatiki labda akope kwa watu wa kulipa kesh ila kwa kutumia check no haita wezekana
Wewe ni mtumishi?
 
Amen , huwa nakopa pale tu najua kuna deal flani hela imechelewa ila imo inakuja.
Vingine najifiaga na tai shingoni.
 
Mkuu mbona umeongea point mbofumbofu sana leo? Huwa nakuaminia sana lkn leo umeniangusha. Kukopa kupo, hata akina mo wanakopa. Cha msingi mshauli mtu namna ya kuutumia mkopo.
Sio kila mtu ana mali ambazo anaweza kuuza akapata hela nzuri.
Matajiri wote duniani wana mikopo.

Sisi matajiri tuna msemo wetu wa mikopo" use other people's money to create your wealth'

Hizo za mikopo ndio pesa za wengine wanahifadhi benki.Benki wamekuwa watu wa kati tu yaani middlemen.

Ukikopa ukafanya anasa na kununu la liabilities imekula kwako unajiweka kwenye utumwa.

Ukikopa ukaweka kwenye investment utakuja jishukuru baadae.

Mwaka jana nilikopa hela ndefu nikaweka kwenye investment fulani na mwezi huu naanza pata returns zangu. Ni lifetime returns unless otherwise.

Kopa wekeza somewhere utajirike, au kopa kat.om.bee.eee ndio utajiua kuwa hujui.[emoji2][emoji3577]
 
Ukishapata barua ya kuthibitishwa nenda NMB watakuelekeza.

#YNWA
 
Sentensi ya mwisho inaonyesha wazi wewe ni kula kulala kwa shemeji yako tena graduate usiyekuwa na ajira ya kueleweka mzee wa vizinga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…