HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Yes, kinachomharibia zaidi ni tamaa na haraka ya maisha
Yah hapa sikupingi kaka..ila nimeshafanya self evaluation nimeona mahali nilipokosea hela nilipoipokea niliona kubwa so karibia million5 ikaishia kununua vitu vya ndani na nguo na kiasi kidogo nikapeleka kwa biashara ila sikuwa seriously japo
 
Kusimamia biashara mpya huku umeajiriwa ni changamoto hasa hizi biashara uchwara uchwara!!

Utanufaisha watu tu,halafu umeongeza na ulevi juu.
Ulevi nilikuwa nakunywa nikaacha mimi nina pombe sijaiendekeza ila kwa sasa ndo nimezidisha japo kuacha ninaweza ninashukuru Mungu ananipa Hekima ya kuweza kuacha addicted yoyote ila kinachoniumiza kichwa mke wangu ni mpuuzi sana amekuwa kama mzigo
 
Yah hapa sikupingi kaka..ila nimeshafanya self evaluation nimeona mahali nilipokosea hela nilipoipokea niliona kubwa so karibia million5 ikaishia kununua vitu vya ndani na nguo na kiasi kidogo nikapeleka kwa biashara ila sikuwa seriously japo
Hata hapa unapotaka kuanzia, punguza matarajio sana na acha vitu viflow taratibu ndani ya mipango yako
 
Ulevi nilikuwa nakunywa nikaacha mimi nina pombe sijaiendekeza ila kwa sasa ndo nimezidisha japo kuacha ninaweza ninashukuru Mungu ananipa Hekima ya kuweza kuacha addicted yoyote ila kinachoniumiza kichwa mke wangu ni mpuuzi sana amekuwa kama mzigo
Huyo mke ana tabia kama zipi mkuu? Tunaweza kuwa na cha kukushauri kabla hujachukua maamuzi yoyote juu yake
 
Yes, kinachomharibia zaidi ni tamaa na haraka ya maisha
Hili ni tatizo linalowasibu hasa vijana. Wanaharakia maisha. Mtu anaajiriwa ndani ya mwaka anatamani amiliki jumba la kifahari, awe na gari ya gharama, aendeshe miradi ya mapesa mengi mengi, matokeo yake anakopa kopa bila mipango sahihi anaishia kuanguka.

Jifunzeni kusubiri
 
Huyo mke ana tabia kama zipi mkuu? Tunaweza kuwa na cha kukushauri kabla hujachukua maamuzi yoyote juu yake
Mke nishawqhi kueleza kwenye hii thread ni mtu anayependa makuu.
Mfano sio mtu wa kupanga bajeti vitu yaani yeye anaweza kumwachia hela ya matumizi lakini ukakuta ametumia ovyo na hakuna cha maana kipo ndani.

Yeye anajifanya mtu wa fashion.

Pia sio mtu wa kujishughulisha na lolote hata ukimshauri ni kama ameridhika na haya maisha
 
Pole mkuu Maisha ni Kukomaa lakini wewe mwenyewe unasema uliingia shoti sababu ya UZEMBE WAKO MWENYEWE kwahiyo tatizo sio biashara tatizo ni wewe either katika ufwatiliaji au mambo mengine. Biashara yoyote inahitaji DISCIPLINE Kuwa Makini na Madeni Angalia Ulipodondoka Uinuke Usirudie Makosa!
 
Subra ni muhimu sana kwenye maisha,
na kila kitu kwenye maisha lazima kipitie kwenye mchakato wa muda na sio kukurupuka tu.
 
Na hela ya mkopo sio ya kuanzisha biashara au kujenga au kununua gari noo

kupa kwaajili ya kuendeleza biashara.. Am I right?
 
Hapo unaona hiyo laki saba nyingiii hadi unaisema na ndio lengo kuu la kuandika ivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…