Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)


Kwa ufupi sijamaliza kulisoma bandiko lako lote zaidi ya mistari minne ya mwanzo ila nimebaini limezungumzia kutegemeana kwa kila kitu katika mazingira yake kama chanzo na sababu ya uwepo wake.

Lakini pia Mungu nae kumbe nikama binadamu tu na upo uwezekano wa kuishi na kufa kama sisi (kinachotutofautisha na kila kinacho-exist ikiwemo Mungu mwenyewe pengine ni lifespan tu na occupancy).

Ikiwa viungo vya mwili wa binadamu ikiwemo organ zake ufanya kazi kwa ajili ya Mungu wao(MTU) vile vile hata sisi ufanya vyote kwa ajili ya Mungu wetu na yawezekana kama ilivyo viungo vyetu vya ndani pengine na sisi tupo ndani ya huyo Mungu na huu ulimwengu wote ni part ya mwili wake(nirekebishe kama sijakuelewa vizuri)

Kama niko sawa uoni kama hizi ni imaginations tu na nadharia zisizo na mashiko ya kuwepo humu jamii intelligence kama uthibitisho juu ya uwepo wa Mungu?
 
Kabla sijaendelea niweke wazi kuwa huu ni uthibitisho wa uhalali wa lile wazo la Mungu. Yaani the idea of God is sensible and not otherwise. Kwenda kinyume na wazo hili ndio utakuwa humake sense Kong Chi

Undava King tuchukulie mfano huohuo wa organs. Organs ndani ya miili yetu zipo limited in terms of space haziwezi kujongea hapa na pale. Labda humo ndani zinaambizanaga kuwa yule anayezibeba [Mtu] yeye ana uwezo wa kwenda popote anapotaka yaani ana uwezo wa ajabu. Yupo nje ya space na yupo pote katika space hata kwenye hivyo viungo yumo. Kiungo cha ndani kinawaza kuwa laiti kama ningeweza na mie kuwa naweza kwenda kila sehemu yaani ningefurahi acha tu. Sasa kuna namna mbili za kuachieve hiyo hali:

a. Kujiyeyusha na kuwa kama liquid fulani itakayosafirishwa na damu kuenea mwili mzima hadi ngozi, macho masikio. Lakini tunaona hili halitamfaidi chochote maana atakuwa hana organization ya yeye ni kama amekufa. Kwa hiyo kutaka kutoboa ki material material ni futile haisaidii. Mwili wa mtu ukifa unaoza halafu zile atoms zake [mnaita virutubisho] vinaishia kutawanyika dunia nzima kwenye funza, miti, bacteria na wanyama.

b. Kuongeza tu ile awareness yake na kuweza kuinteract na mazingira kama ambavyo mtu anainteract na mazingira hayo. Hawezi moja kwa moja bali ni mpaka aungane na awareness ya mtu mzima! Akifanya hivi huyo organ atafaidi na atakuwa kila sehemu ambako mtu anafika pote ndani na nje. Kumbe ili kuweza kuinteract na mungu wako inabidi ukubaliane naye katika hali ya utambuzi na sio material. Na ili kufanikiwa ni mpaka yeye akubali kukukaribisha kwake. Na unakaribishwa kwake unapokuwa na sense anazozikubali yeye.

Kwetu sisi watu tatizo letu ni muda. Labda ndo na sisi tunapowaza kuhusu muda; Mungu yupo nje ya muda na ndio maana tunatamani kwenda kwake ili tuweze kuishi milele katika raha bila kudhibitiwa na muda. Dini zote zinasolvu hichi kitu, zinampa mtu some form of imortality. To be not bound by time or space whatsover. Na hii ni kama tu utakubali katika akili yako kutenda ya kumpendeza Mungu ili akukaribishe kwake. Mungu yupo juu ya muda. Hafi. Kufa ni kama muda kukuishia, sasa nje ya muda hakuna kifo. Usiongelee mambo ya lifespan kwenye milele.
 
Kama niko sawa uoni kama hizi ni imaginations tu na nadharia zisizo na mashiko ya kuwepo humu jamii intelligence kama uthibitisho juu ya uwepo wa Mungu?
Nakubaliana kuwa hii ni nadharia, na nakubalinkuwa ni imagination. Ila kwenye suala la kutokuwa na mashiko hapo hapana. Hii mifano ndiyo mashiko yenyewe.

Au unaweza nijibu kuwa ni kwa nini katika kila jamii kulikuwa na hili wazo la Mungu bila kufundishwa na mtu yeyote?. Watu wenye intelligence siku zote wanazo imagination zinazotokana na kilichopo na kuextend to infinity [infinity ikiwa ni kutegemeana tu na kinachoweza kujulikana kwa wakati huo]
 
Ukifuatilia uingiaji wa mimba,mtoto akiwa tumboni,mpaka anazaliwa
Utagundua mungu yupo
Hii mimi huwa nachukulia kama simulation ya kuanza kwa ulimwengu.

Kama ambayo mwanzo kulikuwa na kanuni na maelekezo tu katika seli ya kwanza iliyorutubishwa. Lile wazo na kusudi na kanuni iliyokuwapo hiyo ndiyo ikaamuru seli zote zije, ikaamuru moyo uwepo, macho yawepo, miguu iwepo, ubongo uwepo kila kiungo na viungo kiwepo ili vitumikiane vyenyewe na kwa kufanya hivyo vimtumikie yeye 'mtu'. Kanuni zilezile zilizoratibu uanzishwaji wa mwili ndizo hizohizo zinazotumika kuuendesha.

Ulimwengu nao vivyo hivyo: labda
 
It seems that you are not a real scientist
 
It seems that you are not a real scientist
You know what sir. There is no need to limit oneself in a single field wakati zipo field nyingi tu. Sio vibaya mtu akawa kawa mwanasayansi, muumini, mwanasiasa na mwanafalsafa. Life requires the harmonious working together of........ of aaa..--- of kila kitu tu😂😂
 
Ndio maana nimekwambia you are not a real sciencitist because you believe on the absurdity of young Earth
 
Hili suala la mwanabaiolojia kuwa na dhana ya uwepo wa kitu kama "nafsini" au roho linatisha sana. Baiolojia sio mambo yasiyopimika au ya kutungatunga tu. Huwezi kufikia hitimisho la ajabu kama kwamba mungu yupo bila kiunganishi cha moja kwa moja na kinachopimika kwa yeyote atakayejaribu kuchunguza tatizo husika ili lithibitike.

Hakuna consensus ya mambo ya imani sehemu yoyote duniani. Kuna shida sehemu. Shida kubwa.
 
Ongea na Mungu mwambie kule Ukraine watu aliowaumba Putin anawaua kinyama bila huruma yoyote. Mbona Mungu kanyamaza!
Nimekua interested kidogo na hili; why unapenda Mungu aingilie kati anayo yafanya Putin lakini hukufikiria Mungu aingilie kati mauaji yanayo tokea barani Africa, mashariki ya kati nk, why only Ulaya!?
 
Ndio maana nimekwambia you are not a real sciencitist because you believe on the absurdity of young Earth
Why would I. Understanding of true science, true knowledge never contradicts with the Truth of spiritual things. Being a believer of Creator God doesn't automatically make me young earth believer. Make no assumptions. I may make statement such as evolution is the method God used to bring us into being us.

There is no contradiction because everyday we see cells dividing into organs into baby humans which develop into rational thinking humans. No human just pops into existance as full grown human! why not evolution? Look I dont apeal to evolution or no evolution, I don't appeal to creation or no creation ----I only appeal to sense
 
Labda nisaidie lengo la kitu chochote unalipimaje. Je unaweza kusema hilinhapa ndio lengo, lina kilo nne, linatokeza umeme wa millivolt tatu? unaweza? unalipimaje lengo?

Chochote kinachoundwa kinaundwa kwa ajili ya lengo fulani ambalo halishikiki wala halina asili inayofanania hicho kitu mzee. Kitendo cha hicho kitu kuwepo ndio uthibitisho wa lengo la kuwapo kwakee
 
Kazi ya sayansi ni kufanya utafiti kwa manufaa ya mwanadamu. Kisanyansi mambo yote kwenye taaluma huanza kwa msingi wa swali (tatizo) na kutaka kujua au kuelewa suala husika, hii ni kazi ya kwanza na msingi ya sayansi. Kazi ya nyongeza baadae kwa sisi binadamu ni kufanyia kazi elimu na maarifa kurahisisha maisha duniani. Application follows behind knowledge and discovery. Evolution ya wanyama haina lengo. Utasemaje natural selection ina lengo mahsusi wakati ni random process?

Ukizusha suala la mungu ni kuongeza tatizo badala ya kutoa suluhisho. So mungu sio hitimisho sahihi kwa sababu ya kukosa ushahidi wa uhusiano.
 
Logical non sequitur after logical non sequitur.

If any complexity must be created by a higher complexity, that shows there is no God, not otherwise.
 
Evolution ya wanyama haina lengo. Utasemaje natural selection ina lengo mahsusi wakati ni random process?
Angalia, bila lengo la kutengeneza kitu tata kitu hicho hakitokei. Sikia bila lengo unaweza tu kutengeneza kitu rahisi, I mean kitu sahili at best. Kiukweli mara nyingi random processes huwa zinatusaidia kuharibu mifumo tata iliyopoteza lengo la kuwepo kwake.

Mfano mzuri ni kiumbe anapokufa, I mean pale uhai unapoondoka, nafsi inapouacha mwili kinachotokea ni kusambaratika tu kutokana na kwamba lile lengo la kuwepo kwa mfumo ndio limeshaondoka. Hata kama mishipa ipo, ubongo na moyo upo kila kitu kipo lakini bila lengo kuu la kuwepo kwake --- vyote vinaoza. Moyonhauwezintu kuamua kuendelea kupampu damu kupeleka kwenye ubongo bila sababu ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…