Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nikikwambia kuna rangi ambayo haipo utakubali ipo?Nilimuahidi mfano whiteskunk lakini nadhani utaleta mwanga pia kwa akina Kiranga na masdinero masproblemas mfano wenyewe ni;
Imagine dunia au ulimwengu mwingine ambapo wao kutokana na miale ya jua lao kuwa hafifu [au kuwa na spectrum nyembamba] wanaona vitu kama gizanigizani tu kwa hiyo wanaonaga vitu bila rangi yaani black&white tu.
Bahati nzuri mtu kutoka duniani akafanikiwa kuwatembelea akafika akataka kuwaelekeza hii idea ya 'rangi' atawaelekezaje wamuelewe? Akiwaambia kuna nyekundu/bluu/kijani watamuona anazingua tu. Hata kama yeye anaweza kuwa anaziona kihafifuhafifu kutokana na kuishi sana duniani. Kwa watu wa kule ambao hawajawahi kuona rangi atapata tabu tu. Wabishi watakataa tu na akizidi watampiga mawe. Na wanasayansi wao wenye nia njema ya kuthibitisha watamtaka awapelekee ushahidi na hayo maelezo yatoshe katika black and white[B&W] tu! Imagine kuielezea nyekundu katika lugha yenye B&W tu. Huyu jamaa akirudi duniani akachukua maua mekundu na ya njano akapeleka akiyafikisha wakayatazama watacheka halafu watasema. Hii unayosema nyekundu ni kwamba ina weusi zaidi ya hili unalosema la njano hakuna cha rangi wala nini hapo. Na hilo neno njano na nyekundu umetunga tu.
Ili aweze labda amchukue mtu wa huko amlete duniani azione rangi halafu akirudi naye anaweza kuanza kuappreciate idea ya rangi na kuwaelekeza wengine. Sio lazima aje duniani lakini akiwa na imani akakubali kujifunza na akaelewa anaweza naye kuappreciate idea ya rangi. Ndugu zangu huu ndio ugumu wa kuleta uthibitisho wa uwepo wa mambo ya kiroho kwa watu ambao wanachukulia haya material ndio halisi na ndio kitu pekee kilichopo, black and white.
Mfano wako wa rangi hautusaidii kitu.
Kwa sababu unatuambia kuna uwezekano wa kuwepo vitu tusivyovijua.
Hautuambii jinsi ya kutenganisha vitu ambavyo vipo kiuhalisia na vile ambavyo ni vya kufikirika tu havipo nje ya ulimwengu wa kufikirika tu.