Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
- Thread starter
- #101
Sema wewe kwamba mtu ni nani au ni nini ndipo ili tujue tunaanzaje kuthibitisha kulingana na vigezo utakavyosema maana umeipuuzia tafsiri yangu na uthibitisho wangu.Kwa nini unakuja kwa mtu kama hujaweza kujithibitisha wewe upo?
Kiranga tunatofautiana kitu kimoja tu. Ni kwamba mimi kwangu wazo ni 'kitu halisi' kabisa ila kwako sina hakika kama unaamini hivyo.
Maana mimi nilipojithibitisha kwa kusema kuwa nilipogundua ninawaza kuwa mimi ni nani nikagundua kuwa mimi nipo maana mtu ni wazo hai.
Uthibitisho wake ni kule kuwepo kwa hilo wazo hai linalowaza hayo yote. Wazo ni 'kitu halisi' kwangu. Kama ambavyo wewe unasema hili ni gari, huyu ni panzi. Na mimi hivyohivyo ninasema mtu ni lile wazo la yeye.
Tena hata tunaposema kitu halisi inaonesha tu upungufu wa lugha inayojitosheleza ya kuelezea vitu visivyoshikika. Mimi kwangu kitu kiwe kinashikika, kiwe hakishikiki ikiwa kinaonesha athari kwa maisha na vitu hicho ni kitu halisi kabisa