Mimi ni mwanaume ninayeonewa na mke wangu, Dkt. Gwajma nisaidie

Naomba hili jukwaa liwe msaada kwangu wadau.Mpaka nakuja hapa nipo na shida wakuu nisaidieni.
 
Mwalimu wewe umekuwa wa kulialia na wanawake ? mbona enzi unafundisha Matipwili Sec haukuwa hivyo ? ukiona mwanamke anakusumbua achana nae !
 
Kwanza acha kujiita mwenye kipato duni Mtumishi, amua Leo unatamani ufanye nini ukuze hicho kipato

Lingine, kumbuka na ijue nguvu ya kuwa baba katika familia uliyoiunda

Kuna uwezekano umeteleza sehemu hasa unapojiita na kujiona mwenye kipato duni hapo ndipo unapoharibu...

Kuteleza siyo kuanguka, inuka kubali kuanza upya na itafute nguvu yako hasa ya kifedha atakuheshimu tu'
 
Hanipigi ila kamtoa mtoto shule kwa kudangqnywa.Nilipanga nimdhuru ila nimeleta na kuomba msaada hapa wadau.Naomba mumtagi waziri Gwajma. Mimi nimeamua kuleta malalamiko hapa mana naamini waziri yupo hapa na wadau wote mpo hapa

Umefanya vizuri kulileta hapa jukwaani pia nimefurahi kuona namba ya mhushimiwa waziri.
Naomba Sasa tuwe tuna mcheki moja Kwa moja mh waziri kwaajili ya taarifa na ushauri
Ningependa pia tusiwakatishe tamaa Wadau wanao hitaji msaada kwa kejeli au vijembe. Kila mmoja ana namna yake ya kuwasilisha ujumbe kwa hiyo tuheshimiane na tuvumiliane. Ni ushauri tu wadau
 
Mi nimechukulia hivyo kama mwalimu wa kijijini. Hayo mengine siyajui mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…