Mimi nilifanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013, wewe je?

Mimi nilifanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013, wewe je?

View attachment 3093104

Ikiwa siku ya leo wadogo zetu wapo katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, nawaombea wamalize salama na wafanikiwe kuwapa faraja wazazi wao kwa matokeo mazuri.

Binafsi nilifanya mtihani huu mwaka 2013, share nasi ni mwaka gani ulimaliza elimu ya msingi...
Nilifanya mtihani Mwaka 2019.
 
Mimi nilifanya 2005
Darasa la Majaribio hili.
2001 Mungai alifanya yake akaondoa masomo Kama sita hivi kwenye mtaala akaja na Maarifa ya Jamii.

2006 mkiwa form One mnakutana na Physics with Chemistry ghafla waziri mpya mama Sita akarejesha mtaala wa zamani wa 1997.

Ndiyo darasa lililoanzisha shule za kata kwa wingi nchini mkifundishwa na waalimu waliosomea ualimu kwa miezi miwili tu @ Walimu wa Vodafasta.

Ndiyo darasa la kwanza mlionufaika na mkopo kwa wingi sana baada ya maandamano ya kaka zenu huko vyuoni.

2010 mnaingia form Five mnakutana na mtaala mpya kwenye combination za Arts mwathirika mkubwa akiwa English.

Mnamaliza Chuo Kikuu 2015/2016 mnakutana na zee moja la ajabu likazuia ajira za utumishi wa umma for 4 years.

Licha ya darasa hili kuwa na wanafunzi vipanga wengi kwenye kila category ndiyo darasa la watu waliostruggle sana kupata ajira za utumishi wa umma mpaka Sasa kuna baadhi wapo mtaani wanahangaika na ajira portal in their late thirties.
 
Back
Top Bottom