Mimi si Mwanasiasa, ila kwenye hili la Tozo hapana

Mkuu ipo hivi.
Tanesco walisema ili kupata umeme unatakiwa kulipia Zaidi ya 2,000 ili 1,000 ulipie pango kwa mwezi wa saba na 1,000 nyingine tena italipia pango kwa mwezi huu wa nane.
Hivyo ukitaka kupata umeme unalipa labda 3,000 ili wakikata 2,000 yao utabakiwa na 1,000 na hiyo ndo itatumika kununua Umeme.
Lakini mimi na majira pamoja na wadau wa karibu hata ukilipia Umeme wa 4,000 inagoma mpaka ulipe 5,000 au zaidi.
Imeanza lini mkuu!
 
Mama tunakuomba upanue wigo wa tozo. Kuna watu wanamusemasema huku.

Nyoosha nchi mama yetu. Usiwaogope wanaopinga mtandaoni. Waambie kama wanataka tusikie waende TBC waombe kipindi wakasemee huko.
 
Kwahiyo watakuwa wanakata kila mwezi au kila ukinunua luku wao wanafyeka
 
Kila mwezi utakatwa sh.1,000 kwa Nyumba za kawaida na Sh.5,000 kila mwezi kwa wenye appartment
 
Mama tunakuomba upanue wigo wa tozo. Kuna watu wanamusemasema huku.

Nyoosha nchi mama yetu. Usiwaogope wanaopinga mtandaoni. Waambie kama wanataka tusikie waende TBC waombe kipindi wakasemee huko.
Mkuu mungu anakuona
 
Jifunze kuandika kiswahili sanifu japo najua nyie Wasukuma huwa hamna "r" ! Nilopoke × Niropoke√
Msifikili× Msifikiri√
Kwa taarifa yako tozo ni mbadala wa fedha za dhuluma alizokuwa akikusanya Mwendazake kupitia task force zake na wale watu wasiojulikana!
Wewe umemsikia tena Paulo Makonda akitutambia anavyokula raha kuliko wote duniani?!
 
Inatuhusu hata sisi wenye umeme wa REA kwenye nyumba zilizoezekwa kwa nyasi vijijini?!
Kwani hukujua kwanini kufunga umeme ni Tsh. 27,000/= pekee.

Tozo zikionekana zinafaa mwakani tutapanua wigo. Kufunga umeme ni bure, ili tufikie 90% ya nyumba zote. Then tunaweka tozo fixed rate ya 5000 kwa mwezi kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Inawezekana sana.
 
Huna akili.
 
Mwache mama yetu afanye kazi. Kama hukubaliani na maamuzi yake subiri kipindi cha uchaguzi uchague unayeona ataweza kuendeleza nchi bila kodi na tozo.
Mzee mpili yamekuwa hayo tena
 
Kwani hukujua kwanini kufunga umeme ni Tsh. 27,000/= pekee.

Tozo zikionekana zinafaa mwakani tutapanua wigo. Kufunga umeme ni bure, ili tufikie 90% ya nyumba zote. Then tunaweka tozo fixed rate ya 5000 kwa mwezi kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Inawezekana sana.
Dah ila hawa watoto ambao hawajawa na majukumu shida sana.
 
Jifunze kuandika kiswahili sanifu japo najua nyie Wasukuma huwa hamna "r" ! Nilopoke × Niropoke√
Msifikili× Msifikiri√
Kwa taarifa yako tozo ni mbadala wa fedha za dhuluma alizokuwa akikusanya Mwendazake kupitia task force zake na wale watu wasiojulikana!
Wewe umemsikia tena Paulo Makonda akitutambia anavyokula raha kuliko wote duniani?!
Nimekuelawa mha
 
Wakuu najua uzima upo wa kutosha sema mtakuwa na stress za Tozo tu nyie. Baada ya kuwasalimu ngoja kidogo na mimi nitie neno.

Binafsi mimi si Mwanasiasa wala sijawahi kushabikia chama ila kwenye hili ngoja na mimi nilopoke kidogo.

Awamu hii ya sita ambayo inaongozwa na mama shupavu kwango kama sijaelewa maana uzoefu wangu unakinzana na niliyo yaona awamu ya tano.

-Awamu ya tano hapakua na ongezeko la tozo za Miamala, ila awamu hii tutaimba ule wimbo pendwa wa chama tawala Wacha waisome namba.. hapa si chama pinzani bali sote.

Pia kwenye hili naona chama kilichopo kimeamua kutunyonga kwenye ulipaji wa Pango japo wanasema eti unalipia Zaidi ya elfu mbili Unapata Umeme, lakini ukilipa chini ya 5,000 kupata umeme sahau.

Kumbuka haya yote ni awamu hii, pia nikiangalia mama yeye hasemi sana kuhusu haya wapo mawaziri wake yeye busy na kusafiri.

NB: Tulio pinga awamu ya 5 na kuanza kushabikia awamu hii msifikili imewasahau nawacheki tu.
Sina mengi ila tutaisoma namba kiukweli na Yajayo yanafurahisha mko tayari wananzengo?

Watu wengine hivi tozo ni hobby kama mpira? Hakuna tuzo nzuri au mbaya nenda kaishi EU uone hizo kodi wanazolipa
 
Umeandika vizuri, lakini naomba ukumbuke nchi itajengwa na wananchi. Hatutaweza weza kuona manufaa ya hizi tozo ndani ya mwezi mmoja au miwili lakini manufaa ni makubwa japo yanamaumivu.

Uwekezaji wa tozo hizi ni kwenye huduma za afya, elimu na miundo mbinu vijijini. Ndugu zetu vijijini wana hali mbaya sana kuna maeneo wanafunzi wanatembea zaidi ya km 10+ kufuata elimu kwa sababu ya uhaba wa shule kwenye maeneo ya karibu hata shule ikiwa karibu bado kuna mlundikano wa wanafunzi darasa moja wanafunzi 150+. Vilevile upande wa afya kuna kata mpaka leo hazina vituo vya afya watu wanalazimika kusafiri zaidi ya km 10+ kufuata huduma hii pia kwa kupitia barabara mbovu ambazo ni mateso kwa hasa kwa wamama wajawazito.

Tumekuwa tukilalamika serikali haitoi ajira, naimani kupitia tozo hizi, ujenzi wa vituo vya afya, kuongezwa kawa madarasa na hata shule mpya kutatoa fursa za ajira mpya serikalini. Waajiriwa wapya kupitia mishahara wataongeza mzunguko wa fedha na purchasing power kwenye maeneo watakayoajiriwa.

Vilevile kuongezwa kwa tozo ya mafuta kutaupa nguvu mfuko wa barabara vijijini TARURA, kutawezesha movement ya bidhaa za viwandani na mazao kusafirishwa kwa urahisi na kupunguza mfumuko wa bei uliokuwa unachangiwa na ubovu wa barabara. Pia hata watoa huduma kuwafikia wananchi wao kwa ukaribu na wananchi kuyafikia maeneo ya kutolea huduma kwa urahisi.

Pia tukumbuke kazi zote hizi za ujenzi wa vituo vya afya na mashule / madarasa kandarasi wanapewa wananchi wenye sifa. Hivyo pesa itarudi kwa wananchi kupitia ajira za vibarua, usambazaji wa vifaa vya ujenzi kwenye vituo vya afya, shule mpya.

Cha muhimu value for money iwepo, wakurugenzi wabanwe kuhakikiksha uwazi wa matumizi ya hizi fedha unaendana na thamani.
 
Watu wengine hivi tozo ni hobby kama mpira? Hakuna tuzo nzuri au mbaya nenda kaishi EU uone hizo kodi wanazolipa
EU wanalipa kodi na matokeo ya hizo kodi yanaonekana tofauti na huku kwetu. Huwezi kumkamua mwananchi maskini kutafuta hela kuwajengea mahekalu marais wastaafu. Ni ushetani.
 
Back
Top Bottom