Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
- Thread starter
- #41
Ila wameanza kwa kunyonga pakubwa sana mkuu mimi nafkria unyama walio nifanyia leo.Umeandika vizuri, lakini naomba ukumbuke nchi itajengwa na wananchi. Hatutaweza weza kuona manufaa ya hizi tozo ndani ya mwezi mmoja au miwili lakini manufaa ni makubwa japo yanamaumivu.
Uwekezaji wa tozo hizi ni kwenye huduma za afya, elimu na miundo mbinu vijijini. Ndugu zetu vijijini wana hali mbaya sana kuna maeneo wanafunzi wanatembea zaidi ya km 10+ kufuata elimu kwa sababu ya uhaba wa shule kwenye maeneo ya karibu hata shule ikiwa karibu bado kuna mlundikano wa wanafunzi darasa moja wanafunzi 150+. Vilevile upande wa afya kuna kata mpaka leo hazina vituo vya afya watu wanalazimika kusafiri zaidi ya km 10+ kufuata huduma hii pia kwa kupitia barabara mbovu ambazo ni mateso kwa hasa kwa wamama wajawazito.
Tumekuwa tukilalamika serikali haitoi ajira, naimani kupitia tozo hizi, ujenzi wa vituo vya afya, kuongezwa kawa madarasa na hata shule mpya kutatoa fursa za ajira mpya serikalini. Waajiriwa wapya kupitia mishahara wataongeza mzunguko wa fedha na purchasing power kwenye maeneo watakayoajiriwa.
Vilevile kuongezwa kwa tozo ya mafuta kutaupa nguvu mfuko wa barabara vijijini TARURA, kutawezesha movement ya bidhaa za viwandani na mazao kusafirishwa kwa urahisi na kupunguza mfumuko wa bei uliokuwa unachangiwa na ubovu wa barabara. Pia hata watoa huduma kuwafikia wananchi wao kwa ukaribu na wananchi kuyafikia maeneo ya kutolea huduma kwa urahisi.
Pia tukumbuke kazi zote hizi za ujenzi wa vituo vya afya na mashule / madarasa kandarasi wanapewa wananchi wenye sifa. Hivyo pesa itarudi kwa wananchi kupitia ajira za vibarua, usambazaji wa vifaa vya ujenzi kwenye vituo vya afya, shule mpya.
Cha muhimu value for money iwepo, wakurugenzi wabanwe kuhakikiksha uwazi wa matumizi ya hizi fedha unaendana na thamani.
Kweli 5000 unit 1.
LUKU
37212843355
990022123320138178
1.5KWH
0029 2493 0496 3524 7260
Cost 409.84
VAT 18% 73.77
EWURA 1% 4.10
REA 3% 12.29
Debt Collected 4,500.00
TOTAL 5,000.00